Picha: Saa ghali zaidi duniani, ipo inayotengenezwa kwa miaka 25

explicity

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
207
140
Saa ni moja kati ya urembo ambao hutumika kupendezesha mkono au nyumba. Pia zipo saa za aina mbalimbali ambazo hutumika kuonyesha muda katika vyombo vya usafiri. Hizi hapa ni saa ghali zaidi duniani.

1. Breguet Grande Complication Marie-antoinette. Bei $30.000.000
8c80b9278c0beda2385dd5177de64350.jpg

Amini usiamini saa hii inagharimu dola milioni $30m. Saa hii ya kipekee ilichukua miaka 34 kuundwa. Yamkini aliyeagiza saa hii itengenezwe alikuwa ni mpenzi wa malkia wa Ufaransa wakati huo bi Marie Antoinette.
Yeye mwenyewe hakuwahi kuiona ama hata kuitumia saa hii kwani ilikamilishwa muda mrefu, miaka 34 baada yake kupigwa risasi na kuuawa.
Abraham-Louis Breguet alipokea agizo la kutengeneza saa hiyo mwaka wa 1782 hata hivyo aliaga dunia na ikambidhi mwanaye akamilishe kazi hiyo 1827 miaka minne baada ya kifo chake.

2. Chopard 201- Carat Bei: $25.000.000
c87dd2cde25a450acddbc8b89343b8c2.jpg

Saa inayoshikilia nafasi ya pili duniani katika orodha ya saa 5 bora duniani ni saa ya Chopard 201- Carat. Saa hii yenye thamani kubwa zaidi duniani katika kitengo cha mapambo imeundwa kutokana na almasi 874 nadra zaidi duniani.
Iliuzwa mwaka wa 2000 kwa thamani ya dola milioni $25.Wakati huo bei yake iligonga vichwa vya habari kote duniani.
Tofauti na saa ya kawaida , CHOPARD 201- CARAT haina umbo maalum kwani almasi imeunganishwa tu kiholela bila kuzingatia hali halisia ya matumizi yake.

3. Patek Philippe – Henry Graves, Bei:$11.000.000
8bc1c3b02dd9816843eec6d629f029b2.jpg


Saa hii ya Henry Graves ilikuwa saa iliyoweka rekodi ya kuwa ghali zaidi duniani kwa kipindi kirefu. Hata hivyo saa hii iliuzwa kwa bei ya dola milioni $9 mwaka wa 1999.
Amini usiamini saa hii ilitengenezwa mwaka wa 1933 mahsusi kwa ajili ya bwenyenye mmiliki wa benki bwana Henry Graves.
Mtengenezaji wake bw Patek Philippe anasema ilimchukua miaka 5 kuikamilisha saa hiyo ya kipekee.
Imejijengea sifa ya kuwa saa ya pekee duniani yenye uwezo wa kutekeleza majukumu 24 kwa wakati mmoja.
Hadi mwaka wa 2013 hakuna saa yeyote iliyowahi kuishinda saa hiyo kwa ubora.

4. Hublot – Big bang, Bei: $5.000.000
9d1d47ce13415e42c04b81a26a3c6b05.jpg

Saa hii aina ya Hublot -Big bang imeundwa kwa kuunganisha Almasi 1280 zenye ubora wa karati 3 kila moja.
Ilichukua mwaka mmoja wa kukata na kutayarisha Almasi hiyo inayotisha kutengeneza saa moja ya Big Bang.

5. Louis Moinet Meteoris Bei: $4.600.00
ad66163f1c726faaa13c306c60b72033.jpg

Ukiitaka saa hii sharti uwe na uwezo wa kulipa nauli ya roketi kwenda hadi kwenye mwezi ilikuchukua mawe ambayo itachongwa ilikuunda sehemu muhimu ya saa hii.
Hii ni baadhi ya saa nne duniani ambazo zinasehemu muhimu zinazotoka katika anga ya mbali.
Saa hii ni nadra sana hivi kwamba watengenezaji wake yaani Louis Moinet hufunga safari hadi anga ya mbali kuchukua vipuri vya saa hizi zenye nembo ya Meteoris.
Source:BBC
 
Yeuwiiiiiiie,auwiiiiiiieiie, keleuwiiiiiiiiiiiiiieeeeee,,auwiiiiiiiiee nife au Nibaki? Yeuwiiiiiiiiiiiiiiiie
 
The World’s Most Expensive Watches 2010
30 of 31next slideprevious slide
028_louis_moinet_meteoris.jpg





Louis Moinet
Meteoris
Price:
$4,599,487
In January, Swiss watchmaker Louis Moinet introduced a concept, Meteoris: a set of four tourbillion watches, each made out of other worldly materials, such as meteorite from Mars, the moon, an asteroid, and an ancient meteorite called "Rosetta Stone." The company got the materials from meteorite hunter Luc Labenne and worked with universities around the world to authenticate them. Meteoris comes with a planetarium that depicts the solar system and must be purchased as a set.
 
Back
Top Bottom