Picha: Wolper anaswa LIVE kwenye jengo la Freemasons

Picha: Wolper anaswa LIVE kwenye jengo la Freemasons

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,213
Reaction score
18,455
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameibua maswali kwa mashuhuda walimuona ‘ live ’ akiingia kwenye hekalu la watu wa Jamii ya Siri (Secret Society ) ya Freemasons yenye nguvu duniani inayohusishwa na imani za kishetani .

TUJIUNGE MTAA WA SOKOINE

Tukio hilo lililoibua kizaazaa kwa mashuhuda waliomuona Wolper , lilijiri juzikati, mishale ya jioni kwenye hekalu hilo lililopo Mtaa wa Sokoine mkabala na Hoteli ya Hyatt Regency , The Kilimanjaro jijini Dar jirani na Benki Kuu ya Tanzania ( BoT).

SIMU ZAMIMINIKA

Likiwa kwenye majukumu ya kusaka habari kama kawaida yake , gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa mashuhuda hao wakiwataka wanahabari wetu kuwahi eneo la tukio .
Kufuatia umbali waliokuwa mapaparazi wetu , ilibidi kuwaomba mashuhuda hao ‘ kumfotoa’ picha ambapo mmoja wao alifanya hivyo na kuziwasilisha kwenye meza ya gazeti hili.
. ..akitoka .

ALINASWAJE?

Akidadavua mazingira aliyonaswa Wolper , shuhuda huyo alikuwa na haya ya kusema :
“Kwanza mwanzoni hatukumjua kama ni Wolper lakini kuna dada ambaye anamjua vizuri na ni shabiki wake mkubwa ndiye aliyetuhakikishia kuwa ni Jacqueline (Wolper ).
“Kuna waliomuona akiingia . Nilipofika mimi nilimkuta getini anatoka . Walisema hakukaa muda mrefu kwani alitumia dakika kadhaa kisha akatoka na kwenda kwenye gari lake aina ya Prado (Toyota ) alilopaki mbali kidogo na lango hilo , ” alisema shuhuda huyo kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza :
“Baada ya hapo alitoka nduki maana nzi ( watu) walikuwa wameanza kumjalia na kulizingira gari lake. ”

WOLPER AJITETEA

Baada ya kuzikagua picha za Wolper akiwa katika mazingira hayo na kujiridhisha kuwa ni yeye, gazeti hili lilimbana mwigizaji huyo ambapo alijitetea :
... a kiwa getini .
“Jamani nilikuwa sina hili wala lile . Kuna jengo nilikuwa nalitafuta ndiyo nikajikuta nimetokea maeneo hayo .
“Mimi mwenyewe nilishtuka kuona watu wananiangalia sana kumbe ndiyo nikagundua nipo kwenye lango la Freemasons.”
Risasi Jumamosi : Mbona kuna mashuhuda walikuona wakati unaingia na wakati unatoka ?
Wolper : Unajua mimi sikuona kibao chao lakini sikuingia kabisa hadi kule ndani .
Risasi Jumamosi : Lakini kuna madai kwamba wewe ni mwanachama . Unasemaje?
Wolper : Mimi siyo Freemasons, nakumbuka kuna siku watu walinifuata wakaniambia nijiunge Freemasons nitakuwa na mafanikio lakini sijakubaliana nao .
 
Attachments

  • 1431799263526.jpg
    1431799263526.jpg
    25.9 KB · Views: 8,690
Hakika Neno Freemason linatumika vibaya

attachment.php
 
Ndoto za mchana huwa hawakutani mchana, labda alienda kupiga picha😀😀😀
 
Hapo ni nje
Kuna uhakika gani kama aliingia ndani

Hawa bongo ma.vi hawachelewi kumuita imelda wakapiga picha ili kuwa front pages

Kwanza freemanson watakuwa wameishiwa kweli kweli mpaka kuwa na mwanachama bongo mavi
 
Huyu anatafuta kiki ya movie yake mpya hana lolote
Na hawa waandishi wa udaku ni mafala sana wakipewa visenti wanatengeneza story kama movie za hollyhood!
 
Vi habari vya kutengeneza kama hivi ndio vinawashusha thamani hawa watu..yaani unaona kabisa kwamba kuna kiki inatengenezwa...tokea lini jumuia ile ikafuata watu ili wajiunge ?atadanganya hao beki 3 tu
 
Mbona yupo nje ya jengo, hapo kila mtu anaweza kupiga picha. Hyatt kwa geti la nyuma ni opposite na freemanson temple. Wameuza gazeti tu, pesa ngumu inahitaji akili ya ziada kuizalisha.
 
Hicho kizazi cha udaku kinavyojengwa khatari sanaaa.
 
Hahahahaa Hyatt ikawaje akaingia kwenye jengo la Freemason? Maana hata hapafanani useme alijichanganya.

We nawe kwan hupajui kilimanjaro? Hayo si ni mazingira tu kwa kule nyuma ,labda alikuwa kwenye windo anavizia
 
Hapo ni nje
Kuna uhakika gani kama aliingia ndani

Hawa bongo ma.vi hawachelewi kumuita imelda wakapiga picha ili kuwa front pages

Kwanza freemanson watakuwa wameishiwa kweli kweli mpaka kuwa na mwanachama bongo mavi

Ebu nisaidie kushangaa mxiuu freemason my foot
 
Huyu anatafuta kiki ya movie yake mpya hana lolote
Na hawa waandishi wa udaku ni mafala sana wakipewa visenti wanatengeneza story kama movie za hollyhood!

Movie kutoka wapi? Basi atakuwa hana akili, maana yeye hana kampuni ya film kusema anaipigia debe filamu yake, na haruhusiwi ata kugusa kazi za watu ambazo nying ndo ucheza
 
Mbona yupo nje ya jengo, hapo kila mtu anaweza kupiga picha. Hyatt kwa geti la nyuma ni opposite na freemanson temple. Wameuza gazeti tu, pesa ngumu inahitaji akili ya ziada kuizalisha.

Mbwa kabisa hawa mxiuu
 
We nawe kwan hupajui kilimanjaro? Hayo si ni mazingira tu kwa kule nyuma ,labda alikuwa kwenye windo anavizia

Napajua vizuri tu binamu.Hapa nahoji alivyosema kua alijisahau...
Hata hivyo haya mambo ya Shigongo ni too much aisee.
 
Napajua vizuri tu binamu.Hapa nahoji alivyosema kua alijisahau...
Hata hivyo haya mambo ya Shigongo ni too much aisee.

Walijipiga picha babu wee, we unadhan posta wana mda mmchafu wa kufuatilia mastaa ushuzi mxiuuu
 
Back
Top Bottom