chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,385
- 24,939
Majambazi wakamatwa Kariakoo akiwemo raia wa India.
Tarifa zaidi zinakuja.
Tarifa zaidi zinakuja.
Nilikuwa mitaa hiyo muda tukio linatokea. Ilikuwa mida ya SAA tano mtaa wa Swahili.
Walivamia nyumba moja hapo Na kuingia katika Ghorofa ya juu kabisa, wakamfunga Dada wa kazi mdomo. Walichokuwa wanatafuta katika nyumba hiyo hakijukikani. Yule Dada alifanikiwa kutoka kwa kuruka dirishani (tukio hilo ndio lilivuta watu wakidhani Ana ugonjwa wa akili au malaria imepanda kichwani).
Alifanikiwa kupitia zile nyaya nyaya sijui ni za umeme au simu na kushuka hadi ghorofa ya kwanza ambapo alidakwa Na waliokuwa hapo. Ndio akatoa nguo aliyofungwa mdomoni Na kupiga kelele kuwa kuna majambazi katika nyumba hiyo.
Nadhani alipotoka nao jamaa walitoka Na alipopiga kelele aliwaona wakiwa chini hapo ndio akasema ni hao. Jamaa wakashushiwa kipigo Na Askari walikuwa wameshafika tayari.
Nadhani walikuwa ni wezi tu wa kawaida maana hawakuwa Na silaha yoyote.
WATU wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wamenaswa leo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kupewa kichapo ‘hevi’ kutoka kwa wananchi wenye hasira kali waliokuwa eneo la tukio.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, majambazi hao wawili akiwemo mmoja ambaye ni raia wa Kihindi wamekamatwa Mtaa wa Swahili na Mchikichi, Kariakoo na wanadai raia huyo wa Kihindi anajulikana kwa jina la Samir.