Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,882
- 828,453
Achana na huo mpangilio wa ukaaji.. Achana na makochi mazuri na zulia jekundu.. Itazame kiroho zaidi hata kama nyuso zao hazionekani ama hazionekani vema
Ni picha iliyobeba hisia za majuto.. Wote walioko hapo walitokea majumbani kwao kwenye vitanda vyao, wakapata nafasi ya kujiandaa na kuvaa nguo nzuri na safi na kuendeshwa hadi kazini
Kisha wote wakakusanyika kushuhudia kesi ya mahabusu wa kisiasa mwenye tuhuma za uhaini akiwa katokea mahabusu bila familia yake ndugu jamaa marafiki
Akiwa na ulinzi mkali wa magereza polisi na usalama.. Cha ajabu ana tabasamu pana ana furaha ana nuru. . korti iko kimya ikimsikiliza kwa hamasa na tafakuri kuu
Linganisha maudhui ya kortini na ya hapa kwenye hii picha... Kuna ujumbe mbingu zinajaribu kutuambia.. Tuihifadhi vema hii
Baada ya court session.. Wao wamerudi majumbano kwao lakini wakiwa wamejawa fadhaa.. Huku mtuhumiwa akirudishwa rumande akiwa na tabasamu kuu
By the way! Ni nani aliamua kuvujisha hii picha? Jibu ni moja tuu... Nguvu ya asili...Ila sidhani kama kibarua chake kitasalimika!
Nature is taking its course!
Good morning TanganyikaView attachment 3390796
===============
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search ulibaini kuwa picha hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika ukurasa wa Ikulu kwenye mtandao wa X tarehe 13, Juni 2024.
Rais Samia alikuwa akifuatilia Bunge la Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2024/25 kwa njia ya runinga akiwa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma. Hotuba hiyo ilikuwa ikisomwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Picha hiyo imepotoshwa kwa kubadilishiwa picha ya Televisheni, ambapo imeondolewa iliyokuwa ikonesha Televisheni ya Taifa iliyokuwa ikirusha matangaza ya bajeti kuu ya serikali 2024/25 na kuweka picha ya matangazo ya ITV inayohusu matangazo mbashara ya Kesi inayomkabili Tundu Lissu.
Pia soma, Pre GE2025 POTOSHI Picha ya Rais Samia akifuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu