PICHA YA WIKI

PICHA YA WIKI

Alienda kupiga picha tu, Hakwenda kusaidia kuokoa. Kwa maana na yeye pia anasaidiwa asidondoke. Hao wanaomsaidia pekee wangetosha kubeba watu wawili.
Kipindi cha uchaguzi usishangae akatumia hizo picha kwenye kampeni. Kwanza kwa kiasi flani ni dharau kubwa kwa anaotaka kuwaaminisha alikua anaokoa watu. Anawaona ni wajinga.

Labda kama alipigwa bila dhamira yake, na watu wakaitumia isivyo.
Alikisudia mwananchi gani apige picha wakati wa mvua na kitecno chake
 
Hii sio Politics,, anakiuka principles za siasa zinazofanywa kote duniani.,, Uongo, Wizi, Ulafi, Tamaa ya madaraka, ukandamizaji, unyonyaji wa wanyonge, n.k

Unless atuambie nini anafanya lakini asituambie yupo hapo kama kiongozi wa kisiasa..!!

Khaaa!!! wanadamu hatuna shukran,, Ila wenyewe ndo wameyataka
 
Amejitahidi Kwa kumuandaa mpiga picha vizuri....
 
Atakayempa kura mbunge kisa alikubeba wakati mvua inanyesha atakua ana matatizo, kwasababu kilichosababisha maji kutuama ni kukosa miundombinu ya maji taka, mitaro na mifereji ya kuyaelekeza hayo maji sehemu stahiki.

Huyo mbunge ameshindwa kusimamia hayo yote badala yake kaja na fulana nyeupe kuja kukubeba.
Hiyo miundombinu ya kuweza kuzuia maji ya mafuriko ingekuwepo nchi za dunia ya kwanza usingekaa usikie kitu kinachoitwa mafuriko huko kwao
 
Hiyo miundombinu ya kuweza kuzuia maji ya mafuriko ingekuwepo nchi za dunia ya kwanza usingekaa usikie kitu kinachoitwa mafuriko huko kwao
Mara ya mwisho Tanzania kunyesha mvua ambayo iliitwa ya mawe ni mwaka 1999, tulipata after effects za Tsunami kidogo mnoo nadhani 2006 au 2007.
Hatujawahi kukumbwa na vimbunga. Tetemeko liliwahi kutokea mikoa ya kusini kipindi hicho tunatawaliwa na wakoloni.

Tumekuja kupatwa na tetemeko la kuweza kuharibu miundombinu mwaka jana.

Piga hesabu wenzetu wameshakumbwa na vitu vingapi kipindi sisi tupo shwari, na ili kwao yatokee mafuriko hua ni kama mvua iliyonyesha hapa kwetu au kwao huambatana na upepo mkali na vimbunga pia?

Kama haya yote unayajua, basi umejitoa akili. Kama huyajui pole mkuu inabidi usome sana.
 
Kama mtu anakaa bondeni hata utengeneze mifereji gani mafuriko yatatokea tu
Kwa njia pekee ni kusubiri maji yamfike ukambebe aliko......Au kumshauri mapema eneo analokaa ni hatari aondokeee mwenyewe mapema na vitu vyake
 
Mara ya mwisho Tanzania kunyesha mvua ambayo iliitwa ya mawe ni mwaka 1999, tulipata after effects za Tsunami kidogo mnoo nadhani 2006 au 2007.
Hatujawahi kukumbwa na vimbunga. Tetemeko liliwahi kutokea mikoa ya kusini kipindi hicho tunatawaliwa na wakoloni.

Tumekuja kupatwa na tetemeko la kuweza kuharibu miundombinu mwaka jana.

Piga hesabu wenzetu wameshakumbwa na vitu vingapi kipindi sisi tupo shwari, na ili kwao yatokee mafuriko hua ni kama mvua iliyonyesha hapa kwetu au kwao huambatana na upepo mkali na vimbunga pia?

Kama haya yote unayajua, basi umejitoa akili. Kama huyajui pole mkuu inabidi usome sana.
Unaamua kuruka ruka sasa... Hakuna sehem yeyote dunian wanakoweza zuia lililotokea Tanga... Unless mtu aamue tu kupiga kelele kama ilivyo desturi ya mtanzania.... Uwe umepumzika hata kwa miaka 100000 bila kash kash yeyote, siku likifika limefika halizuilik
 
Narudia tena 'SOMA'

Tafuta articles mbalimbali zikuoneshe mafuriko ya wenzetu yanatokana na nini, mvua yetu ya Tanga siyo ya kusababisha mafuriko kama tungekua na utamaduni wa kujiandaa.

Hivi kweli kwenye mafuriko, unaenda kumuokoa mtu huku umesimama na maji yanafika kwenye ugoko? Kama unaishi Dar kipindi cha mvua za masika nenda sehemu inaitwa Kawe halafu fananisha.
 
Hapo nadhani maeneo ya Mombo.
Huyo Mbunge wa Korogwe Vijijini kwa kweli anajitahidi sana kupigania wananchi wake japo serikali inaweka pamba masikioni. Nadhani wanampuuza tu mana hata suala la maji safi kwenye jimbo lake analisemea sana sijui wanamsikiliza au vipi!!

Eneo kubwa au karibu lote la Wilaya ya Korogwe lenye ardhi nzuri ni mashamba ya mikonge. Wajerumani walimiliki eneo lote lenye Rutuba na kuwafanya wananchi wa maeneo hayo kuwa manamba kwenye mashamba ya mikonge.
Wananchi wa eneo hilo hawana ardhi nzuri ya kuishi. Pamoja na Mwalimu kutaifisha eneo hilo na kumilikiwa na serikali Cha ajabu serikali ya awamu ya pili iliuza eneo hilo kwa wawekezaji bila kupunguza maeneo ya mashamba na kuwapimia wananchi wananchi viwanja kama sehemu za kujenga miji yao kama Mombo ,Mazinde,Mkumbara ,Makuyuni n.k. kwa kuwa Miji hii inakua kwa kasi.
Matokeo yake watu wamejenga kiholela mabondeni na chini ya milima yenye maporomoko makubwa ya maji wakati wa mvua bila kuwa na mipango miji.

Serikali zetu zinakosa mipango ya muda mrefu ndio maana maeneo hayo waliyagawa kwa bei chee kwa mwekezaji uchwara enzi hizo jambo ambalo inakua shida kwa Serikali ya awamu hii kuchukua eneo hilo kwani wamiliki watadai fidia kubwa sana.

Hata hivyo ni vyema serikali ikapunguza eneo la mashamba ya mikonge na kuwagawia wananchia maeneo ya kuishi yenye miundo mbinu bora. Hata kwa kushirikiana na wananchi wenyewe namna ya kulipa fidia.
Serikali inaweza ikalipa fidia nusu na wananchi nusu.
Pia serikali inaweza ikawapa wawekezaji wa eneo hilo eneo lingine na yaliyopo kwenye miji yakapunguzwa ili wananchi wanyonge wapate maeneo bora ya kuishi iwe rahisi hata kuokolewa wakatibwa mvua kubwa.
Kwa sasa maeneo ya Miji midogo yote ya Korogwe hayana Miundo mbinu bora ya mifereji ya maji wakati wa mvua. Ikichangiwa zaidi na barabara iliyojengwa kwa kiwango cha chini bila mitaro na makalavati makubwa wakati makandarasi wetu wakiwa wanajua fika kuwa wakati wa mvua kuna maji mengi yanayotokea kwenye milima na kusomba udogo toka mashambani.
 
cheap politics
ila bora uyu aliyeenda kupiga picha kwenye matope kuliko makamba ambaye utadhani anaishi uamishoni
 
Back
Top Bottom