Picha nne ambazo ningependa Mh. Rais azione!

Picha nne ambazo ningependa Mh. Rais azione!

Nyie hamjaelewa. Swala hapa ni nchi haina chakula kwenye mahala yake. Hiyo nyingine ni jj company
 
Na si ajabu anataka kuwasahaulisha swala la Mr two oclock
 
FB_IMG_1483799526089.jpg
 
Mwisho wa mjadala ama ni mwanzo wa mjadala.

Unaleta picha za siku moja!. Kijani hicho ndicho kinaashiriakwamba hakuna njaa?
Unajua cropping calendar za mikoa yote ya Tanzania?
Hicho kijani ulichokiona kwenye google map kimetokana na mvua. Hizo mvua zimenyesha lini?
Unajua kwamba mabadiliko ya msimu wa mvua pia yanaweza kuwa sababu ya njaa kubwa, kwamba mvua imeharibu mazao na kusababisha mafuriko?
Unafahamu kwamba kijani cha nchi kinaweza kupatikana ndani ya juma moja la mvua? Je juma moja hilo linatosha pia kufanikisha kilimo, kupanda na kukomaza chakula tayari watu wasiwe na njaa?
Kama watu walilima mazao yakakosa mvua na kukauka, halfu mvua ikanyesha kuotesha nyasi, itahuisha na hayo mazao ghafula na kuyarudisha kwenye trend yake ya kawaida ya growth?

Unafiki ni mauti ya aibu.
Uko vizuri mkuu, hana uwezo wa kukujibu hizi hoja huyu jamaa
 
Mimi nadhani wataalam ndio wanataka kumwangusha mh rais. Najiuliza maswali kadhaa. 1. Ghala la taifa la chakula (Nafaka) lina chakula? Kama kipo namuunga mkono. Hakuna njaa.
2. Hicho kilimo, kimewekewa mkakati maalum?? Mwalim aliwahi kutangaza mpango wa kauli mbiu ya Kilimo cha kufa na kupona. Maredio yote yakakitangaza, watu wakalima mpaka juu ya lami. Je, huo ukijani kuna mkakati maalum wowote wa kuutumia?
3. Kwakuwa wengi haswa wapinzani wameanza kutangazia taifa kuwa kuna njaa, hivi kweli mh rais ana haja ya kulumbana na hao wapiga dili?? Kwani data zinadanganya?? Kama ana chakula cha kuwatosha wananchi ana hofu gani??
Nadhani hatuna haja kulumbana tungojee. Namba hazisemi uongo, na soon muongo wetu atajulikana tu. Tutakapo omba kibali cha kwenda kuuza chakula nje ya nchi, hakika weye uliyeleta hayo mahindi ya kulishia mifugo huko nje na sasa yameanza kuozea pale bandarini, utayala mwenyewe.
 
jamani picha za google earth huwa zinapigwa kwa mda mrefu,ili kuamini hili zoom hizo picha ukisha fungua google earth ndio utagundua kuwa kumbe google earth huwa inatumika kwa ajili ya location tu.mfano mm nataka kwend mbeya wilaya ya mbeya vijijin kata ya nsalala na sijawahi fika huko nikitumia google earth nitafika hapo
sasa basi hii haijatenngenezwa kwa ajili ya scientific analysis kama alizoleta mtoa post.
 
  1. Kipindi cha uhaba wa sukari alisingizia, kuwa wafanyabiashara wameficha.
  2. Likaja suala la fedha kuadimika, nazo akasema kuwa mafisadi wameficha fedha.
  3. Issue ya DANGOTE akasema ni wajanja walitaka kujinufaisha na mradi huo.
Sasa kwenye suala la njaa, wanasingizwa waandishi wa habari...!
Mwishowe atasema kufungwa kwa Yanga ni kwa sababu ya Faruku Karimu...
 
Kumekuwa na ubishani kuhusiana na hali ya njaa nchini na mengi yemeongelewa. Lakini ili kutatua ubishani huu na 'kumaliza' malumbano, ningeomba picha hizi zimfikie mheshimiwa Rais.

View attachment 458424 View attachment 458428 View attachment 458431 View attachment 458432

Assesment yangu ni hivi:

In general, sehemu kubwa kulingana na picha zilizopigwa na mtandao wa Google Earth zinaoesha kuwa zaidi ya asilimia sabini ya nchi iko katika hali ya ukijani.
Hiyo asilimia kama thelathini iliyobakia, acccording to Google Earth ni mikoa kama ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, na nusu ya Singida inaonekana kuwa na ukijani, ihali nusu ikionekana kuwa na hali ya jangwa.

Kwa kutumia picha hizi za google earth ninamuomba muheshimiwa kuwa watu wa mikoa hii ambayo inaonekana kuwa imeathiriwa na ukame, wapate msaada wa chakula cha dharula iwapo hali itabidi, pia wale walio na mifugo kwenye maeneo haya yalioathiriwa na ukame, waruhusiwe kuihamishiak wenye mikoa inayonekana kuwa na hali ya kijani kibichi kama inavyoonekana kwenye picha za Google Earth.

In general,
Naungana na mheshimiwa Raisi kukiri kuwa suala la ukame limekuzwa na wafanya biashara na wanasiasa wenye nia ya kuichafua serikali yake, kwani kutokana na assesment yangu ya picha za google earth, inaonekana sehemu kubwa ya nchi ikiwa katika hali ya ukijani....
Mwisho wa Mjadala...
Hii no zaidi ya hayari. Yaani rangi ya majani pori yanayokuwa ya kijani kwa mvua za kawaida tena kwa kutumia google earth ndiyo ushahidi wako wa hali ya chakula, mkuu upo serious au unafurahisha genge tu?
Kijani kinaweza kuwa kweli kipo lakini siyo suluhu ya kuwepo chakula.
 
Hakuna njaa inayoweza kuwa linked na ukame, sijasikia Dubai wanakufa njaa, tutumie akili zaidi kwenye kazi na sio nguvu
Dubai ni jangwa siyo ardhi yenye rutuba iliyokumbwa na ukame au umewahi kusikia mazao gani yanalimwa Dubai?
Unatia aibu kwa umri ulionao.
 
Mmeamua kuihonga na Google pia eenh Kasema Chakula hakitoki ng'o
 
  1. Kipindi cha uhaba wa sukari alisingizia, kuwa wafanyabiashara wameficha.
  2. Likaja suala la fedha kuadimika, nazo akasema kuwa mafisadi wameficha fedha.
  3. Issue ya DANGOTE akasema ni wajanja walitaka kujinufaisha na mradi huo.
Sasa kwenye suala la njaa, wanasingizwa waandishi wa habari...!

Na mvua je, nayo ni wanasiasa wamezuia.....???!!! (Ni swali nililomuuliza rafk ndotoni)
 
Upuuzi mkubwa!!!
Mvua ikinyesha kwa muda wa siku mbili majani ya porini yanaota kwa kasi lakini hii haina maana kuwa wanachi wamevuna mazao.
Pili kumbuka kuwa ukame haujatangazwa leo,mvua za vuli zimekosekana sehemu na suala la kufa mifugo is so obvious.
Hilo ndo watu wanashindwa kutambua
 
  1. Kipindi cha uhaba wa sukari alisingizia, kuwa wafanyabiashara wameficha.
  2. Likaja suala la fedha kuadimika, nazo akasema kuwa mafisadi wameficha fedha.
  3. Issue ya DANGOTE akasema ni wajanja walitaka kujinufaisha na mradi huo.
Sasa kwenye suala la njaa, wanasingizwa waandishi wa habari...!
Nyinyi mtanyooka tu. Mlitaka kutuuzia mbuzi wa kwenye gunia!. Mlitaka kutuuzia kanyaboya, jipangeni na punguzeni siasa za bei rahisi.
 
Hivi we jamaa umesomea wapi na inatumia nalysis gani kusema palipo na ukijani basi hakuna ukame


Kwanza naomba nikueleze kwamba hiyo picha ni ya satelite afu pili imepigwa kutokea juu hizo kijani mara nyingi zinaonyesha miti na vichaka ambavyo kiuhalisia haiathiriki na ukame wa mda mfupi sababu huwa na mizizi mirefu na imesambaa sana sasa niambia hayo mahindi na mpunga au mazao yanaweza kulimwa na kuvuta maji yaliyo mita za mbali kutoka ardhini tumia akili mahindi yamenyauka kwa ukosefu wa mvua unaleta picha za google earth
 
Back
Top Bottom