Tanzania Railways Corp
JF-Expert Member
- Mar 23, 2018
- 251
- 595
Picha hizi zinaonesha Maendeleo ya Ujenzi wa Stesheni za Dar es Salaam, Pugu na Soga. Katika kipande cha kwanza cha Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR ambao utakuwa na jumla ya Stesheni Sita ikiwemo Stesheni kuu mbili ambazo ni Dar es Salaam na Morogoro huku Stesheni ndogo (za kati) zikiwa ni Pugu, Soga, Ruvu na Ngerengere. Wastani wa Jumla wa Maendeleo ya Mradi Dar es Salaam - Morogoro ni zaidi ya 73%
Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa ya Dar es Salaam likiwa limeanza kuwekwa vioo.
Jengo la Stesheni ya Dar es Salaam limejengwa kwa muonekano wa Madini ya Tanzanite ambayo upatikanaji wake ni adimu, madini haya hupatikana Tanzania pekee.
Jengo la Stesheni ya Dar es Salaam limejengwa kwa muonekano wa Madini ya Tanzanite ambayo upatikanaji wake ni adimu, madini haya hupatikana Tanzania pekee.
Muonekano wa Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa ya Pugu, ambayo ujenzi wake umefika 80%
Moja kati ya Vituo vya kupokea, kupoza na kusambaza umeme utakaoendesha treni za Umeme eneo la Mpiji, kikiwa katika hatua za mwisho kuweza kukamilika.
PICHA; Muonekano tofauti wa Stesheni ya Pugu ambayo ujenzi wake umekamilika kwa 90%.
Majengo ya Stesheni za Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere ni ya kufanana yakiwa yamejengwa kiusanifu kuakisi Vazi la Kilemba ambalo ni maarufu kwa wanawake hapa Tanzania.
Majengo ya Stesheni za Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere ni ya kufanana yakiwa yamejengwa kiusanifu kuakisi Vazi la Kilemba ambalo ni maarufu kwa wanawake hapa Tanzania.