Picha: Timu ya taifa ya netiboli yarejea kwa kishindo baada ya kutwaa ubingwa wa kimataifa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

TIMU YA TAIFA YA NETIBOLI YAREJEA KWA KISHINDO BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA MICHUANO YA KIMATAIFA





IMG_2805.JPG



Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi akiwa Mwenyekiti wa wake za viongozi, Germina Lukuvi mara baada ya timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens) iliporejea nchini na Kombe la Michiuano ya Kimataifa iliyofanyika nchini Singapore.
IMG_2872.JPG

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens' wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo wakitokea Singapore walikokuwa wakishiriki michuano ya Kimataifa na kutwaa Kombe la michuano hiyo.
IMG_2925.JPG

Mlezi wa Chaneta kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Ain Sharif akikabidhi kitita cha sh. 500,000 ikiwa ni kama zawadi kwa timu hiyo baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa yaliyofanyika Singapore na Taifa Queens kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
IMG_2945.JPG

Wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Quees) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili leo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Singapore.





Na Mwandishi Wetu


TIMU ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens' imerejea kwa kishindo leo baada ya kushiriki na kutwaa Kombe la michuano ya Kimataifa iliyokuwa ikifanyikia Singapore barani Asia.


Taifa Queens ilitwaaa ubingwa huo baada ya kuingia fainali ikiwa na pointi 10 ikicheza na timu ya Malasia iliyokuwa na pointi 4 ambapo ilifanikiwa kuifunga magoli 45-38.


Akizungumza baada ya kurejea, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi alisema maandalizi ni kitu kizuri sana, anaamini kocha aliwapa wachezaji mbinu za kutosha hadi kupelekea ubingwa huo.


"Hii imetusaidia sana maana kocha mwenyewe ni kijana hivyo anambinu za kisasa kitu kilichotusaidia wakati tukiwa ugenini, hakuna kitu kizuri kama kupigiwa wimbo wa taifa lako ukiwa ugenini huku wazungu ambao ni wenyeji wa mashindano hayo wakiwa penbeni," alisema Bayi.


Kwa upande wake Kocha wa Taifa Queens, Mary Waya alisema mashindano yalikuwa ni magumu anawapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo ambao umemuweka pazuri yeye pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.


"Kila kitu unatakiwa umtangulize mungu, akili, na nguvu ndio zinafuata naimani wachezaji wangu walikuwa makini na kujua nini wamekifuata huko, akili ni kitu cha muhimu ukiwa mchezoni hivyo mimi sina la kusema zaidi ni kumshukuru mungu kwa ushindi tulioupata," alisema Kocha huyo ambaye ni Mmalawi.


Kocha huyo alisema amefurahishwa na ushindi huo na kwamba kwasasa anajipanga kuifua timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia.
Naye Nahodha wa timu hiyo, Lilian Sadolin alisema anamshukuru mungu kwa ubingwa huo pia Watanzania wanatakiwa kuendelea kuwapa sapoti katika mashindano mbalimbali.


"Wakati tunaondoka niliwaahidi Watanzania lazima turudi na ushindi, sisi ubingwa tushaapata kabla hatujaenda kule tulienda kutimiza wajibu, naimani tuliwazidi mbinu unapokuwa uwanjani unatakiwa kuwa na mbinu za ziada hivyo tunamshukuru mungu kwa ushindi tulioupata," alisema Lilian.

KWA HISANI YA HABARI NA MATUKIO BLOG
960924483110490008-2893072135355139372







 
Hongereni WanaNETIBOLI wa Tanzania... Wanaume Wametokwa JASHO huko KAMPALA

HONGEREKI kwa MLICHOKIFANYA SINGAPORE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom