Picha: Maaskofu watoa tamko kuchomwa kwa makanisa jijini Dar es salaam

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Pg2..JPG

Askafu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Dk. Alex Malasusa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutoa tamko la maaskofu kutokana na kuchomwa kwa
makanisa katika vurugu zilizotokea Mabagala jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Katibu wa Mkuu wa Baraza Maaskofu Tanzania, Padri Anton Makunde na Padri Silvester Gamanywa .

_MG_8182.JPG

Katibu wa Mkuu wa Baraza Maaskofu Tanzania, Padri Anton Makunde akisoma tamko la maaskofu kutokana na kuchomwa kwa makanisa katika vurugu zilizotokea Mabagala jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Picha na Mdau Dande Francis
Sisi maaskofu na viongozi wa makanisa ya kikristo kutoka CCT, TEC na PCT baada ya kusikia na kuona katika vyombo vya habari juu ya uvamizi wa makanisa tumechukua fursa ya siku hii ya leo ili;-
1)Kujionea wenyewe madhara yaliyotokea
2)Kutoa pole kwa waumini wetu
3)Kushiriki pamoja uchungu wa madhara yaliyotupata
4)Kuwepo kwa pamoja namna ya kukabiliana na uvamizi huo

Baada ya kutembelea maeneo yaliyovamiwa na kujionea uharibifu uliotokea
1)Tumeona uchungu na masikitiko ya kwamba watanzania tumefikia kiwango hicho cha kumtendea jirani yake
2)Tunatambua subira na uvumilivu mkubwa uliooneshwa na wakristo kuepusha majibizano ambayo yangeweza kuleta athari kubwa zaidi.
3)Tumeziona juhudi za jeshi la polisi katika kudhibiti hali ya vurugu na kuepusha kupoteza uhai wa raia.

Katika wakati huu
1) Tunawaalika wakristo wote kutolea sala na maombi kwa Mungu aliye mlinzi wet,usalama na ulinzi wetu uko mikononi mwa Mungu pekee.
2)Tunatambua kuwa usalama wa wafuasi wa Kikristo ni haki ya msingi kama raia wengine wowote, ni mategemeo yetu kwamba wakristo na nyumba zao za ibada vinastahili kuhakikishiwa usalama.

Tunapenda kuwaambia Wakristo wenzetu kwamba kikao chetu cha leo kimetupa fursa ya kujionea wenyewe hali halisi ya uvamizi, kwasasa tunajiandaa kuchukua hatua muafaka. Tutawarudia hivi karibuni mbele ya vyombo husika yale yaliyo maamuzi yetu.
Kwa wakati huu tunawaomba muendelee kuwa wavumilivu na watulivu na muwe macho katika kulinda mali na nyumba zetu za ibada kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

Tunawapa pole wote na kuwatakia Baraka za Mungu.

5996140674267894691-4819547071237133193

Tatizo Halihusu hawa MAASKOFU; Tatizo zaidi liko kwenye SIASA za NCHI; Uongozi wa NCHI ndio Unaopaswa Kuweka VIKAO na WAANDISHI wa HABARI kuona ni njia gani ya kutatua TATIZO HILO...
 
Sisi maaskofu na viongozi wa makanisa ya kikristo kutoka CCT, TEC na PCT baada ya kusikia na kuona katika vyombo vya habari juu ya uvamizi wa makanisa tumechukua fursa ya siku hii ya leo ili;-

1)Kujionea wenyewe madhara yaliyotokea
2)Kutoa pole kwa waumini wetu
3)Kushiriki pamoja uchungu wa madhara yaliyotupata
4)Kuwepo kwa pamoja namna ya kukabiliana na uvamizi huo

Baada ya kutembelea maeneo yaliyovamiwa na kujionea uharibifu uliotokea
1)Tumeona uchungu na masikitiko ya kwamba watanzania tumefikia kiwango hicho cha kumtendea jirani yake
2)Tunatambua subira na uvumilivu mkubwa uliooneshwa na wakristo kuepusha majibizano ambayo yangeweza kuleta athari kubwa zaidi.
3)Tumeziona juhudi za jeshi la polisi katika kudhibiti hali ya vurugu na kuepusha kupoteza uhai wa raia.

Katika wakati huu
1) Tunawaalika wakristo wote kutolea sala na maombi kwa Mungu aliye mlinzi wet,usalama na ulinzi wetu uko mikononi mwa Mungu pekee.
2)Tunatambua kuwa usalama wa wafuasi wa Kikristo ni haki ya msingi kama raia wengine wowote, ni mategemeo yetu kwamba wakristo na nyumba zao za ibada vinastahili kuhakikishiwa usalama.

Tunapenda kuwaambia Wakristo wenzetu kwamba kikao chetu cha leo kimetupa fursa ya kujionea wenyewe hali halisi ya uvamizi, kwasasa tunajiandaa kuchukua hatua muafaka. Tutawarudia hivi karibuni mbele ya vyombo husika yale yaliyo maamuzi yetu.
Kwa wakati huu tunawaomba muendelee kuwa wavumilivu na watulivu na muwe macho katika kulinda mali na nyumba zetu za ibada kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

Tunawapa pole wote na kuwatakia Baraka za Mungu.
 
Ameni. Nasi twasema tuko tayari kutenda mliyoyanena kwetu kwa kadri Mungu wetu alivyowajalia kuyaneena na atakavyotujalia kuyatenda.

Ameni, tutazidisha Sala la Maombi kwake yeye Mungu wetu ili atujalie amani na upendo maishani mwetu.

Ameni, tutaendelea kumsihi atujalie maarifa na nguvu kutwaa ushindi dhidi ya vitisho vilivyombele yetu.
 
Tumeanza lini kupeana "matamko" kwa link?
Mkuu nngu007 nakuomba basi weka sawa hii taarifa, maana link ushapewa hizo, zifungue edit thread.
Wengine tupo kwenye vitochi hivi.
 
Inatia moyo kuwa na jamii kama hii kwa kweli!
Sijui na wenyewe wangeshika petrol na kwenda miskitini ingekuaje?
 
maaskofu wetu jamani, nasi tunaomba ruhusa kwenu mtubariki tuonyeshe kile alichoonyesha Bw. wetu Y. Kristu alipokuta biashara ikifanyika hekaluni... upole wetu haumaanishi kuwa hatujui kujibu mapigo! Mungu wetu wa amani uwajalie wenzetu watambue kuwa sisi sote ni ndugu twapaswa kuishi kwa upendo. Amen
 
Back
Top Bottom