Msinishangae bandugu!!!
mimi naona hawa viongozi wa serikali ya palestina hata hesabu rahisi kabisa zinawashinda. Mimi naamini ukiupigania uhuru unatakiwa uupate wewe unayeupigania ukiwa hai.
Manake haya ni maajabu ya binti chura!!! yaani waenda msituni wamchokoza kifafu, akikutoa nduki unakimbilia nyumbani kwako, unaingia kwa mlango wa mbele na kutokea mlango wa nyuma unasepa, kifaru akifika anawakanyaga kanyaga wanao ma mkeo, anawatia pembe watoto wa jirani yako na wanakijiji kwa ujumla,
Wewe unaibukia kwenye magezeti oooh! kifaru mkorofi, eti Kifaru hana chembe ya utu hata kidogo!!! kifaru anawaua watoto, Kifaru anaporomosha majumba ya wanakijiji.
Angalia sasa wameshawaponza raia wao zaidi ya 60 wameshauliwa na "kifaru"
wanavitumaini na kuvihusuuuuuudu vikombora wanavyovirusha kwenye pori la "kifaru" ambavyo havimdhuru kwa vyovyote huyu "kifaru"
Ni busara kwa wapalestina kujitambua kuwa kuna wakati haki yako inaweza kukuangamiza,
KWA NINI UFE KABLA YA WAKATI WAKO?