Picha kutoka gazeti la Mambo Leo la mwaka wa 1934. Watazame Mangi waliopambana na Rajabu Kirama - Mangi Ngilisho na Shangali

Na kwako ni pale Nkuu Sinde njia nne.. Mpaka leo ni wauzaji wakubwa wa nyama..

Kuna mwaka ule waislam wanalilia kuchinja wachinje wao tu, kule Machame hawa akina Rajabu wakaivalia njuga, eti wachinje wao na kuuza nyama wauze wao wakati waislam ni 0.001 ya population yote Machame. Wakristo wala hawakutaka fujo, wakawaambia sisi tuacheni tutanunua kwenye bucha za wakristo wenzetu nyama hizihizi mnazoziita najisi na nyie wauzieni waislam wenzenu. Mbona wenyewe waliomba poo na kukubali yaishe..

Waislam kule uchagani ni tone tu lakini tunaishi nao vizuri bila matatizo yoyote, ila kama kwenye ile jamii waislam wangekuwa ni wengi kuliko wakristo sijui hata hawa wakristo wangeishije..
Hata nkuu ndoo njia nne pale wamejazana na wengi ni Kutoka ukoo wa Nkya..
Ni wachinjaji wazuri .
Hilo swala la uchinjaji nilikuwepo wakati huo diwani akiwa Rajabu Nkya ...Anaishi waramu pale... Wakristo walipoamua kununua nyama Kwa wakristo wenzao wakaanza vitisho...Nakumbuka kuna mzee walimwekea risasi na petroleum buchani kwake ila Hilo halikufua Dafu.
 
Hata mimi ndivyo navyofahamu.Ukoo huu ulikuwa ni ukoo wa wachinjaji miaka na miaka,toka enzi na enzi.

Ilipoanza kazi ya uchinjaji "rasmi" kwa minajili ya dini,kwa maana ya wachijaji LAZIMA wawe Waislam,kazi hii ilichukuliwa na Wasomali na Wagunya kutoka Mombasa,Mzee Rajabu hakutaka kuipoteza kazi hii,pale alipoamabiwa ili aendelee na kazi yake ni LAZIMA asilimu,na wao ukoo wa Nkya walijipa "haki miliki" ya kuchinja,akaamua kuwa Muislam,na waliomsilimisha ni hao Wagunya wa Mombasa.
Hapo ndio Uislam ukaingia eneo la Uchaga na hasa Machame,ili kuendelea na kazi yao ya uchinjaji,ukoo ukawa wa Kiislam..Imeenda hivyo mpaka kesho,wengi ni wauza nyama na wachinjaji na wauza mirungi toka Mombasa.

Hili ndio shina la ukoo wa akina Said Mwema
Umenena mkuu.
Hata ndugu wengi wa Said mwema wameoa wasomali ...from Mombasa na Somalia yenyewe ukifika nkuu sinde Ukiulizia Kwa Mzee kasa Utaona Ni wasomali kabisa.
 
Umenena mkuu.
Hata ndugu wengi wa Said mwema wameoa wasomali ...from Mombasa na Somalia yenyewe ukifika nkuu sinde Ukiulizia Kwa Mzee kasa Utaona Ni wasomali kabisa.
Na huu ndio ukweli,ukweli unaoelezea chanzo cha Uislam kuingia Uchaggani kwa kupitia eneo la Machame.

Wasomali unawaona hapo Nkuu Sinde ni kwa sababu ya Uchinjaji,walikuwa wachinjaji katika mnada wa eneo ambalo lilifahamika kama "Boma la Ng'ombe",sababu palikuwa na boma kubwa ambalo Wamaasai toka uwanda wa eneo la sasa la Manyara(Mererani) na eneo la Ruvu ya Same walileta mifugo yao hapo na kuifungia wakisubiri mnada.

Na siku ya Mnada waliochinja walikuwa Wasomali tu,lakini kwa sababu ukoo wa akina Rajabu na wao kwa asili walikuwa ni wachinjaji,hawakutaka kuipoteza hiyo "haki yao ya kimila",na kwa sababu baadae kigezo ilikuwa LAZIMA uwe muislam,Mzee Rajabu hakuona tabu hiyo,na katika hili palizuka mgogoro wa kimila,hapo ndipo chimbuko sasa la Uislam kuingia eneo hilo na kufanya kuwa na Wachagga waislam ambao koo zao zimechanganyika na Wagunya wa Mombasa na Wasomali.

Mpaka leo,eneo hilo lina "masalia" ya Wasomali na watu kutoka Mombasa wengi tu.Hivi ndivyo navyojua chanzo cha dini hiyo kuingia eneo la Machame.
 
Hata nkuu ndoo njia nne pale wamejazana na wengi ni Kutoka ukoo wa Nkya..
Ni wachinjaji wazuri .
Hilo swala la uchinjaji nilikuwepo wakati huo diwani akiwa Rajabu Nkya ...Anaishi waramu pale... Wakristo walipoamua kununua nyama Kwa wakristo wenzao wakaanza vitisho...Nakumbuka kuna mzee walimwekea risasi na petroleum buchani kwake ila Hilo halikufua Dafu.
Basi hali hii ya wao kutaka kuwa wachinjaji tu na sio watu wengine si jambo jipya,ni jambo la kihistoria.Na kwa aina hiyo,ndio sababu hata wakati imeonekana Wachinjaji katika machinjio ya Boma la Ng'ombe yawe mikononi mwa Wasomali na Wagunya wa Mombasa,akina Nkya(Mzee Rajab) waliamua kusilimu na kuwa Waislam,ili tu ile "haki yao ya kimila" ya wao kuwa Wachinjaji iendeleee.

Hapa ndio unakuja kuanza kuona Uislam wa Mzee Rajabu na ukoo wa akina Nkya.
 
Na huu ndio ukweli,ukweli unaoelezea chanzo cha Uislam kuingia Uchaggani kwa kupitia eneo la Machame.

Wasomali unawaona hapo Nkuu Sinde ni kwa sababu ya Uchinjaji,walikuwa wachinjaji katika mnada wa eneo ambalo lilifahamika kama "Boma la Ng'ombe",sababu palikuwa na boma kubwa ambalo Wamaasai toka uwanda wa eneo la sasa la Manyara(Mererani) na eneo la Ruvu ya Same walileta mifugo yao hapo na kuifungia wakisubiri mnada.

Na siku ya Mnada waliochinja walikuwa Wasomali tu,lakini kwa sababu ukoo wa akina Rajabu na wao kwa asili walikuwa ni wachinjaji,hawakutaka kuipoteza hiyo "haki yao ya kimila",na kwa sababu baadae kigezo ilikuwa LAZIMA uwe muislam,Mzee Rajabu hakuona tabu hiyo,na katika hili palizuka mgogoro wa kimila,hapo ndipo chimbuko sasa la Uislam kuingia eneo hilo na kufanya kuwa na Wachagga waislam ambao koo zao zimechanganyika na Wagunya wa Mombasa na Wasomali.

Mpaka leo,eneo hilo lina "masalia" ya Wasomali na watu kutoka Mombasa wengi tu.Hivi ndivyo navyojua chanzo cha dini hiyo kuingia eneo la Machame.
Mkuu Mohamed Said sijui kama ana kubali huu ukweli
 
Mkuu Mohamed Said sijui kama ana kubali huu ukweli
"Wakibosho wakimfahamu kama Rajabu Ibrahim Kirama kwa majina yake ya udogoni ya Kirama Muro lakini sasa amewatokea akiwa Rajabu Ibrahim Kirama na yale mavazi waliyozoea kumuona akivaa udogoni hakuwanayo tena."

Mzee kwenye andiko lake,kuna sehemu kaandika hivi,hii ni kusema kuwa,Mzee Rajabu (Kirama Muro) aliingia katika dini hii akiwa mtu mzima.Na chanzo ni hicho,kuwa na "haki" ya kuendelea kuchinja.

Na mgogoro kati yake na Mangi ulikuwa ni wa "LAZIMA" sababu Mzee Kirama Muro alikulia kwenye familia ya Mangi,kusilimu na kuonekana yu mtofauti kwa dini na mavazi,ulikuwa ni "mgogoro" wa lazima wa kimila.

Ndio kusema,hata sasa,Uislam katika uchagga upo kwenye koo za Mzee Rajabu eneo la Machame
 
Mkuu Mohamed Said sijui kama ana kubali huu ukweli
Mzee Mohammed Said ni mtu wa kusoma sana.Namfuatiliaga sana fb.Ila jambo moja analolifanya linalonikwaza ni kuendelea kuaminisha wasomaji wake kuwa Waislam wanaonewa.Napenda sana makala zake, maana ni za kitafiti kweli kweli, ila yeye binafsi nadhani anashindwa kuvumilia kutokututia matatani na ndugu zetu Waislam.Ni kweli waislam walionewa na Wakoloni au labda serikali.Lakini kuendelea kutukumbusha mambo hayo kizazi cha sasa ni sawa na kuwaambia ndugu zetu Waislam wasitupende na wao ama walipe kisasi.
 
Asanteni sana kwa hii historia. Maana nlikuwa najiuliza uislam umefikaje Kilimanjaro na hasa uchagani. Maana kihistoria biashara za waarabu na utumwa hazikufika sana uchagani na umasaini. Kwa kuendelea kujifunza, uislam ulifikaje upareni?
 
Hata nkuu ndoo njia nne pale wamejazana na wengi ni Kutoka ukoo wa Nkya..
Ni wachinjaji wazuri .
Hilo swala la uchinjaji nilikuwepo wakati huo diwani akiwa Rajabu Nkya ...Anaishi waramu pale... Wakristo walipoamua kununua nyama Kwa wakristo wenzao wakaanza vitisho...Nakumbuka kuna mzee walimwekea risasi na petroleum buchani kwake ila Hilo halikufua Dafu.
Hivi pale njia nne ni Nkuu ndoo ee? Mi najuaga Nkuu ndo inaanzia pale kwa kina Muro na marehemu Charles Kileo (Balozi)..

Basi nadhani pale njia nne ndio mpaka wa Nkuu Ndoo na Nkuu Sinde
 
Hata mimi ndivyo navyofahamu.Ukoo huu ulikuwa ni ukoo wa wachinjaji miaka na miaka,toka enzi na enzi.

Ilipoanza kazi ya uchinjaji "rasmi" kwa minajili ya dini,kwa maana ya wachijaji LAZIMA wawe Waislam,kazi hii ilichukuliwa na Wasomali na Wagunya kutoka Mombasa,Mzee Rajabu hakutaka kuipoteza kazi hii,pale alipoamabiwa ili aendelee na kazi yake ni LAZIMA asilimu,na wao ukoo wa Nkya walijipa "haki miliki" ya kuchinja,akaamua kuwa Muislam,na waliomsilimisha ni hao Wagunya wa Mombasa.
Hapo ndio Uislam ukaingia eneo la Uchaga na hasa Machame,ili kuendelea na kazi yao ya uchinjaji,ukoo ukawa wa Kiislam..Imeenda hivyo mpaka kesho,wengi ni wauza nyama na wachinjaji na wauza mirungi toka Mombasa.

Hili ndio shina la ukoo wa akina Said Mwema
Barafu,
Liepzig Mission waliingia Kilimanjaro 1893 na kwa miaka yote kuchinja hakukupata kuwa suala.

Mzee Rajabu hakuingia kwa ajili ya kuwa na ruhusa ya kuchinja kwani jamii iliyomzunguka yote ilikuwa inajichinjia wanyama wake bila ya kufata sheria ya Kiislam kwa sababu hapakuwa na Waislam.

Rajab Kirama kaingia Uislam mwaka wa 1930 na Machame hawakuwapo Waislam wa kutosha kuwa na sauti ya kuhitaji uchinjaji kwa mujibu wa sharia.

Uislam Machame ulipata nguvu kuanzia miaka ya mwishoni 1940 baada ya Sheikh Abdallah Minhaj kufika na kuanza kusomesha Uislam.
 
Asanteni sana kwa hii historia. Maana nlikuwa najiuliza uislam umefikaje Kilimanjaro na hasa uchagani. Maana kihistoria biashara za waarabu na utumwa hazikufika sana uchagani na umasaini. Kwa kuendelea kujifunza, uislam ulifikaje upareni?
Helios,
Uislam ulipata nguvu Kilimanjaro na Upare pale mwaka wa 1943 Rajabu Ibrahim Kirama alipokwenda Dar es Salaam na kumchukua Sheikh Hassan bin Ameir na kujanae Machame.

Baada ya safari hii Sheikh Hassan bin Ameir alileta walimu wanne kuja kufundisha dini Machame na Upare.

Walimu hawa walikuwa Sheikh Salehe Mwamba, Shariff Alawi, Sheikh Mahmud Mshinda na Sheikh Abdallah Minhaj.

Hiki ni kisa kirefu sana kinahitaji muda kukieleza chote kwa ukamilifu.
Vijana hawa walimu wamecha athari kubwa sana katika historia ya Uislam.

Picha hiyo hapo chini ni Sheikh Abdallah Minhaj na hakurudi tena kwao Zanzibar na Ngazija.

Kaburi lake lipo hapo Moshi.

1611087099301.png
 
Wakati hizo picha zinapigwa miaka ya 1930 hatukujua kwamba mchaga Ben Saanane atatekwa na kutoweka miaka 85 baadae.
 
Licking...
Unasubiri majibu gani kutoka kwangu?

Hii ndiyo faida ya kuandika kwani kunatoa nafasi ya watu kuchangia kilichoandikwa.

Katika ukoo wa Mzee Rajabu aliyekuwa mfanya biashara wa nyama na mchinjaji ng'ombe ni mwanae Salim.

Mzee Rajabu yeye alikuwa mkulima wa kahawa.

Ukoo wa Nkya Wachagga kabla ya kuingia Ukristo ulichukuliwa kama ukoo wa watu waliobarikiwa kwa hiyo Mangi alipotaka kuwatia wanae suna (kuwatahiri) atawatia na watoto kutoka ukoo wa Nkya katika kundi lile la vijana ili kuepusha mikosi.

Halikadhalika Mangi alipokuwa anachinja mnyama mchinjaji atakuwa kutoka ukoo wa Nkya.

Majemadari wa Vita wote wa Mangi wa Machame kutoka ukoo wa Shangali walikuwa kutoka ukoo wa Nkya kuanzia Nshau hadi Muro Mboyo baba yake Mzee Rajabu.

Hii ndiyo historia niliyoikuta katika utafiti wangu.
Asante sana Mzee Said kwa hii Historia nzuri. Barikiwa sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom