Picha ya Leo

Picha ya Leo

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
pastor.jpg
Hii ndiyo hali halisi ya makanisa haya mapya!
 
Na ndio kisa na maana hawafundishi neno la mungu zaidi ya kupigana vijembe kuwa nani ni zaidi katika kuwakamua waumini.
 
Mkuu,

Neno la Mungu sasa ni biashara. Nimejiuliza sana kwa nini hawa viongozi wa 'Makanisa Mapya' yenye majina ya ajabu yanayoibuka kila kukicha hayaendi sehemu zenye watu huko vijijini, bali yamejikita mijini? Utasikia wanafanya 'lunch hour fellowship' Serena Hotel, kweli hapo kuna ukweli wowote wa huduma ya kiroho zaidi ya kusafisha pesa yao chafu?

Wamisionari waliokuja kueneza dini ya Kikristo enzi zile walikwenda mikoani na mpaka kwenye vijiji. Misheni za kwanza za makanisa ya Anglikana, Katoliki, Kilutheri na hata ya wasabato zilianzishwa Ndanda, Peramiho, Ifakara, Pugu, Minaki, Maneromango, Bagamoyo, Magila n.k. Na si hizo tu miisheni kubwa, bali wale wamisionari waliingia mpaka vijijini, kuna sehemu walitafsiri Biblia na vitabu vya nyimbo, na hata kujifunza lugha za kiasili ili waweze kuwapa mafundisho ya kiroho na kuwapatia waumini huduma mbalimbali za kiroho na kimwili pia (kama hospitali, shule n.k)

Hawa wamisionari wa siku hizi na vyeo vikubwa wanavyojipachika, wengine Manabii, maaskofu ambao hawakusomea hata Theologia yoyote na wachungaji wao ni matajiri wa kutupwa kama picha inavyoonyesha, wanaishi kwenye mahekalu, wanaendesha magari ya thamani, ambavyo vinatokana na kuwanyonya waumini wao wanaoendelea kutumbukia kwenye dimbwi la ufukara. Wote tunaujua utajiri wa kina Gertrude Lwakatare, Mwingira, Kakobe, Lutumba na wengineo wengi. Hizo pesa kwanza wanazipata wapi kama sio kuwanyonya waumini na pengine hata kusafisha pesa chafu zinazopatikana kwa njia mbalimbali zisizo halali...
 
Hivi haya mambo, ni tunafanywa wajinga Waafrika tu au hata kwa wenzetu wanaojiita dunia ya kwanza yapo??
 
Huko Marekani ambapo ndio chimbuko la haya makanisa wana makanisa yao makubwa wanayaita Mega Churches, yaani ni zaidi ya kumbi za matamasha ya BET au au KORA.....

Kuna jamaa mmoja mwanamuziki aliingia hayo makanisa kwa mara ya kwanza walipomuhoji akasema 'Nimeingia Kanisani kwasababu najisikia kama niko Club niliyoizoea tofauti ni kunawakati jina la Yesu linatajwa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom