figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,165
- 64,515
Mayor wa Ilala na diwani wa Gongo La Mboto Jerry Silaa alipotembelea mtaa wa Gulukakwalala

Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia) na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe wakiongea wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Tabora Januari 10, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (yumo garini kushoto) akikagua sehemu ya kutua na kupaa ndege ya uwanja wa Tabora Januari 10, 2013 mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wake.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe Radhia Msuya mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataikfa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Tabora alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali.
Mwenyekiti wa asasi ya siasa ya Ulinzi na Usalama ya nchi za Jumuiya ya maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika (SADC) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine ambao ni wajumbe wa asasi hiyo wakati wa mkutano wa siku moja uliofanyika ikulu jijini Dar es Salaam .Wapili kushoto ni Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini,Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji(Watatu kushoto),Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(kulia) na wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu wa SADC Dr.Tomaza Salomao(picha na Freddy Maro).

Taifa Stars imefika salama jijini Addis Ababa tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Ethiopia. Mechi hiyo inataraijiwa kuchezwa (Januari 11) Addis Ababa Stadium kuanzia saa 11.30 jioni ambpo majira ya ( Tanzania na Ethiopia hatupishani saa). Stars imefikia katika Hoteli Hilton. inafanyia mazoezi katika uwanja wa Addis Ababa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Kimataifa wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo Perin L.Saint Ange,wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar, kwa ajili ya mazungumzo akiwa na ujumbe wake.

Hili ni moja ya bango la tangazo linalozuia kuegesha gari, au magari katika eneo hili lililopo karibu na Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam, lakini kwa sasa imekuwa ni tofauti kwani si gari moja ambalo labda waweza kusema limeegeshwa kwa bahati mbaya, la hasha ila eneo hili limegeuka kuwa maegesha ya magari tu kwa muda wote, sasa kama hivyo ndivyo Tangazo hili bado lina maana kuwapo neo hili?
<tbody>
</tbody>

Hali ya Baridi imezidi katika Jiji la Istanbul, nchini Uturuki ambapo imeelezwa kuwa hadi jana usiku ilifikia nyuzi joto 3, na kuwafanya wakazi wa jiji hilo kushindwa kufanya shughuli zao kwa kutotoka nje. Katika picha hizi ni baadhi tu ya picha zilizopigwa eneo la Mitaa ya Basiktas Istanbul, jana usiku. tunapenda kuwaondoa hofu mashabiki, wapenzi na wote wa Timu ya Yanga, ambao wanahisihali hii itawasumbua wachezaji wa timu hiyo. Ni kwamba hali hii ya baridi kali ipo katika Jiji la Istanbul tu kama ilivyo kwa nchi yetu ya Tanzania, ambapo Jiji la Dar es Salaam, lina hali ya hewa tofauti na mikoa mingine, ambapo Timu ya Yanga ipo katika mji wa ANTALYA, na hadi sasa imeelezwa kuwa bado barafu ipo na inazidi kadri muda unavyosogea.

Mji huo jinsi unavyoonekana ukiwa hauna watu kutokana na na baridi kuzidi kuwa kali.

Sehemu ya magari yakiwa yamejaa barafu...

Baadhi ya wakazi wa Istanbul, wakionekana mmoja kwa mmoja katika mitaa ya Basiktas.

Magari yakiwa yamejaa barafu....

Barafu ikiwa imetanda eneo la njia na maduka...

Hii ni hali halisi inayoendelea kwa sasa katika jiji la Istanbul......

Magari yakiwa na barafu.


Hii ni staili mpya kuezeka Bati? hii haiwezi kutufaa wengine wa jiji hili la Dar kutokana na hali halisi ya maisha ya matamanio na kila mmoja kupenda chake kuwa chake na cha wenzake kuwa chake, nahisi nyumba hii ingekuwa maeneo ya fulani ya hapa Dar, asubuhi wenyeji wangejikuta wanaangaliana na mawingu tu. Nyumba hii ipo eneo la Manzese, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini-Unguja hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana. Barabara hiyo imejengwa na Kampuni ya Mecco kwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,(wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Mindombinu, Mawasiliano Issa Haji Gavu,(wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Miundombinu,Mawasiliano,Dk.Juma Malik Akili,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kasakazini Unguja Pembe Juma,(kushoto) wakitembea katika Barabara ya Mfenesini-Bumbwini, baada ya kuifunguliwa rasmi jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
[h=3][/h]

Abiria wa kike mwenye asili ya kigeni 'Mzungu', akimsaidia dereva wake wa Bajaji, ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, baada ya usafiri wao wa Bajaji kupata pancha eneo la Lugalo Jeshini Barabara ya Bagamoyo, jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Abiria huyo mwanamama alionyesha ushirikiano wa hali ya juu huku akimsaidia dereve huyo kuinua Bajaji hiyo upande mmoja ili waweze kufungua tairi bovu na kubadili na kuendelea na safari yao na kuwaacha hoi watu wote waliokuwa wakiwaona katika harakati zao. Je angekuwa ni abiria mwanamke wa 'Kibongo' angeweza kutoa msaada huu wa hali na mali kwa kumsaidia dereva wake au ndo kwanza angesimamisha Bajaji nyingine na kusepa zake???

''Hadi kieleweke'' Abiria mzungu, akimsaidia dereva wake kuinua Bajaji ili kubadili tairi.....

''Moja, Mbili, Tatuuuu, Haya twendee........Imeinuka kazi sasa kufungua tairi.

Shuguli ilianza hivi Mdada mzungu akiwa na vijitambaa mkononi kwa ajili ya kushikia bodi la Bajaji kuepuka kuumia mikono.

Chumba cha chini ya Bahari kikionekana kwa mbali kikiendelea na matengenezo kwenye Hoteli ya Manta Resort Makangale iliyoko Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akishusha Nanga kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chumba cha chini ya bahari katika Hotelai ya Manta Resort, iliyoko Makangale Kaskazini mwa Kisiwa cha Pemba jana.

Meneja wa Hoteli ya Manta Resort Makangale mkoa wa kaskazini Pemba Bwana Metthew Saus {maarufu kama Babu kwanini) na msaidizi wake wakiwa tayari kumsubiri mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi kuweka jiwe la Msingi na Nanga katika ujenzi wa chumba cha chini ya bahari.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa na Mkewe Mama Pili Seif Iddi, wakiwa kwenye Boti kuelekea kwenye uwekaji wa jiwe la msingi na nanga ya ujenzi wa chumba cha chini ya bahari katika Hoteli ya Manta Resort iliyoko Makangale Mkoa Kaskazini Pemba.mia
