Picha: Mbunge msigwa afikishwa mahakamani

Picha: Mbunge msigwa afikishwa mahakamani

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,092
Reaction score
34,904
[h=3][/h]

​

Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama
IMG_4824.JPG

Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
IMG_4860.JPG

Watuhumiwa wengine wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi

IMG_4861.JPG

IMG_4873.JPG

Wakili wa Msigwa kulia akiteta jambo nje ya mahakama
IMG_4876.JPG

Kada wa Chadema Frank Mwaisumbe akiingia na viongozi wengine wa chadema mahakamani hapo huku wafuasi wao wakizuiwa nje ya mahakama
IMG_4882.JPG

Wafuasi wa Chadema wakiwa wamezuiliwa nje ya viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa wakati mbunge alipofikishwa katika mahakamani mchana huu
IMG_4890.JPG

Ulinzi mkali kweli kweli. PICHA: MBUNGE MSIGWA AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO - MPEKUZI HURU

​

[h=3]MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MSIGWA KWA DHAMANA.....[/h]

WATUHUMIWA 60 wa vurugu kati ya machinga na polisi mjini Iringa akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa wanafanyiwa utaratibu wa dhamana baada ya mahakama kukubali kupewa dhamana.

Awali watuhumiwa walisomewa mashitaka matatu huku mbunge akisomewa shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu.

Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na kwa sasa utaratibu wa dhamana unafanyika mbele ya mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa, Mheshimiwa Godfrey Isaya.

Mashitaka waliyosomewa watuhumiwa ni pamoja na shitaka la kwanza la mbunge ambalo ni kushawishi kufanya vurugu, huku wengine wote makosa yao yakiwa ni kufanya mkutano bila kibali, kuharibu mali kinyume na sheria ni kufanya vurugu.​

​

Safi sana afungwe ili iwe fundisho na kwa wabunge wengine
 
​

Miaka ya nyuma mtu ukifanya kosa, askari wanakuja wawili mmoja amevaa kiraia, mwingine ana sare wanamchukua mjumbe wa nyumba kumi, unachukuliwa kwa mahojiano. Sasa hivi, Nguvu kubwa - Rasilimali fedha na Watu inatumika katika mambo ambayo sio ya lazima. Hii pesa iliyotumika kununua mafuta na itakayotumika kufanya service ya magari haya, ingetumika kununua dawa katika moja ya hospitali nchini. Aidha, matumizi ya silaha za moto kama hizi yanawafanya wananchi wazoee kuona silaha kama ni kitu cha kawaida na kuamini kama hakuna amani.
 
Mkuu sawabho hakuna vita nchini mwetu ma askari wapo wengi hawana kazi ya kufanya ikitokea matatizo madogo ndio wanakwenda wengi utafikiri wanakwenda vitani hiyo ndio Tanganyika yetu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
kama nguvu hizi zingetumika kudhibiti magaidi wanao lipua makanisa na mabomu tungekuwa tumetumia vizuri rasilimali watu ya jeshi letu la polisi lakini mhhhhhhhh. sikio la kufa halisikii dawa
 
afungwe tu hata mimi naafiki mtu gani hata akili hana, ndio maana akaambiwa ni mchungaji wa nguruwe. hata nyie mnaemshabikia kwa kuanzisha vurugu ni vinyago tena vya mpapule. hamna akili.
 
Jambo ambalo watu wengi wameshindwa kulibaini kwa muda mrefu ni kuwa hata polisi iko katika mkakati wa kuiongezea chadema na viongozi wake umaarufu, na mpaka ss wameifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa bila kujali lawama wanazopewa kwani wao ni miongoni mnwa waathirika wakubwa wa utawala wa ccm, leo nimeona nifunguke tu
 
Sheria inasemaje kuhusu mbunge kufikishwa mahakamani? Je, sheria zimefuatwa?
 
afungwe tu hata mimi naafiki mtu gani hata akili hana, ndio maana akaambiwa ni mchungaji wa nguruwe. hata nyie mnaemshabikia kwa kuanzisha vurugu ni vinyago tena vya mpapule. hamna akili.
asiejua maana haambiwi maana
ipo siku utajua maana ya haya mambo
 
Back
Top Bottom