Picha: Yaliyotokea Dumila, Morogoro

Picha: Yaliyotokea Dumila, Morogoro

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,357
8296308_orig.jpg


Wananchi wakiwa wamefunga barabara.

712946_orig.jpg


Walichoma mataili barabara kuu ya Dodoma Morogoro kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa serikali ya mkoa wa Morogoro kuzungumza nao, jambo ambalo walifanikiwa.

9119568_orig.jpg


4876978_orig.jpg


3475869_orig.jpg


3540168_orig.jpg


attachment.php



attachment.php


Msururu wa magari

attachment.php


Kupita kwa shida.

attachment.php


attachment.php


3902729_orig.jpg


Afisa Tabibu wa Zahati ya Dumila Dkt. Mathew Kayunga. Uliofunikwa kwa shuka jeupe, kushoto kwa daktari ni mwili wa marehemu.

Hafisa Tabibu wa Zahati ya Dumila Dr Mathew Kayunga ambaye alithibitisha kupokea majeruhi saba waliojeruhiwa kwenye vulugu hizo,pia alithibitihsa kupokea mwili wa marehemu mohamed Msigala majira ya saa 6 mchana wakati vulugu hizo zikiendele kupamba moto eneo hilo la Dumila Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.

Alipoulizwa kama kifo cha mzee huyo kimetokana na vulugu hizo Daktari huyo alidai kwamba hawezi kuthibitisha jambo hilo kwa kuwa marehemu alifikishwa kwenye Zahanati hiyo kwa usafiri wa boda boda akiwa tayari amekufa.

" Huyu marehemu kaletwa hapa tayari amekufa hivyo hatujamfanyia uchunguzi na kubaini ni kitu gani kimesabisha kifo chake ingawa anajeraha mdomoni na anavuja damu sikio la kushoto'alisema Daktari huyo

Akizungumza na Mtandao huu nje ya Zahanati hiyo Baba mdogo wa marehemu huyo Bw Salum Hussein Mnyika[69] alidai kwamba kwa kipindi kirefu mwanaye huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo mkubwa.

"Mwanangu ni mkazi wa kijiji hicho cha Mwabwegele kinachogombaniwa hivyo leo asubuhi alijumuika na wenzake kwenye maandamo hayo ya kufunga barabara na kwamba alitoka kwenye kijiji hicho kwa kutumia usafiri wake wa baiskeli mpaka nyumbani kwangu ambapo aliichacha baiskeli na kwenda kujumuika nawakulima wenzake, majira ya saa sita nilijulishwa kwamba mwanangu huyo amefariki,tunahisi huenda mstuko ule wa mabomu umestua moyo wake na kusababisha kifo hicho"alisema Bw Mnyika.

6293212_orig.jpg


Wananchi wakiwa nje ya Zahanati ya Dumila kwa lengo la kuwapa pole wenzao waliojeruhiwa kwenye vurugu hizo.

40873_orig.jpg


938826_orig.jpg


Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kilosa eneo la Dumila.

7688208_orig.jpg


Wananchi wa wilaya ya Kilosa ambao wengi wao walikuwa ni wakulima wakimsikiliza Mkuu huyo wa Mkoa.

3993205_orig.jpg


Mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akizungumza na kamti hiyo nje ya kituo cha polisi Dumila kabla ya kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Kilosa leo mchana

Chanzo: http://dustanshekidele.blogspot.co.uk/2013/01/mapigano-ya-wakulima-na-wafugaji-kilosa.html
 
Huu ni mwanzo tu,mengi yatafuatia tena makubwa zaidi ya haya.Mapinduzi ya viongozi wenye uchu wa kinyonyaji,haya ndiyo matokeo yake.Tujifunze zaidi.
 
Sasa hiyo barabara ndo shamba wanalogombania?
Na abiria na jamaa wa magari wangeamua nao kuwatandika hawa wanajamii wa hapo ingekuwaje?
 
Picha hizo zina mambo mengi ya kujadili aaaangalieni bara bara za kichina picha ya kwanza toka juu hio bara bara haina kingo muda sio mrefu haitakuwepo na ni tz kote walipojenga wachina
 
Watanzania Bado Uoga ni wa Kiwango cha Juu kabisa, Hatuna Tofauti na wahindi, Cheki kule Mtwara hulianzisha and then baadae ukipita huwezi jua kama kulikuwa na vurugu, haya mambo inatakiwa yawe non stop, ni vurugu usiku na Mchana kama Mkuru hajakimbia kule magogoni

Hao wakulima kwa sasa kimya utazai ndo wamerudishiwa mashamba yao,
 
Amani yetu inatakiwa ipelekwe india kwani iko mahututi!
 
haya mavi-ongozi ya ccm bana, mpaka watu wafe ndo yashituke. hivi yangeenda tangu awali haya yangetokea? kwakeli haya majamaa yamelewa madaraka. come 2015 mkapumzike kwa tabu.
 
Watanzania Bado Uoga ni wa Kiwango cha Juu kabisa, Hatuna Tofauti na wahindi, Cheki kule Mtwara hulianzisha and then baadae ukipita huwezi jua kama kulikuwa na vurugu, haya mambo inatakiwa yawe non stop, ni vurugu usiku na Mchana kama Mkuru hajakimbia kule magogoni

Hao wakulima kwa sasa kimya utazai ndo wamerudishiwa mashamba yao,
looks like toilet thought
 
serikali ya ccm/kikwete lazima iwajibike kwa wananchi kwa kufanyia kazi yale wayatakao. sio mpaka watu wafe. hivi nyinti ccm mmelaaniwa na nani? kwanini watu wanakufa kwa sababu zinazoepukika? mmeniudhi sana nyie wapumbavu. oneni mnavyobabinkia watu vyesi mfano kule kibiti. kamanda simoni siro ansema wananchi waliwapongeza kwa kuua watumia madawa ya kulevya dakika chache baadaye anatuambia wananchi hao hao waliopongeza zaidi ya 120 waliandamana kwenda kuvamia polisi. this is stupidy.
 
kwa ujinga wa viongozi wetu hapo utawasikia muda si mrefu hao ni Chadema ndo wanaosababisha hii vurugu, lakini chadema hawana mamlaka ya kugawa ardhi kwamba hapa ni kwa sababu ya wafugaji tu na hapa ni kwa sababu ya wakulima wenye mamlaka hayo ni ccm! lakini subiri utasikia tu, kwani hawa jamaa wameishiwa kabisa uwezo wa kufikiri. Wanafanya mambo kijinga halafu baadaye wanamtafuta aliyesababisha huo ni ujinga wa hali ya juu kabisa.
 
Angalizo: Pimeni sana maneno yenu mnayotoa wakati wa KAMPENI kwani huwa mnaahidi kila mnaloletewa. Mmekuwa ndumilakuwili: Huku Mwataka na Kule Mwataka, matokeo yake NDIYO HAYO.
 
Picha hizo zina mambo mengi ya kujadili aaaangalieni bara bara za kichina picha ya kwanza toka juu hio bara bara haina kingo muda sio mrefu haitakuwepo na ni tz kote walipojenga wachina
Mchina anajenga barabara au kuuza bidhaa kulingana na pesa yako; so kama wanasiasa wanatuaminisha kuwa wametoa mabilioni kuzijenga wakati ni tofauti matokeo yake ndio hayo. mchina amefanya kazi nzuri sana za barabara na kuuza bidhaa za viwango vya hali ya juu katika nchi nyingi za Africa, na pia nchi za ulaya na marekani. nadhani ishu hapa mfuko tu.
 
Huu ni mwanzo tu,mengi yatafuatia tena makubwa zaidi ya haya.Mapinduzi ya viongozi wenye uchu wa kinyonyaji,haya ndiyo matokeo yake.Tujifunze zaidi.

KIKWETE's POLICE STATE. Yeye yuko USWIZI na Leodgar Tenga anakula KUKU. Akitoka huko atapitia ETHIOPIA, Baadae labda Honolulu
 
Back
Top Bottom