Kwenye mahusiano/ndoa watu hua wanapiga picha pamoja . . . kwaajili ya ukumbusho.
Kwa wale mlioko facebook mnajua siku hizi hizo picha haziishi kwenye album makabatini tu na ukutani ila mpaka mitandaoni unakuta mmoja ana picha kibao za mwenzake bila kusahau description za ohh huyu ndie. . baby wangu and so so.Nimeona mmoja kajaza kweli za girlfriend wake nikajikuta najiuliza kama siku wakiachana atazifutilia tu mbali au itakuaje.
Swali. . .je ikiwa mahusiano yatavunjika zile picha mlizopeana na kupiga pamoja zinatakiwa zifanyweje?Ni sahihi kuziweka tu?Zinatakiwa zitupwe/chanwe. . . kama jibu ni ndio je za harusi?Ni sahihi kweli kuharibu/tupa picha unayopenda kisa tu uliyeachana nae yumo?Na kama ukiweka kuna madhara?
ikitokea baby come back?Mkibwagana unachana chana na kuzifuta zote hata line za simu unavunja vunja hata simu yenyewe unaanza upya.
Hahahaha. . . Bishanga umenichekesha na hilo la nguo mpaka za ndani. Wengine wanaweza kuweka kumbukumbu kama bado anakupenda . . wengine wakadekia au mwagia mafuta ya taa na kuchomelea mbali.nyumbani kwangu nina sanduku maalum linakaa darini,humo nimejaza bad memories zote,siku nikipigwa chepe watakaobaki duniani watajua wenyewe nini walifanyie.Ila hata mimi huwa najiuliza hao mahawara ambao tuki differ huwa tunatelekeza huko nguo (mpaka za ndani) baadae huwa wanazifanyia nini?
ikitokea baby come back?
Yani mpaka simu ubadili kisa break-up?
Kwanini haswa?Wakati unaweza kufuta tu namba na kuendelea?
Honest sina jibu,ila ukweli ndo huo,situpi ila nazidi ku pile up,picha,zawadi,nguo,vidani,shanga,hirizi nilizokuta chini ya godoro, yaani we acha tu,ni sanduku kubwa.Hahahaha. . . Bishanga umenichekesha na hilo la nguo mpaka za ndani. Wengine wanaweza kuweka kumbukumbu kama bado anakupenda . . wengine wakadekia au mwagia mafuta ya taa na kuchomelea mbali.
Ila sasa wewe hiyo collection yako unaiweka kwa madhumuni gani haswa?Kumbukumbu?
iko siku utakutana na mwanaume wa shoka,kila mki break he will need only one phone call unamrudia mbio,,si unajua kila shetani na mbuyu wake?Aaaah wapi mi huwa siruhusu kitu kama hicho mkataba ukikatika basi nahama mpaka mtaa ili kupunguza bugudha
acha kusikilizia bana,mwaga ma uzoefu?enhee...am listening...:A S-coffee:
Honest sina jibu,ila ukweli ndo huo,situpi ila nazidi ku pile up,picha,zawadi,nguo,vidani,shanga,hirizi nilizokuta chini ya godoro, yaani we acha tu,ni sanduku kubwa.
Bishanga siku ukifa utaacha mzozo duniani lol!Honest sina jibu,ila ukweli ndo huo,situpi ila nazidi ku pile up,picha,zawadi,nguo,vidani,shanga,hirizi nilizokuta chini ya godoro, yaani we acha tu,ni sanduku kubwa.
Lizzy binafsi if we are done we are done.....
I want nothing to remind me of you, kwanza ili iweje?