PICHA; Shamrashamra baada ya hukumu ya JJ Mnyika!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765







Kwa mbali watu wakiserebuka baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali mashtaka matano yaliyokuwa yana mkabili Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika hivyo wana CHADEMA walikuwa wengi Mahakamani hapo kulipuka kwa furaha na kuingia Barabarani kushangilia ushindi wa kesi hiyo.



Shamrashamra zikiendelea hapo..



Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiteta na waandishi wa habari nje ya Mahakama kwa kuwashukuru wananchi wote waliokuwa bega kwa bega na Mh.Mnyika katika kipindi chote cha kesi hiyo.



Madai hayo yalikuwa kama ifuatavyo:
-Kuwepo tuhuma za kashfa kuwa mlalamikaji aliuza jengo la Umoja wa Wanawake, UWT.
-KUbadilishwa kimakosa kwa kura katika formu za matokeo ya Ubunge
-Kuwepo kwa watu katika chumba cha majumuisho ya kura
-Matumizi ya tarakilishi(Laptop) ya mlalamikiwa wakati wa kujumlisha kura
-Ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika uchaguzi ambazo zilisababisha kuwepo kura hewa 14,854


Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. John Mnyika (wa pili kushoto) akisubiri kusomewa hukumu katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo huku akiwa amekaa sambamba na mpinzani wake kwa tiketi ya CCM Bi. Hawa Ng'umbi (wa tatu kushoto).
Mashabiki wa Chama cha CHADEMA wakiwa wamefurika ndani ya Mahakama kuu jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya kesi ya Mh. John Mnyika.
Wengine walikosa nafasi na kuamua kusimama nje ya Lango kuu la Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Wafuasi wa Chama cha CHADEMA wakimpongeza Mh. John Mnyika mara baada ya kuibuka mshindi dhidi ya kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na wafuasi wa Chama hicho pamoja na mashabiki wake nje ya Mahakama Kuu jijini Dar mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
"Pole sana Mama ndio Siasa hiyo" Mmoja wa Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi akimpa pole Bi. Hawa Ng'umbi (katikati) mara baada ya kutoka Mahakamani.
Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakiwa na sura za huzuni baada ya kutoka Mahakamani.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akifunguka na kuelezea furaha yake wakati wa mahojiano na Mwandishi wa ITV Godfrey Monyo nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.

Maandamano ya wafuasi wa CHADEMA wakishangilia ushindi wa Mbunge John Mnyika wakielekea katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho.
Mh. John Mnyika ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake katika Jimbo la Ubungo katika hukumu iliyotolewa leo na mahakama kuu ya Tanzania na kukifanya chama cha CHADEMA kuendelea kushikilia jimbo hilo.
 
Hii ndio hukumu ya ukweli. Hii inadhihirishia Umma wa watanzania CDM na Mnyika Ni chaguo lao. Lakini ile ya Segerea mbona Makongoro Hakubebwa aliishia kukimbia kama ndege ya kivita huku watu wakichana bendera za CCM huku wakiimba Fisadi fisadi. CDM kipenzi cha watu kwi! kwi! kwi! ha ha ha! Nape kwisha habari yenu
 
Kwa niaba ya gamba langu mwenyewe nakupongeza JJ Myika kwa kutetea vizuri jimbo lako la Ubungo.
Nafahamu kuwa Mnika ni mmoja wa vijana makini ndani ya CDM.
 
Hongera kamanda mpiganaji,sasa kinachofuata ni mapambano ya kuelimisha wananchi juu ya katiba mpya jumamosi
 
Magamba bwana hv mnanini?poleni sana,ama baada ya hapo hongereni kwa kumuongezea jj.mnyika umaarufu.
 
Udom tunakupongeza sana kamanda wetu Johm Mnyika wewe nijembe. Wasira anajisikiaje leo maana yeye jana alifukuzwa na wananchi wake kwenye mkutano.

Kushinda kesi ni kitu kimoja, ila kiukweli huyu jamaa hajafanya chochote jimboni kwake, ajipange vizuri, huu ni ushauri wa bure tunampa.:israel::israel:

 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom