Picha mbali mbali zinavyojieleza wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha mbali mbali zinavyojieleza wenyewe

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Sep 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Tatizo la usafiri...

  [​IMG]

  Wakazi wa kata ya Katumba Songwe, Wilayani Kyela, Mkoa wa Mbeya wakisaidiana kuweka sawa gunia la Mpunga katika daraja la Nepanepa linalopita katika mto Kiwira, baada ya gunia hilo kutaka kudondoka. Picha na Geofrey Kahango

  mtoto kama huyu anatakiwa kuwa shule
  [​IMG]

  Kijana akiwa amebeba gunia la mahindi katika eneo la stendi mjini Iringa.Vijana wengi hukatisha masomo na kujiunga katika kazi kutokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha.
  PICHA NA WILLY SUMIA


  Polisi:Tuko tayari kumlinda Ulimboka
  [​IMG]
  Mpita njia kipita pembeni mwa nyumba anayoishi Dk Steven Ulimboka katika eneo la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam jana ambapo sasa ulinzi umeimarishwa na kuwekwa uzio na geti ili kudhibiti watu.Picha na Michael Jamson
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Tuhuma: Biashara haramu
  [​IMG]

  Mtuhumiwa Salim Ali akirejeshwa rumande jana katika Mahakana ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dra es Salaam aliposhtakiwa kwa kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha binadamu na kuwatumikisha katika nchi za kiarabu. Picha na Venance Nestory


  Mwezi mtukufu Ulivyokuwa....

  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete akiwapa zawadi watoto yatima na walemavu walohudhuria futari iliyoandaliwa Ikulu, jijini Dar es Salaam, juzi jioni. Picha na Ikulu


  Mtoto akitoka shambani
  [​IMG]


  Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Katoju, katika kijiji cha Buhanga, wilayani Bukoba Vijijini, Leah Sebastian akitoka shambani huku akiwa na mzigo wa kuni kichwani, kama alivyokutwa mwishoni mwa wiki. Picha na Phinias Bashaya
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Askari wa Usalama barabarani akijiandaa kuendesha daladala inayofa safari zake kati ya Ubungo na Mnazi mmoja baada ya kulikakamata kutokana na kuzimika katikati ya Barabara ya mandela eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam jana huku dereva wa gari hilo akimua kuondoka na kumwachia gari hilo.Picha na Venance Nestory  Bodaboda:Mgomo
  [​IMG]

  Baadhi ya vijana wanaofanya huduma ya usafiri maarufu kama boda boda katika Jiji la Arusha, wakiwa wameegesha pikipiki zao eneo la Sakina, baada ya kugoma kufanya kazi wakipinga kulipishwa ushuru wa maegesho wa Sh 500 kwa siku. Picha na Mussa Juma


  Sikukuu:Ununuzi

  [​IMG]

  Wananchi wakiwa katika mtaa wa Congo jijni Dar es Salaam jana, wakifanya manunuzi ya vitu mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya Idd inayotariwa kuwa keshokutwa kutegemea na kuandama kwa Mwezi . Pichana Michael Jamson
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Nanihii na nanihii wakijirusha kwa raha zao
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  FFU wa Ngoma Africa band imewasha moto,TUBINGEN

  [​IMG]
  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya,Ngoma Africa Band siku ya Jumamosi 11.8 .2012 walishambuli jukwaa na la
  International Africa Festival 2012,Tubingen,Ujerumani, na kuhakikishia washabiki kuwa FFU ni tishio la kimataifa !

  Taswira katika Taifa

  [​IMG]

  Mtoto Salima Rashid wa Kijiji cha Msufini Kata ya Embeti akikusanya mahindi kwa ajili ya kwenda kupukuchua yawe tayari kwa kwenda kusagwa katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.Picha na Pamela Chilongola
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Watalii: Wakiandika dondoo
  [​IMG]
  Watalii kutoka nchini Italia wakiandika dondoo ndan ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara walipokuwa wakitembelea hifadhi hiyo juzi. Picha na Filbert Rweyemamu


  Zitto Kabwe akihutubia wananchi
  [​IMG]


  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe akihutubia wananchi wa Mji wa Katesh,mkoani Manyara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mnadani mjini humo, juzi. Picha na Habel Chidawali

  [​IMG]

  Mbeba mizigo akivuka barabara ya Kawawa maeneo ya Karume akiwa amebeba mizigo ya mifuko ya salfeti jana jijini Dar es salaam. Picha na Aika Kimaro
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Pata cheo mtu:
  [​IMG]

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, akimvisha cheo cha Meja Jenerali kwa niaba ya rais, Meja Jenerali Grace Mwakipunda, ambaye kwa sasa ni kaimu mkuu wa utumishi Jeshini.  Lowassa na vijana CCM
  [​IMG]

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Edward Lowassa (kushoto) akiwapungia
  mkono vijana wa chama hicho alipokuwa akiwasili makao makuu ya chama
  hicho mjini Dodoma jana kuhudhuria kikao cha Nec, jana. Picha na Edwin
  Mjwahuzi  Mabasi ya wafungwa yazinduliwa

  [​IMG]


  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbande (mwenye suti) akizindua moja ya mabasi ya kubebea wafungwa yaliyonunuliwa kupitia programu ya maboresho katika sekta ya sheria jana jijini Dar es Salaam. Nyuma yake ni Mratibu wa programu ya Maboresho katika sekta ya sheria Emmanuel Mayeji.Picha na Aika Kimaro
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  'Wewe mimi nakamatwa na askari wakubwa sio wewe au najipeleka mwenyewe'

  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akizozana na askari waliotaka kumkamata kwa kesi nyingine baada Hakimu Mkazi Mfawidhi wa kisutu kumwachia huru jana, katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili.Picha na Silvan Kiwale


  Mtikila ashinda kesi

  [​IMG]

  Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila akipunga mkono kizimbani baada ya kushinda kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Picha na Silvan Kiwale


  Mafunzo ya tiba
  [​IMG]

  Kaimu Mkuu wa kitengo cha mafunzo ya tiba ya magonjwa ya tumbo, Dk. John Rwegasha (kulia) akimuonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo Kikuu cha Philipps cha Ujerumani, Profesa Rudolf Arnold (katikati) baadhi ya vitendea kazi kwa ajili mafunzo ya magonjwa ya mfumo wa chakula na ini yaliyoanza jana jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Medical Equipment (TAMEQ) Alexander Riefer. Picha na Rafael Lubava
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kikwete na Kikao

  [​IMG]

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiimba wimbo wa chama hicho
  pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa
  CCM, Wilson Mukama wakati wa kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya chama
  hicho kilichofanyika katika ukumbi wa White House, mjini Dodoma jana.
  Picha na Edwin Mjwahuzi

  [​IMG]

  mu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Pamela Kalala (kushoto),akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana,baada ya kusomewa shitaka la kuomba rushwa ya Shilingi milioni tatu.Picha na Michael Matemanga


  Furaha:Wahitimu darasa la saba

  [​IMG]

  Wanafunzi walihitimuDarasa la saba Wakifurahia
  Wanafunzi waliohitimu darasa la saba wa shule ya Msingi Kigogo ya jijini Dar es salaam,wakishangilia baada ya kumaliza kufanya mitihani yao ya Taifa jana.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Biashara:Mahindi............

  [​IMG]

  Mfanya biashara wa mahindi katika soko la Makanya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akisubiri wateja ambapo debe moja la mahindi huuzwa kwa Sh6,000. Picha na Dionis Nyato.


  Miili ya askari wa kulinda amani waliofariki kwa ajali ikipokelewa
  [​IMG]

  Askari wa Jeshi la Wananchi (Jwtz) wakiwa wamejipanga wakati wa kupokea miili ya Askari wa kulinda amani waliofariki kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan wiki iliyopita Kwa ajali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Air Wing Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix


  Teknolojia:Matumizi ya gesi
  [​IMG]


  Mhadhiri wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Augustine Katani, akiwaelekeza waandishi wa habari namna gari la gesi linavyofanya kazi wakati wa mkutano wa 10 wa mwaka wa wahandisi, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.Picha na Michael Jamson
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Korti yamaliza mgogoro wa Anglikana Arusha

  [​IMG]

  Askofu wa Kanisa la Anglikana, Stanley Hotay akitoka nje ya Kanisa la Christ mjini Arusha Jumapili iliyopita. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na baadhi waumini wa Kanisa hilo.
  Picha na Filbert Rweyemamu

  Serikali itatue tatizo la maji ili kuondoa kero kwa wananchi

  [​IMG]
  Maria Idabu mkazi wa Kimbanyasi, wilaya ya Chemba, mkoa wa Dodoma akiswaga punda kwenda kutafuta maji katika kijijij cha Paranga. Kutokana na safari hiyo kuwa ngumu huwalazimu kusafiri na vifaa na chakula cha kutumia kwa siku watakazokaa huko. Picha na Shakila Nyerere

  Ajali;Basi

  [​IMG]

  Basi likiwa limepinduka juzi Kijiji cha Bukulu, Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma lilipokuwa likielekea mkoani Arusha kondakta wa basi hilo alifariki juzi. Picha na Shakila Nyerere
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Waziri Nchimbi aunda kamati
  [​IMG]

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dr Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, wakati wa kuitangaza kamati ya kuchunguza kifo cha mwandishi wa habari wa mkoa wa Iringa, Daudi Mwangosi. Kushoto ni kamishna wa Oparesheni wa Polisi, Paul Chagonja na kamishna wa utawala wa Rasilimali wa jeshi hilo, Clodwin Mtweve. Picha na Michael Jamson


  Marais: Mkutano

  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Asasi ya Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Mandeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza marais wenzake Hifikepunye Pohamba wa Namibia (kushoto), Armando Emílio Guebuza wa Msumbiji ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Jamhuri nya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila kuangia katika makutano wa asasi hiyo Dar es Salaam jana kujadili masuala ya usalama wa DRC. Picha na Emmanuel Herman


  Mazishi ya Mwangosi


  [​IMG]

  Mjane wa Daudi Mwangosi aliyekuwa mwandishi wa Channel Ten,Itika akilia kwa uchungu juu ya kaburi la mumewe kwenye mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Kasoka wilayani Rungwe mkoani Mbeya jana.Picha kwa hisani ya mbeyayetu.blogspot.com
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mbunge Nchemba ashughulikia kero ya maji Makunda
  [​IMG]

  Mbunge wa Iramba Magharibi, mkoani Singida, Mwigulu Nchemba na wananchi wa Kijiji cha Makunda, wakitazama mashine ya kusukumia maji iliyonunuliwa na mabunge huyo ili kukabiliana na tatizo la maji katika kijiji hicho.
  Picha na Gasper Andrew


  Tatizo la maji
  [​IMG]

  Mtoto akichota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwenye bomba lililokatika wakati wa upanuaji wa eneo la reli Mabibo jijini Dar es Salaam kupisha mdadi wa treni ya abiria kutoka Ubungo kwenda katikati ya jiji la Dar es Salaam.Picha na Silvan Kiwale


  Tanesco yazidi kuwabana wateja sugu
  [​IMG]

  Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika msururu kwa ajili ya kununua umeme jana. Usumbufu huo ulitokana na Tanesco kufanya maboresho kwa watumiaji wa mita za Luku. Picha na Salhim Shao
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Shahidi aeleza jinsi mbunge alivyokamatwa kwa rushwa

  [​IMG]
  Mbunge wa Bahi, Omary Badwel (Katikati) akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkaza Kisutu jijini Dar es Salaam jana baada ya ushahidi wa kesi inayomkabili ya kuomba na kupokea rushwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo kutokamilika. Picha na Venance Nestory


  Mauaji yamtesa IGP
  [​IMG]
  Marehemu Daud Mwangosi


  Mafao

  [​IMG]

  Mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyovunjika mwaka 1977, Pascala Maziku akiomba dua, kwenye mkutano wa wastaafu hao uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, ambapo alikua akimuuliza kama kweli wana haki ya kulipwa mafao ya au la. Mzee huyo ana anadai kuwa alipewa ishara ya kuwa wa haki ya kupatiwa mafao. Picha ns Zacharia Osango
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Askari aliyefariki Darfur kuzikwa Lindi

  [​IMG]

  Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Marehemu Yusuph Said (mmoja wa wanajeshi waliofariki akilinda amani huko Darfur, Sudan) katika eneo la Kingugi jijini Dar es Salaam jana. Waombolezaji hao walikusanyika tangu juzi. Picha na Michael Jamson


  Hawa Ngulume afariki dunia jijini Dar es Salaam

  [​IMG]

  Ndugu wa Mwanasiasa Mkongwe Hawa Ngulume aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Lugalo, wakilia wakati wakiwasili nyumbani kwake Goba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana.Marehemu aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Mbarali na Bagamoyo atasafirishwa leo jioni kwenda Singida kwa mazishi.Picha na Silvan Kiwale


  Askofu Katoliki afariki dunia

  [​IMG]
  Askofu Paschal Kikkoti
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Sitta:Tishio la Urais Chadema ni Dr. Slaa
  [​IMG]

  Dr. Wilbrod Slaa  Wanawake:Tusaidiwe

  [​IMG]


  Zuwena Ibrahim, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) jijini Dar es Salaam jana, ambako yeye na mwenzake Hadija Mohamed (kushoto), walikwenda kuomba msaada wa kisheria. Picha na Michael Jamson


  Mishale:Tumekamata
  [​IMG]
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akionyesha kwa waandishi wa habari jiji Dar es Salaam jana silaha za kijadi zilizokamatwa kwenye operesheni maalumu ya kuwaondoa wavamizi wa mashamba katika eneo la Madale Nyakasangwa wiki ilipita.Picha na Fidelis Felix
   
 17. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,580
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  RIP konda, huenda alikaa mlangoni basi lilipoanguka likamlalia.
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,858
  Trophy Points: 280
  hiyo ya diamond na wema lol! hivi kwanini jamani wema anajiachia hivi??? sikatai anahaki ya kupenda ila hadi kubambwa akiwa kwenye pozi kama hilo sehem isiyokuwa na faragha ni aibu na kuidhalilisha na funny enough yeye ndo anaonekana kama kazidiwa sana wakati mwenzie akiwa kalala fofofo lolest. sijaipenda kabisa.

  niliyoipenda ni ya jembe langu mh Edward Lowassa huyu ni jembe langu kwanza angalia tu alivyo mkakakamavu kisha angalia anavyojiamini tofauti kabisa na hata alivyo waziri mkuu Pinda na mwenzie Kikwete. wasipompa nafasi ya kugombea urais CCM wajue watakuwa wamewapa CDM nchi kilainiii kama wananawa.
   
 19. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,485
  Likes Received: 4,757
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu unatisha sana
   
 20. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Hivi ulimboka hata kazini haendi?hatembei?
   
Loading...