Picha mbaya

Picha mbaya

JAMANI SASA KAMA HEDIMASTA AU CLASS TICHA NI MWANA INAKUAJE HAPO CLASI AU SKULI?:whoo:😛arty:
 
Uwezi kujua labda na wenyewe hawamtambui rais,kwa kuwa wanajua hana rizaa ya watanzaniandiyo maana heshima ipo chini sana!
 
ITV wamejaribu kuonyesha jinsi JK asivyo kuwa serious sasa subili mchelea mwana hulia yeye
 
Nimeshangaa sana. ITV imeonesha Mh. Rais anatoa maelekezo na ufafanuzi muhimu kwa Baraza la Mawaziri & Manaibu wao HUKU BAADHI YAO WANAONEKANA HAWANA HABARI KABISA (NOT PAYING ATTENTION AT ALL) NA WENGINE WAKIANZISHA MIJADALA YAO PEMBENI NA MAJIRANI ZAO VITINI.

AMA

ITV wametoa picha mbaya (poor Video production) ya kuunga picha ambayo Rais anatoa maelekezo wakati picha ya Mawaziri ni ya wakati mwingine pengine wakiwa wanapumzika na kunywa.

AU

Baadhi ya Mawaziri wamejisahau na kuleta mazoea hata katika vikao muhimu vilivyoitishwa na mkuu aliyewateua na kuwaapisha mbele ya Watanzania.

N.B Endeleeni kuangalia ITV nadhani watairudia unless waitoe au wairekebishe na nitakuja juu wakiirekebisha bila kuomba msamaha kwa usumbufu waliousababisha!

Mkuu Kibunago, Picha niliyopata mimi ni hiyo AU yako ya pili. Zile picha za Waheshimiwa kupiga story zilipigwa kabla Mheshimiwa hajaingia ukumbini na alipoingia zikapigwa akiongea lakini wakati ya wanahabari wa ITV wakifanya Editing kwenye studio zao ama kwa makusudi ama Kwa Bahati mbaya wakaamua kuchanganya vipande vya picha walizochukua kuonyesha kwamba Waheshimiwa Mawaziri walikuwa wanapiga Story na kutafuna Big G wakati Mheshimiwa akiongea. Swali kubwa hapa linapaswa kuwa ni Je, Editing ile ilifanywa kwa makusudi na ITV ama imetokea tu kwa bahati mbaya?? Na kama imefanywa makusudi ni Kwa ajili gani na kwa faida ya nani?? Tuchemshe Bongo zetu kupata jibu.
 
Vyovyote vile kama wachache walivyochangia kwa umakini.

Kwenye Ama:
Bado ITV ilipaswa kuomba radhi maana haijalishi kuwa waliunga vipande tofauti vya matukio tofauti. Umakini na ufanisi ni media kuwasilisha mbele ya umma kile kisichosababisha utata usiokuwepo au kuweza kupotoshwa kwa urahisi. Maana unaona kama Wakuu walikuwa wanatafuna vitu au wanaongea wakati wa mapumziko halafu wewe ukaonyesha kama ni wakati Mkuu wa nchi anaongea nao tena kwa kwa mara ya kwanza akitoa msisitizo wa mwelekeo wake katika kipindi hiki na akiwataka kuwa makini na kuajibika basi watakuwa wamesababisha maumivu na pia wananchi kuwatafsiri vibaya viongozi wetu. Usumbufu kwa viongozi husika na kwa watizamaji ndio unapaswa kuombewa radhi!

kwenye Au:
Sina cha kusema; maana ndio kwanza unamwelekeza uliyemteua katika nafasi adhimu kwa ajili ya umma lakini yeye bila aibu anaonyesha dharau hata kabla hajaingia ofisini kuanza kazi. Mtu wa namna hiyo kwa mawazo yangu hafai na ningekuwa miongoni mwa watumishi husika ningefuatilia na kuuomba huo mkanda nikiungana na ITV ambayo role yake hapo ingestahili kusifiwa (as a change agent in the society) kuonyesha huo uozo na mara moja hatua ingechukuliwa kwa waliohusika. Hakika nilishtuka sana nikaruka na kusema moyoni kwa uchungu laiti ningekuwa nafanya kazi hapo basi tu maana si wote tutajaliwa kula na kunywa katika nyumba za Wafalme na Malkia!

Zaidi ya yote naomba tutofautishe sana hali ya mahusiano na mawasiliano baina ya Wabunge toka vyama tofauti wawapo Bungeni na mahusiano na mawasiliano katika kikao kama hiki (hata kama si Baraza la mawaziri proper) lakini ni kikao kimeitwa cha Mawaziri na Manaibu wote toka chama kimoja na aliyewateua wakakubali na kula kiapo mbele ya umma.
 
Nakubali tatizo sio ITV(hilo sina mjadala nalo), lakini napinga kwamba tatizo sio mkuu aliyekuwa akiongea.Tatizo ni yeye kuruhusu wateule wake kutompa heshima/attention anayostahili

Labda ungetusaidia, kutoheshimiwa udhaifu huwa unakuwa unasababishwa na nani cameraman au producer?
 
Hiyo ni ishara kuwa hawamtambui kama ni rais maana wanajua ameingia kwa kura za wizi. Hawawezi kumheshimu. Pili hana point ndio maana mtu huwezi kumsikiliza mtu anayetoa pumba

signature yako mie hoi! du
 
Kibunago unaelewa vikao vya baraza la mawaziri ni siri.
Kwa hiyo hata ingekuwa TBC lazima habari ya kikao cha baraza la mawaziri ingeambatana na Picha ambayo haiusiani na kikao hicho..
Sioni kama ni Tatizo la ITV au hao waheshimiwa.
 
Mtazamaji, Je kulinda siri ni kusababisha mkanganyiko?

Wengi wetu si wageni wa unachokisema na kwa taarifa yako hata huwa inabidi iandikwe kuwa NI KUTOKA MAKTABA AU IMEREKODIWA NK

Narudia kwa maneno mengine. Inaruhusiwa kuunga picha na maneno ambayo hayakuwa katika tukio moja lakini bado haimuondolei wajibu producer kutosababisha utata usio wa lazima ambao unaweza kutafsiriwa vibaya!

AMA , AU IKO PALE PALE!
 
Back
Top Bottom