Picha: Rais Magufuli akiwa katika kikao cha AU Addis Ababa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Ikulu
VIDEO.

3.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.
C3VePGlWEAIu-Er.jpg:large

4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.
Screen-Shot-2017-01-29-at-3.49.43-PM-768x398.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga.
C3ZW34jWQAEDbPq.jpg

Rais Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU anayemaliza muda wake, Mama Nkosazana Dlamin-Zuma, Addis Ababa.
5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia.
1.jpeg

C3Wb3z_WMAAhlzp.jpg:large

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo jipya la kituo cha Amani na Usalama (JULIUS NYERERE) lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini Ethiopia.
 
Nimeona habari ITV mbona alikua hampi nafasi mkalimani jamani.. yeye anaongea mwanzo mwisho hana break hadi mkalimani kabaki kaduwaa hajui afanyaje

hii inasadifu hata huko Ikulu atakua yeye ndio muongeaji mwanzo mwisho wengine mawazo yao hawapi nafasi..
 
Back
Top Bottom