Picha za uzinduzi safari za treni jijini Dar es Salaam, Dr. Mwakyembe afanya uzinduzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha za uzinduzi safari za treni jijini Dar es Salaam, Dr. Mwakyembe afanya uzinduzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  A SAFARI ZA TRENI JIJINI DAR ES SALAAM, DR. MWAKYEMBE AFANYA UZINDUZI HUO
  TAZAMA PICHA 19 ZA UZINDUZI WA SAFARI ZA TRENI JIJINI DAR ES SALAAM, DR. MWAKYEMBE AFANYA UZINDUZI HUO


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]  Na Joachim Mushi, Thehabari.com

  USAFIRI wa kutumia treni jijini Dar es Salaam kutokea eneo la Ubungo Maziwa kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) umeanza leo. Treni ya kwanza imeondoka Ubungo majira ya saa 12:00 asubuhi kuelekea katikati ya jiji, ambapo kwa mujibu wa maofisa wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) imetumia wastani wa dakika 30 kufika katikati ya jiji.


  Treni ilioanza kazi leo iliyokuwa na injini mbili (vichwa vya traini) moja ikiwa imefungwa nyuma na nyingine mbele huku ikiwa na mabehewa sita, yaani matano ya abiria wa kawaida (watu wazima) na moja likiwa ni maalumu kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Abiria mmoja ni sh. 400 kwa tripu huku wanafunzi wakitakiwa kulipa sh. 100 kwa kila mmoja.

  Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndiye aliyezindua usafiri wa leo ambao ni wamajaribio, akiwa pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha Reli. Treni hiyo pia imezinduliwa pamoja na treni ya TAZARA ambayo itafanya kazi kama ya Ubungo, lakini yenyewe ikianzia eneo la TAZARA kuelekea Mwakanga.

  Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Waziri Mwakyembe alisema atahakikisha treni hiyo inaendelea kufanya kazi ili kuwasaidia kiusafiri wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kero ya usafiri hasa kwa foleni, ambapo utumia muda mrefu njiani kuingia na kutoka jijini.

  Alisema jumla ya mabehewa ya treni 14 pamoja na injini mbili zimekarabatiwa na mafundi wazalendo nchini, ambayo ndiyo yatakayokuwa yakifanya kazi ya kusafirisha abiria kuingia na kutoka jijini kila asubuhi na jioni. Alisema kwa sasa inafanya treni moja kwa majaribio lakini baada ya uzinduzi mkubwa zitafanya kazi treni mbili, na zitakuwa zikipishana njiani moja ikirudi na nyingine ikienda.

  Akifafanua zaidi alisema kitendo cha mafundi wazalendo kufanya ukarabati kwa mabehewa na injini kimeokoa kiasi kikubwa cha fedha za umma kwani ukarabati wote umetumia sh. bilioni 2.1 tu, ilhali kama Serikali ingelazimika kukodi injini gharama ingekuwa kubwa zaidi kwani bei ya kukodi injini moja ya treni ni sh. milioni moja kwa siku.

  Hata hivyoDk. Mwakyembe amewataka Watanzania hasa abiria kuwa wavumilivu kwa upungufu utakaojitokeza kwa safari za mwanzo kwani bado wanaendelea kufanya marekebisho kadhaa, lakini baada ya muda mambo yatakaa sawa. Mwandishi wa habari hizi alikuwa ni mmoja wa wasafiri walioizindua treni hiyo leo.

  Awali akizungumza mmoja wa viongozi waandamizi wa TRC, alisema treni hiyo itafanya kazi kila siku isipokuwa kwa siku za jumapili na siku kuu na itaanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa sita mchana na kupumzika hadi saa 9:00 za jioni, itakapoendelea tena na safari zake hadi majira ya saa nne usiku.

  Uchunguzi uliofanywa na muandishi wa habari hizi umebaini kuwa behewa moja la treni linauwezo wa kuchukua abiria 66 wakiwa wamekaa, lina milango minne, feni, taa, muziki/redio, pamoja na mikanda maalumu ya kujishikia kwa abiria ambao watakuwa wamesimama.

  Aidha mabehewa yote yana madirisha ya kutosha kuingiza na kutoa hewa ya kutosha. Treni ilioanza kazi leo, ikitokea Ubungo ilikuwa ikisimama vituo vya eneo la Mwananchi (relini), Tabata Relini, Buguruni Miamani, Tazara, Kariakoo Gerezani (Kamata), na mwisho Kituo Kikuu cha Treni kilichopo jirani na Kituo cha Polisi Kati (Katikati ya Jiji).


  *Imeandaliwa na mtandao wa Thehabari.com
  CHA 19 ZA UZINDUZI WA SAFARI ZA TRENI JIJINI DAR ES SALAAM, DR. MWAKYEMBE AFANYA UZINDUZI HUO


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]

  Na Joachim Mushi, Thehabari.com

  USAFIRI wa kutumia treni jijini Dar es Salaam kutokea eneo la Ubungo Maziwa kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) umeanza leo. Treni ya kwanza imeondoka Ubungo majira ya saa 12:00 asubuhi kuelekea katikati ya jiji, ambapo kwa mujibu wa maofisa wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) imetumia wastani wa dakika 30 kufika katikati ya jiji.​


  Treni ilioanza kazi leo iliyokuwa na injini mbili (vichwa vya traini) moja ikiwa imefungwa nyuma na nyingine mbele huku ikiwa na mabehewa sita, yaani matano ya abiria wa kawaida (watu wazima) na moja likiwa ni maalumu kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Abiria mmoja ni sh. 400 kwa tripu huku wanafunzi wakitakiwa kulipa sh. 100 kwa kila mmoja.​


  Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndiye aliyezindua usafiri wa leo ambao ni wamajaribio, akiwa pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha Reli. Treni hiyo pia imezinduliwa pamoja na treni ya TAZARA ambayo itafanya kazi kama ya Ubungo, lakini yenyewe ikianzia eneo la TAZARA kuelekea Mwakanga.​


  Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Waziri Mwakyembe alisema atahakikisha treni hiyo inaendelea kufanya kazi ili kuwasaidia kiusafiri wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kero ya usafiri hasa kwa foleni, ambapo utumia muda mrefu njiani kuingia na kutoka jijini.​


  Alisema jumla ya mabehewa ya treni 14 pamoja na injini mbili zimekarabatiwa na mafundi wazalendo nchini, ambayo ndiyo yatakayokuwa yakifanya kazi ya kusafirisha abiria kuingia na kutoka jijini kila asubuhi na jioni. Alisema kwa sasa inafanya treni moja kwa majaribio lakini baada ya uzinduzi mkubwa zitafanya kazi treni mbili, na zitakuwa zikipishana njiani moja ikirudi na nyingine ikienda.​


  Akifafanua zaidi alisema kitendo cha mafundi wazalendo kufanya ukarabati kwa mabehewa na injini kimeokoa kiasi kikubwa cha fedha za umma kwani ukarabati wote umetumia sh. bilioni 2.1 tu, ilhali kama Serikali ingelazimika kukodi injini gharama ingekuwa kubwa zaidi kwani bei ya kukodi injini moja ya treni ni sh. milioni moja kwa siku.​


  Hata hivyoDk. Mwakyembe amewataka Watanzania hasa abiria kuwa wavumilivu kwa upungufu utakaojitokeza kwa safari za mwanzo kwani bado wanaendelea kufanya marekebisho kadhaa, lakini baada ya muda mambo yatakaa sawa. Mwandishi wa habari hizi alikuwa ni mmoja wa wasafiri walioizindua treni hiyo leo.​


  Awali akizungumza mmoja wa viongozi waandamizi wa TRC, alisema treni hiyo itafanya kazi kila siku isipokuwa kwa siku za jumapili na siku kuu na itaanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa sita mchana na kupumzika hadi saa 9:00 za jioni, itakapoendelea tena na safari zake hadi majira ya saa nne usiku.​


  Uchunguzi uliofanywa na muandishi wa habari hizi umebaini kuwa behewa moja la treni linauwezo wa kuchukua abiria 66 wakiwa wamekaa, lina milango minne, feni, taa, muziki/redio, pamoja na mikanda maalumu ya kujishikia kwa abiria ambao watakuwa wamesimama. ​


  Aidha mabehewa yote yana madirisha ya kutosha kuingiza na kutoa hewa ya kutosha. Treni ilioanza kazi leo, ikitokea Ubungo ilikuwa ikisimama vituo vya eneo la Mwananchi (relini), Tabata Relini, Buguruni Miamani, Tazara, Kariakoo Gerezani (Kamata), na mwisho Kituo Kikuu cha Treni kilichopo jirani na Kituo cha Polisi Kati (Katikati ya Jiji).​
  *Imeandaliwa na mtandao wa Thehabari.com

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tusibebe Nyembe na Screw Drivers - kukatakata VITI na kubeba hizo FENI
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nilichopenda kwenye hii habari ni kua wametumia engineers wazalendo..big up mwakyembe...ingekua wengine hapo ka akina ngeleja na maige wangeagiza engineers kutoka south africa wangelipwa dollars nyingi tu za bure bora hiyo hela wamepewa locals...inaonyesha vitu vingi tunaweza fanya wenyewe sio lazima kuleta watu weupe kutusaidia
   
 4. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Hongera sana Dr. Mwakyembe, wenzako wameshindwa kwa miaka 50 lakini wewe umeweza kwa miezi 4 tu!! Kweli tukiamua tunaweza.
   
 5. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona watu walikuwa wachache sana, au ndo wanaogopa kupitilizwa na tren? Isije ikaanza kugonga watu tena ikiwa balaa
   
 6. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ila hapo kwenye bilioni mbili tu za ukarabati kidogo pangehitaji maelezo ya kutosha.
   
 7. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwakweli nimefurahishwa sana na hii habari,kumbe tukipata mtu alie tajiri wa kufikiri matatizo yale sugu yatapungua kwa kiwango kikubwa sana.Ila ningewaomba abiria wajitahidi kutunza mazingira waliyotengenezewa ili na sisi tuonyeshe kama tunaweza kuenzi mazingira kwa serikali ili wapate moyo wa kuboresha na mengineyo tunayohitajia.
   
 8. StayReal

  StayReal JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 519
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  One thing to be proud about!
   
 9. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  KWA UZEMBE UZEMBE LAZIMA WAHUJUMU UCHUMI WATAIUA Treni YETU.BIG UP MWAKYEMBE
   
 10. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 714
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Big up Mwakyembe..lakini c vibaya tungempa Mulugo hii Wizara ili aweke mambo vizuri..!!:mwaaah:
   
Loading...