picha:RAIS KIKWETE AITEKA IGUNGA

picha:RAIS KIKWETE AITEKA IGUNGA

Asante kwa kunielewesha

Je itifaki inasemaje kuhusu hii bendera maana sijawai kuiona labda sign kwenye magari ya IKULU
Nchi imeshakuwa ya Kiswahili wala usishangae lolote. Bloger Michuzi anakuwa ndio mpiga picha wa Rais na yule Maro ana kazi gani? haya Mambo ya kupeana mapande hata kwenye taasisi nyeti ndio yametufikisha hapa.

Ndio maana usishangae kumuona Pasco yuko bize kumpamba Lowasa anajuwa kazi ya Salva Rweyemamu atapewa yeye na kazi ya kupiga picha anaweza kumchukuwa kishoka yeyote na kumpachika hapo Ikulu.
 
mbandika picha ni vizuri ungeelezea na hali halisi ya alichozungumza rais wetu na jinsi ya huo umati ulivyofika hapo na ni % ngapi ya watu wa mjini igunga wamehudhuria

1. Mapokezi yake yalikuwa jana na alipokelewa na wananchi wachache na vijana wa bodaboda na bajaji walichukuliwa kwa ahadi ya kupewa tsh.5,000/= jambo ambalo ni aibu na pia hata hiyo fedha yenyewe hawakupewa.

2. Juhudi za kusomba watu zimeanza tangu jana na watu walifikishwa ma maloli kama 5 hivi na wote walilazwa chini katika ofisi za ccm chakula cjui kama walipata. Aibu ya pili hiyo.

3. Leo siku ya mkutano watu wamesombwa na malori yasiyopungua 20 kutoka maeneo yote ya vijijini.

Aliyoongea mengi yalikuwa yamejaa ushabiki wa kisiasa na sio ya kujenga umoja na mshikamano kwa watanzania.
Kuna kauli ambayo niliona haikufaa kwa kiongozi wa nchi kuizungumza.
** alisema ujenzi wa daraja ni ahadi ya serikali ya chama cha ccm na ipo katika ilani ya ccm sasa anashangaa imekuwa ni kigezo cha kuvuliwa ubunge kwa kafumu, itabidi sasa tuwe tunafanya kampeni za kibubu kwani ukiongea tu inakuwa kosa na hapo mbeleni itabidi tutafute namna ya kuepukana na hili(namna gani anajua yeye) kwa kauli hii naona anapingana moja kwa moja na sheria za nchi hii. Pia alisema dr. Kafumu amekata rufaa wanachosubiri ni uamuzi wa mahakama kama watashinda au la lakini wakishindwa wataingia kwenye uchaguzi na watashinda kwa kishindo kuliko uchaguzi uliopita. Hapa watu wengi waliguna. Hapa inaonyesha ccm kazi wanayo.

Labda kitu kinachonishangaza kwa nchi yetu inatakiwa tutenganishe ziara za serikali na chama rais anapofanya ziara za serikali na kuingiza mambo ya chama yanaleta sintofahamu kwa watu wengine. Wenzetu usa rais akishachaguliwa iwe ndani au nje ya nchi anapeperusha bendela ya taifa huku kwetu nimeshangaa kuona mitaa yote ikiwa imetapakaa bendera za kijani (ccm) nimeshindwa kuelewa hii ni ziara ya serikali au chama.

umezoea cdm mnavyofanya arusha; kuna watu wana nyota za kupendwa hasa majina ya jk
john kennedy....................................jk
julius kambarage...........................jk
kakaya kikwete...............................jk
 
igu2.jpg

Rais Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga leo.
igu3.jpg

igu4.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utakaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga leo.
igu6.jpg

Rais Kikwete akisalimiana na mamia ya wananchi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.
igu1.jpg


igu5.jpg



Mamia ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.


ile picha ya kwanza ukiangalia nywele unaona mchizi yuko na acute syndrome.
 
kaka Michuzi unafanya vibaya kuchakachua picha za Rais

Kwanini usilete hali halisi ya mkutano? kwanini unachakachua picha

Huu mtindo utaauacha lini maana unadhalilisha chama chetu wewe huoni hizi picha kuwa ni tofauti?

Source:MICHUZI: JK AITEKA IGUNGA LEO

Nakala kwa Nape Nnauye, @Nnauye Jr, Mwigulu LM Nchemba W. J. Malecela, chama, Ritz

Huyu michuzi anaitaji kushughulikiwa la sivyo anaangamiza chama

Ikiwa Michuzi kakachua picha tuletee hizo zako ulizonazo; kumbuka kitu kimoja mh. Kikwete sio katibu wa chama ni Raisi wa JMT wananchi wa Igunga wamekwenda kushuhudia ni jinsi gani serikali iliyo chini ya chama makini CCM inavyoendelea na kazi yake ya kuwaondolea wananchi wa Igunga kero zinazowakabili.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
picha ya kwanza kizungumkuti usingeiweka maana imepigwa gizani

kwanini inavivuli vya giza?

Huyu aliyeleta alishindwa kufanya photoshop vizuri?

Haya mambo ndio yanazalilisha chama chetu

Sioni kuwa ni photoshop.

Picha ya kwanza . mpigaji ametumia flash na pia juu kuna bati, limerudisha mwanga ndio unamwona mkulu anangara, pia imepigwa kwa karibu na alipo mkulu, mkulu na suti yake ndio focus.

Hiyo ya pili, mwanga wa flash kama ilitumika haikugonga kwenye bati la jukwaa.
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Lohhh,

Wee ni jamaa wa home kama sikosei ila hizi propaganda zako zimenishinda kuvumilia. Ngoja nikuweke kwenye listi yangu ili nisivunje Computer. Samahani lakini na usichukulie PERSONAL.
Ikiwa Michuzi kakachua picha tuletee hizo zako ulizonazo; kumbuka kitu kimoja mh. Kikwete sio katibu wa chama ni Raisi wa JMT wananchi wa Igunga wamekwenda kushuhudia ni jinsi gani serikali iliyo chini ya chama makini CCM inavyoendelea na kazi yake ya kuwaondolea wananchi wa Igunga kero zinazowakabili.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Lohhh,

Wee ni jamaa wa home kama sikosei ila hizi propaganda zako zimenishinda kuvumilia. Ngoja nikuweke kwenye listi yangu ili nisivunje Computer. Samahani lakini na usichukulie PERSONAL.

Mkuu Sikonge
Kudai picha zenu nalo ni kosa? Jamaa yako anadai Michuzi kakakachua picha ndiyo sababu nimemuomba atuwekee zake alizonazo propaganda zipo wapi hapo mkuu?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Ikiwa Michuzi kakachua picha tuletee hizo zako ulizonazo; kumbuka kitu kimoja mh. Kikwete sio katibu wa chama ni Raisi wa JMT wananchi wa Igunga wamekwenda kushuhudia ni jinsi gani serikali iliyo chini ya chama makini CCM inavyoendelea na kazi yake ya kuwaondolea wananchi wa Igunga kero zinazowakabili.

Chama
Gongo la mboto DSM
Unamfahamu huyo unaebishana naye au ni speed za bangi ndio zinakupelekesha? huyo ni CCM kindakindaki na yupo front na siyo wewe Mkimbizi wa kiuchumi unayepractice siasa kwenye keyboard.
 
Asante kwa kunielewesha

Je itifaki inasemaje kuhusu hii bendera maana sijawai kuiona labda sign kwenye magari ya IKULU
kaka ni kwa sababu raisi mwenyewe hana hadhi tena hivyo anajiegemeza kwenye kitambaa kiitwacho bendera ndio tatizo la kandambili kukaa inapotakiwa kukaa kofia.tumekwisha sie nami nimo
 
Hivi hii bendera ya pili ni ya CCM au muungano?

Naomba mwenye kujua hii bendera aniambie

Kama sikosei itakuwa ni bendera ya Ikulu ile ambayo inakuwaga kwenye gari la rais, lakini sidhani kama kulikuwa na haja hiyo. Nchi inapelekwa kimagumashi tu.

Speed

Hiyo bendera ni bendera ya Rais, sio bendera ya Ikulu. Inapoonekana hiyo maana yake ni kuwa Rais yupo sehemu hiyo. Rais akiwa nje ya jengo la ikulu basi hiyo bendera hutaiona ikipepea Ikulu. Hiyo inamfuata/ inapepea/inapandishwa pale alipo ndani ya nchi.

Tanzania zipo serikali mbili na marais wawili. Hapa tusibabaike. Tembelea links.
http://www.crwflags.com/fotw/flags/tz-pres.html

http://www.crwflags.com/fotw/flags/tz-zan.html#zp
 
mkuu Sikonge, vipi naona una furaha sana leo. LIKE LIKE LIKE! Wasalimie Tutuo!
 
Last edited by a moderator:
igu2.jpg

Rais Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga leo.
igu3.jpg

igu4.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utakaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga leo.
igu6.jpg

Rais Kikwete akisalimiana na mamia ya wananchi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.
igu1.jpg


igu5.jpg



Mamia ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.

Inawezekana wengi wao hiyo ni nafasi ya kupumzika na kazi za jasho za kila siku basi na wala si kwa ajili ya umaarufu!
 
Hujakosea ni mamia mi nilifikiri ni maelfu bana
 
hakuna cha kuiteka wala kutawala haya ni malori yamepelekwa vijijini kubeba watu kwa ajili ya wale washamba kuja kumzubalia
 
Nimezaliwa na kukulia Igunga, siku zote anapokuja jk au kiongozi wa juu wa serikali kuna malori huwa yanaleta watu toka vijijini kuhudhuria mikutano na ndio nilichokiona katika picha hizi, walio mbele wanaonekana ni watu wa vijijini kabisa, huwa wanapewa vijiposho na pia huja kwa wingi maana kwao huo ni mtoko wa kuja mjini. Wana Igunga mjini huwa hawahudhurii mikutano ya aina hii isipokuwa wakereketwa wachache.
 
Back
Top Bottom