Picha: Timu ya wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa CCM, NEC - 2007-2012

Picha: Timu ya wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa CCM, NEC - 2007-2012

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM NEC>>>2007-2012 WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

256025_412807155449939_329937755_o.jpg






579729_368940586514987_1671510653_n.jpg



Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kabla ya kikao cha NEC, leo mjini Dodoma. Wengine, waliokaa. Kutoka kushoto ni Mawaziri Wakuu wa zamani, John Malecela na Cleopa Msuya, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Kulia ni Mawaziri wakuu wa zamani Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wana-CCM, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama




Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishiriki kucheza wimbo wa hamasa ya Chama, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, WisoMakamu (kushoto) baada ya kupiga picha ya pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, leo, kwenye viwanja vya Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma leo.



Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Samwel Sitta akimsalimia kwa unyenyekevu Mjumbe mwenzake, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, nje ya ukumbi, kabla ya kikao cha NEC mjini Dodoma leo.

Mjumbe wa NEC, Frederick Sumaye akimweleza jambo Mjumbe wa NEC mwenzake Kingune Ngombale-Mwilu, baada ya kukutana nje ya ukumbi, kabla ya kikao cha NEC mjini Dodoma leo.

Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa ukumbini kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma leo

Ahhh! kweli? hapa ni Mjumbe wa NEC, Shamsi Vuai Nahodha alizungumza jambo na Mjumbe mwenzake Cleopa Msuya ukumbini.





Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa ukumbini kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma leo (picha zote na Bashir Nkoromo)​



338367_149110025231995_251624945_o.jpg



414140_445719442138480_1523532558_o.jpg





404593_419543078104942_1935484941_n.jpg
 
Wangapi Wapenda UJAMAA na KUJITEGEMEA ?

Na Wangapi Wanatukuza JEMBE na NYUNDO ? na Kina nani Waupenda MUUNGANO ?
 
Tija kwa taifa?
Alaf walipewa posho!
 
Hao wemye kaki ni CHADEMA walikaribishwa nini
 
Ivi kuna cha kujivunia kwenye iyo team kwenye ie i mean mwananchi wa kawaida kule Dumira,kibaigwa,tunduru,Kyaka.Namanyere etc ?
Nazani wao kama wao watajivunia ulaji walioupata na si kwa kuwatumikia wananchimkwa Dhati kabisa
 
Kumbe by then Baba January alikuwa na kwashakoo
Hapo ni baada ya kutemwa ukatibu Mkuu. Huoni jinsi alivyo nuna na kumwangalia Mukama jicho pembe? zamani angekuwa amepewa kiti. Cheo bwana! ndio maana wanatoleana bastola hawa CCM
 
Dah,yani sioni hata mwenye uchungu na nchi hii,sura ni zilezile za miaka nenda rudi bado wanafikiria tanzania ni ileile kila siku,wanafiliria namna ya kugawa ubwabwa 2015
 
ndiyo maana chadema wanauchukia sana mwenge kumbe upo kwenye kadi ya hawa vijana
 
Ivi kuna cha kujivunia kwenye iyo team kwenye ie i mean mwananchi wa kawaida kule Dumira,kibaigwa,tunduru,Kyaka.Namanyere etc ?
Nazani wao kama wao watajivunia ulaji walioupata na si kwa kuwatumikia wananchimkwa Dhati kabisa

wakumtumikia mwananchi upinzani hakuna hamja pata sehem ya kula nyinyi mkiipata wananchi watakoma kwani mapema kabisa mnaonekana nyinyi njaa kali
 
Back
Top Bottom