Picha: Mauaji ya Kimbari Rwanda (Rwanda genocide)

samsun

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
7,386
Reaction score
5,968
Hebu tuone waliopitia wenzetu ili tujifunze kitu hapa.


Inadhaniwa zaidi watu 800,000 walikufa kwenye mauaji haya.


Maiti zilizagaa mitaani na mbarabarani, kwa wakati huo kila mtu aliangalia nafsi yake tu.


Nani atamsaidi mwenzake, watoto walipoteza karibia familia nzima.


Chakula hakuna,na maji yote yalijaa damu za watu.


Hata kama hatujali kuhusu sisi basi tuwatafakari watoto wetu wataishi ktk mazingira gani.


Hakuna wa kumsaidia, ni kilio chake kwa mama yake kipenzi.




Unabakwa na kisha wanakuua.


Mitaani utazika ya ndugu yako yupi uache yupi.


Watoto kuona maiti walishaanza kuzoea.


Kila sehemu ni maiti tu.


Ni vilio visivyo na msaada,wapo waliosubiri na wao wauliwe kwa maana ana alichobakisha.


Wahutu na watutsi wote ni wahamiaji.


Maiti zilikusanywa na kutupwa kwenye kaburi la pamoja kisha kijiko kinafukia.


Baadhi ya watu waliobahatika kubaki wamening'iniza picha za wapendwa wao waliokufa.


Hakuna mwenye tabasamu,ni kumbukumbu mbaya mno maana inasemekana wengine wanawajua waliowauwa ndugu zao ila wameombwa kusameheana ili maisha yaendelee mbele.
 
Haya mauaji huwa najiuliza sana kama siku 100 tu waliuana kiasi hicho wangeendelea mwaka mzima si wangemalizana kabisa
 
Kujenga chuki kati ya makundi mawili! Chuki inakua inafikia hapo! Tujitafakari
 
Bado siamini idadi ya waliopoteza maisha nahisi km kuna siasa imeingizwa ktk hii ishu
 
Haya mauaji huwa najiuliza sana kama siku 100 tu waliuana kiasi hicho wangeendelea mwaka mzima si wangemalizana kabisa
Kama umeona hizo picha, ukikutana na mtu akakwambia ni Mnyarwanda au Mrundi mwogope - ni zaidi ya hatari na hao ndo wanaleta shida kwenye mapori mkoani Kagera. Jamaa wana roho za ajabu.
 
pole yao sana[emoji27][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Bado chuki itaendelea kuwatafuna kila wakikumbuka hayo mauaji
 
Me nakumbuka mwaka huo nilikuwa ngara braza wangu alikuwa RED CROSS dahhh ilikuwa inatisha walikuwa wanaopoa maiti za watoto mto kagera zimetungwa km mshkaki.mbwa walishiba rwanda kwa kula maiti yaani nakumbuka ingawa nilikuwa mdogo kuna mzungu alikuwa anachukua video kwa helicopta anasema alikuw mita karibu 2000 ila alikuwa anashiba harufu ya maiti.daaahhh yale mauaji ilikuwa shida silaha ni mapanga,shoka na majembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…