Piga Kura: Mkuu wa Mkoa Bora 2018

Piga Kura: Mkuu wa Mkoa Bora 2018

Baadhi ya wakuu wa mikoa wameonekana kutekeleza vyema sera ya maendeleo na pia wameomyesha sura za kiuongozi katika maeneo yao.

Kati ya wafuatao yupi unadhani ji bora zaidi

1. Simiyu (Mtaka)
2. Tabora (Mwamri)
3. Geita (Gabriel)

Wamejitahidi sana kusimamia mambo yanayo igusa jamii. baadhi ya mambo ambayo wameyasimamia.

1. Robert Gabriel: Amesimamia fedha zinazo toka migodini (CSR) kwa kuhakikisha zinajenga zahanati kwa kila kijiji.

2. Mtaka : Ameonyesha uongozi kwanza kwa kupiga marufuku viongozi kuwekwa rumande bila sababu ya msingi.

3. Mwamri: Amesimamia vyema swala la ndoa za utotoni kwa mkoa wa tabora ndio unaongoza kwa ndoa za utotoni.

Yapo mengi lakini jambo la msingi ni uongozi wao umeonekana sio wa kukurupuka na kutaka kiki.

Piga kura yako.

Siku zingine uje na Swali la Je tunadhani ni Mkuu wa Mkoa gani anaongoza kwa Upopoma / Upumbavu ' Uliotukuka ' Tanzania nzima nadhani utaona jinsi Watu tutakavyoserereka na kutiririka kwa majibu ' mubashara ' kabisa bila Kupepesa macho, Kutikisa Masikio wala Kumung'unya maneno.
 
Mkuu wa mkoa wa Tabora sio tu ajenda yake kubwa ni mimba ,hapana agenda kubwa ya Mh.Mwanry ni mazingira.

Tangu amefika Tabora alianzisha kampeni ya kuboresha mazingira kwa kupanda miti kwenye kila barabara,kwenye Ofisi za serikali,taasisi binafsi na zile za dini nk.

Mpaka sasa mkoa umeotesha miti zaidi ya mil moja.

Ukifika Tabora kila kona unakopita unakutana na miti iliyohamasishwa na mkuu wa mkoa.

Chakufurahisha zaidi kila siku anamwagilia mwenyewe akiwa na wafanyakazi wa halmashauri.

Hatumi mtu.......jamaa anachapa kazi sana,sema hapendi media
 
Antony Mtaka yupo vizuri anapanga na kutekeleza! Tangu alipokuwa mkuu wa wilaya kule Mvomero hadi sasa yuko Simiyu kwa kweli anajitahidi sana!
 
Tukuulize kwanza hii shortlist uliipataje hata Baba Keagan akawa hayumo humu? Bila ya baba Keagan humu ni sawa na PL bila ya Yanga
 
Ole sendeka, mtaka flekelea mbali, mwanri flekeleaaaaaaa mbali esopo
 
Sijui vigezo ulivyotumia kuwa short list hao watatu pekee...Ila kwa ulioweka Mwanry anaongoza akifuatiwa na Antony Mtaka japo kila mmoja ana kipawa ambacho mwenzake hana!
 
Huyo wa geita umemuweka kwasababu amezuia watumishi kuvaa suti
 
Huu uchaguzi bila Makonda ni batili, uchaguzi urudiwe watu wapige kura upya
 
1. Eng. Ndikilo Pwani (kimia kimia)
2. Mtaka (media)
3. Makonda (matukio)
 
Baadhi ya wakuu wa mikoa wameonekana kutekeleza vyema sera ya maendeleo na pia wameomyesha sura za kiuongozi katika maeneo yao.

Kati ya wafuatao yupi unadhani ji bora zaidi

1. Simiyu (Mtaka)
2. Tabora (Mwamri)
3. Geita (Gabriel)

Wamejitahidi sana kusimamia mambo yanayo igusa jamii. baadhi ya mambo ambayo wameyasimamia.

1. Robert Gabriel: Amesimamia fedha zinazo toka migodini (CSR) kwa kuhakikisha zinajenga zahanati kwa kila kijiji.

2. Mtaka : Ameonyesha uongozi kwanza kwa kupiga marufuku viongozi kuwekwa rumande bila sababu ya msingi.

3. Mwamri: Amesimamia vyema swala la ndoa za utotoni kwa mkoa wa tabora ndio unaongoza kwa ndoa za utotoni.

Yapo mengi lakini jambo la msingi ni uongozi wao umeonekana sio wa kukurupuka na kutaka kiki.

Piga kura yako.
Nafikiri tungewapata kwanza wanaoongoza kukiuka sheria, kanuni na maadili ya kiuongozi katika nchi yetu.
 
Baadhi ya wakuu wa mikoa wameonekana kutekeleza vyema sera ya maendeleo na pia wameomyesha sura za kiuongozi katika maeneo yao.

Kati ya wafuatao yupi unadhani ji bora zaidi

1. Simiyu (Mtaka)
2. Tabora (Mwamri)
3. Geita (Gabriel)

Wamejitahidi sana kusimamia mambo yanayo igusa jamii. baadhi ya mambo ambayo wameyasimamia.

1. Robert Gabriel: Amesimamia fedha zinazo toka migodini (CSR) kwa kuhakikisha zinajenga zahanati kwa kila kijiji.

2. Mtaka : Ameonyesha uongozi kwanza kwa kupiga marufuku viongozi kuwekwa rumande bila sababu ya msingi.

3. Mwamri: Amesimamia vyema swala la ndoa za utotoni kwa mkoa wa tabora ndio unaongoza kwa ndoa za utotoni.

Yapo mengi lakini jambo la msingi ni uongozi wao umeonekana sio wa kukurupuka na kutaka kiki.

Piga kura yako.
Wote hapa ni hamna kitu
 
Nadhani mleta mada kakosea kidogo...kwa kuwa sifa namba moja inayotakiwa katika uteuzi wa maRC, maDC na viongozi wa serikali katika awamu hii ni ukichaa wao kwa kiwango cha mteuzi, swali lingekuwa mkuu wa mkoa yupi ni kichaa zaidi. Nadhani sisi sote ni mashahidi wa matamko ya kushangaza yanayotolewa na hawa watu, matamko ambayo yanaweza kutolewa tu na kiongozi kichaa.

Je yupi mkuu wa mkoa ni kichaa zaidi kuliko wote?
 
Back
Top Bottom