Picha kutoka gazeti la Mambo Leo la mwaka wa 1934. Watazame Mangi waliopambana na Rajabu Kirama - Mangi Ngilisho na Shangali

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,409
2,000
PICHA KUTOKA GAZETI LA MAMBO LEO LA MWAKA WA 1934 WATAZAME MANGI WALIOPAMBANA NA RAJABU KIRAMA - MANGI NGILISHO NA SHANGALI

Katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama Mangi wa Kibosho Ngilisho Sina alimwandikia barua kali Mzee Rajabu kuhusu msikiti aliokuwa anataka kujenga Kibosho.

Nakuwekea hapo chini maelezo ya kisa hicho kama nilivyokiandika katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama na picha ya Mangi Ngilisho (wa pili kutoka kulia safu ya mbele) akiwa na machifu wengine wa Uchaggani:

''Juu ya haya yote msikiti ulijengwa na kwa mara ya kwanza Machame Nkuu pakawa panaadhiniwa mara tano kila siku kuwaita Waislamu kwenye sala mara tano kwa kutwa.

Halikadhalika kengele ikawa inapigwa kanisani ambayo kwa takriban miaka mia moja ilikuwa inasikika kote kijijini hapo.

Pale Machame kwa Mangi kutoa amri ya kuvunjwa kwa misikiti lilikuwa jambo la kawaida na kadri Wachagga walivyozidi kusilimu na kuwa Waislamu, matukio ya kuvunjwa misikiti iliyokuwa inajengwa ikawa kitu cha kawaida.

Kufikia mwaka wa 1945 Kibosho kulikuwa na jumla ya Waislamu 500 na hawa Waislamu walihitaji kuwa na msikiti kwa ajili ya sala na pia kama sehemu ya madrasa kutoa elimu kwa watoto wao. Ikasadifu pia hapo Kibosho kuwa Waislamu walikuwa katika kipindi hicho wakivunja mawe kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Waislamu hawa walijenga msikiti lakini Mangi Ngilisho Sina wa Kibosho alitoa amri msikiti uvunjwe.

Mzee Rajabu akiwa ameongozana na wazee 18 kutoka Kibosho walikwenda kuonana na Mangi Ngilisho Sina kwa ajili ya shauri la kiwanja cha msikiti maombi ambayo yalipelekwa siku nyingi lakini majibu hayakutoka.

Mzee Rajabu ikawa sasa anarudi nyuma kwenye historia yake na ujenzi wa msikiti wake wa Machame mwaka wa 1930 ulioibua uhasama mkubwa baina yake na Mangi Abdieli Shangali (safu ya mbele wa tatu kutoka kushoto).

Kama alivyokuwa anamfahamu Chifu Abdieli Shangali ni hivyo hivyo ndivyo walivyokuwa anafahamiana na Mangi Ngilisho Sina.

Mzee Rajabu alikuwa kalelewa Kibosho ndani ya nyumba ya Mangi Sina pamoja na mtoto wa Mangi Sina, Ngilisho Sina.

Hii ilikuwa baada ya baba yake Muro Mboyo kwenda uhamishoni Old Moshi kama ilivyokwishaelezwa huko nyuma na mama yake kurudi kwao Kibosho kwa wazazi wake na kwa Mangi Sina.

Rajabu Ibrahim Kirama na Mangi Ngilisho Sina walikuwa wamelelewa ndani ya nyumba moja.

Wakibosho wakimfahamu kama Rajabu Ibrahim Kirama kwa majina yake ya udogoni ya Kirama Muro lakini sasa amewatokea akiwa Rajabu Ibrahim Kirama na yale mavazi waliyozoea kumuona akivaa udogoni hakuwanayo tena.

Amewatokea akiwa kavaa kama Mswahili kavaa kanzu na kapiga kilemba.

Lakini ingawa alisharudi kwao Machame kwa baba yake miaka mingi lakini ile lafudhi ya Kikibosho haikumtoka.

Mzee Rajabu aliweza kuyatupilia mbali yale mavazi yake ya zamani ya kawaida yaliyokuwa yanavaliwa na takriban kila mtu lakini lafudhi ya Kikibosho ilikuwa imemganda na kama humjui utasema huyu ni Mkibosho.

Mangi Ngilisho alikuwa ameshalitolea uamuzi mapema suala la kujenga msikiti.

Katika barua kali iliyoandikwa kwa hati ya mkono na kuambatanishwa na karatasi iliyokuwa na majina hayo 18 yameandikwa maneno haya yakieleza msimamo wa Mangi Ngilisho Sina:

“Waissiramu walio Kibosho ni 500 waliyokwenda kwa mangi kutaka mahali pakujenga mussikiti walipomuuliza Mangi wao amesema hamwezi kupata hata mkifika kwa District Officer [Afisa Mtendaji wa Wilaya] Moshi na Arusha kwa pissii hamuwezi kupata maana mimi Mangi Ngilisho c/s Sina nimeweka sahihi mbele ya Bwana pissii Arusha wakati nilipovunja mussikiti ule wa kwanza ndipo nilipoweka sahihi kama katika nchi yangu ya Kibosho sitakubali kujenga mussikiti haya ndiyo majibu Mangi aliyowajibu wazee waliopelekwa na jamiaya waissiram wa Kibosho wazee waliyokwenda majina yao ni haya...”
(Taarifa haina jina la mwandishi iliyoandikwa kwa hati ya mkono katika karatasi mbili moja ni taarifa na karatasi ya pili ina majina ya wazee 18 tarehe 1 Novemba, 1945: Mhamed bin Makwini, Sofiani bin Ngelechi, Ali bin Nangeda, Hassani bin Kisamu, Salim bin Choloi, Abubakali bin Tira, Abudian bin Ngelechi, Hamissi bin Mchomba, Salim bin Urawe, Rashidi bin Maimbi, Ali bin Mzuli, Rashidi bin Ngowiya, Salehe bin Mangale, Omali bin Mkenya, Ali bin Tuta, Hassana nin Mangale, Asumani bin Mbonika, Ramazani bin Mota. Angalia barua ya tarehe 5 Novemba, 1945 kutoka kwa Rajabu Kirama, Jamiatu Islam, Machame kwa Sulemani Rajabu inayoeleza kuwa alikwenda na wenzake kwa Mangi tarehe 27 Oktoba, 1945 kusadikisha kuwa Kibosho kuna Waislamu 500 ambao hawana msikiti kwa hiyo apatiwe kiwanja cha kujenga msikiti). Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama).

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,409
2,000
Hawa Wazee wana nyonga tai na suti miaka huyo?
Ndugu zangu wamatumbi wanavaa kaniki tuu.
Kyalow,
Mavazi yanakwenda na utamaduni wa jamii husika.

Kuvaa kaniki kwa akina mama au msuli kwa wanaume si udhalili.

Angalia picha hiyo hapo chini ya babu zangu wamepiga mwaka wa 1933 siku ya ufunguzi wa ofisi ya African Association, New Street Dar es Salaam:

1610565471607.png
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,705
2,000
Mzee Said Wasalaam

Ukifuatilia kwa undani,utagundua kuwa Mzee Rajabu hakuwa Muislam tu kwa hiyari yake,aliamua kusilimu sababu ya ushawishi wa Wasomali waliokuwa wanachinja ng'ombe pale Boma La Ng'ombe,ambao ni mnada na machinjio ya ng'ombe toka enzi za Ukoloni.

Mzee Rajabu alikuwa mmoja wa wachinjaji wazuri sana,lakini akawa anapata vikwazo sbb mkoloni alitaka wachinjaji wawe waislam ili kutokukwaza wengine,na wachinjaji wengi walikuwa wasomali na Wagunya kutoka Mombasa.

Mzee Rajabu akaamua kusilimu ili asipoteze kazi yake ya kuchinja,na hapo akaanza kueneza uislam...na hawa akina Rajabu ni ukoo wa Nkya,ambao kwa kichaga ina maana ya mkia,na waliitwa hivyo sbb wakati wa kuchinja mwenye ng'ombe alichukua kila kitu akaacha mkia.

Ndio maana mpaka leo,ukoo wa akina Rajabu ndio wauza nyama maarufu,wenye connection na mirungi na ndio pekee wachaga wanaoenda Mombassa kama "Their Second home".Nikipata wasaa ntaeleza kwa kirefu jambo hili.

Ukifika Kimashuku(Lambo) mahali ambapo kulikuwa na swamp ya kunyweshea ng'ombe kabla ya kwenda Boma la Ng'ombe kutiwa kisu,utapata mengi.
 
Kyalow

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,360
2,000
Mzee Said Wasalaam

Ukifuatilia kwa undani,utagundua kuwa Mzee Rajabu hakuwa Muislam tu kwa hiyari yaje,aliamua kusilimu sababu ya ushawishi wa Wasomali waliokuwa wanachinja ng'ombe pale Boma La Ng'ombe,ambao ni mnada na machinjio ya ng'ombe toka enzi za Ukoloni.

Mzee Rajabu alikuwa mmoja wa wachinjaji wazuri sana,lakini akawa anapata vikwazo sbb mkoloni alitaka wachinjaji wawe waislam ili kutokukwaza wengine,na wachinjaji wengi walikuwa wasomali na Wagunya kutoka Mombasa.

Mzee Rajabu akaamua kusilimu ili asipoteze kazi yake ya kuchinja,na hapo akaanza kueneza uislam...na hawa akina Rajabu ni ukoo wa Nkya,ambao kwa kichaga ina maana ya mkia,na waliitwa hivyo sbb wakati wa kuchinja mwenye ng'ombe alichukua kila kitu akaacha mkia.

Ndio maana mpaka leo,ukoo wa akina Rajabu ndio wauza nyama maarufu,wenye connection na mirungi na ndio pekee wachaga wanaoenda Mombassa kama "Their Second home".Nikipata wasaa ntaeleza kwa kirefu jambo hili.

Ukifika Kimashuku(Lambo) mabali ambapo kulikuwa na swamp ya kunyweshea ng'ombe kabla ya kwenda Boma la Ng'ombe kutiwa kisu,utapata mengi
Asante sana mkuu kwa historia hii
Mzee Said hatuambii chanzo cha Rajabu kuwa muislamu
Mimi nilimwambia pia mchango wa wasudani na wazigua waliokua vibarua katika mashamba ya mkoloni hapo Machame ila akapita kimya.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,622
2,000
PICHA KUTOKA GAZETI LA MAMBO LEO LA MWAKA WA 1934 WATAZAME MANGI WALIOPAMBANA NA RAJABU KIRAMA - MANGI NGILISHO NA SHANGALI

Katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama Mangi wa Kibosho Ngilisho Sina alimwandikia barua kali Mzee Rajabu kuhusu msikiti aliokuwa anataka kujenga Kibosho.

Nakuwekea hapo chini maelezo ya kisa hicho kama nilivyokiandika katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama na picha ya Mangi Ngilisho (wa pili kutoka kulia safu ya mbele) akiwa na machifu wengine wa Uchaggani:

''Juu ya haya yote msikiti ulijengwa na kwa mara ya kwanza Machame Nkuu pakawa panaadhiniwa mara tano kila siku kuwaita Waislamu kwenye sala mara tano kwa kutwa.

Halikadhalika kengele ikawa inapigwa kanisani ambayo kwa takriban miaka mia moja ilikuwa inasikika kote kijijini hapo.

Pale Machame kwa Mangi kutoa amri ya kuvunjwa kwa misikiti lilikuwa jambo la kawaida na kadri Wachagga walivyozidi kusilimu na kuwa Waislamu, matukio ya kuvunjwa misikiti iliyokuwa inajengwa ikawa kitu cha kawaida.

Kufikia mwaka wa 1945 Kibosho kulikuwa na jumla ya Waislamu 500 na hawa Waislamu walihitaji kuwa na msikiti kwa ajili ya sala na pia kama sehemu ya madrasa kutoa elimu kwa watoto wao. Ikasadifu pia hapo Kibosho kuwa Waislamu walikuwa katika kipindi hicho wakivunja mawe kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Waislamu hawa walijenga msikiti lakini Mangi Ngilisho Sina wa Kibosho alitoa amri msikiti uvunjwe.

Mzee Rajabu akiwa ameongozana na wazee 18 kutoka Kibosho walikwenda kuonana na Mangi Ngilisho Sina kwa ajili ya shauri la kiwanja cha msikiti maombi ambayo yalipelekwa siku nyingi lakini majibu hayakutoka.

Mzee Rajabu ikawa sasa anarudi nyuma kwenye historia yake na ujenzi wa msikiti wake wa Machame mwaka wa 1930 ulioibua uhasama mkubwa baina yake na Mangi Abdieli Shangali (safu ya mbele wa tatu kutoka kushoto).

Kama alivyokuwa anamfahamu Chifu Abdieli Shangali ni hivyo hivyo ndivyo walivyokuwa anafahamiana na Mangi Ngilisho Sina.

Mzee Rajabu alikuwa kalelewa Kibosho ndani ya nyumba ya Mangi Sina pamoja na mtoto wa Mangi Sina, Ngilisho Sina.

Hii ilikuwa baada ya baba yake Muro Mboyo kwenda uhamishoni Old Moshi kama ilivyokwishaelezwa huko nyuma na mama yake kurudi kwao Kibosho kwa wazazi wake na kwa Mangi Sina.

Rajabu Ibrahim Kirama na Mangi Ngilisho Sina walikuwa wamelelewa ndani ya nyumba moja.

Wakibosho wakimfahamu kama Rajabu Ibrahim Kirama kwa majina yake ya udogoni ya Kirama Muro lakini sasa amewatokea akiwa Rajabu Ibrahim Kirama na yale mavazi waliyozoea kumuona akivaa udogoni hakuwanayo tena.

Amewatokea akiwa kavaa kama Mswahili kavaa kanzu na kapiga kilemba.

Lakini ingawa alisharudi kwao Machame kwa baba yake miaka mingi lakini ile lafudhi ya Kikibosho haikumtoka.

Mzee Rajabu aliweza kuyatupilia mbali yale mavazi yake ya zamani ya kawaida yaliyokuwa yanavaliwa na takriban kila mtu lakini lafudhi ya Kikibosho ilikuwa imemganda na kama humjui utasema huyu ni Mkibosho.

Mangi Ngilisho alikuwa ameshalitolea uamuzi mapema suala la kujenga msikiti.

Katika barua kali iliyoandikwa kwa hati ya mkono na kuambatanishwa na karatasi iliyokuwa na majina hayo 18 yameandikwa maneno haya yakieleza msimamo wa Mangi Ngilisho Sina:

“Waissiramu walio Kibosho ni 500 waliyokwenda kwa mangi kutaka mahali pakujenga mussikiti walipomuuliza Mangi wao amesema hamwezi kupata hata mkifika kwa District Officer [Afisa Mtendaji wa Wilaya] Moshi na Arusha kwa pissii hamuwezi kupata maana mimi Mangi Ngilisho c/s Sina nimeweka sahihi mbele ya Bwana pissii Arusha wakati nilipovunja mussikiti ule wa kwanza ndipo nilipoweka sahihi kama katika nchi yangu ya Kibosho sitakubali kujenga mussikiti haya ndiyo majibu Mangi aliyowajibu wazee waliopelekwa na jamiaya waissiram wa Kibosho wazee waliyokwenda majina yao ni haya...”
(Taarifa haina jina la mwandishi iliyoandikwa kwa hati ya mkono katika karatasi mbili moja ni taarifa na karatasi ya pili ina majina ya wazee 18 tarehe 1 Novemba, 1945: Mhamed bin Makwini, Sofiani bin Ngelechi, Ali bin Nangeda, Hassani bin Kisamu, Salim bin Choloi, Abubakali bin Tira, Abudian bin Ngelechi, Hamissi bin Mchomba, Salim bin Urawe, Rashidi bin Maimbi, Ali bin Mzuli, Rashidi bin Ngowiya, Salehe bin Mangale, Omali bin Mkenya, Ali bin Tuta, Hassana nin Mangale, Asumani bin Mbonika, Ramazani bin Mota. Angalia barua ya tarehe 5 Novemba, 1945 kutoka kwa Rajabu Kirama, Jamiatu Islam, Machame kwa Sulemani Rajabu inayoeleza kuwa alikwenda na wenzake kwa Mangi tarehe 27 Oktoba, 1945 kusadikisha kuwa Kibosho kuna Waislamu 500 ambao hawana msikiti kwa hiyo apatiwe kiwanja cha kujenga msikiti). Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama).

Kwanini Marealle ndiye alitokea kuwa maarufu sana huko Kilimanjaro kuliko watemi wenzake?
 
Licking Wounds

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
2,383
2,000
Mzee Said Wasalaam

Ukifuatilia kwa undani,utagundua kuwa Mzee Rajabu hakuwa Muislam tu kwa hiyari yaje,aliamua kusilimu sababu ya ushawishi wa Wasomali waliokuwa wanachinja ng'ombe pale Boma La Ng'ombe,ambao ni mnada na machinjio ya ng'ombe toka enzi za Ukoloni.

Mzee Rajabu alikuwa mmoja wa wachinjaji wazuri sana,lakini akawa anapata vikwazo sbb mkoloni alitaka wachinjaji wawe waislam ili kutokukwaza wengine,na wachinjaji wengi walikuwa wasomali na Wagunya kutoka Mombasa.

Mzee Rajabu akaamua kusilimu ili asipoteze kazi yake ya kuchinja,na hapo akaanza kueneza uislam...na hawa akina Rajabu ni ukoo wa Nkya,ambao kwa kichaga ina maana ya mkia,na waliitwa hivyo sbb wakati wa kuchinja mwenye ng'ombe alichukua kila kitu akaacha mkia.

Ndio maana mpaka leo,ukoo wa akina Rajabu ndio wauza nyama maarufu,wenye connection na mirungi na ndio pekee wachaga wanaoenda Mombassa kama "Their Second home".Nikipata wasaa ntaeleza kwa kirefu jambo hili.

Ukifika Kimashuku(Lambo) mabali ambapo kulikuwa na swamp ya kunyweshea ng'ombe kabla ya kwenda Boma la Ng'ombe kutiwa kisu,utapata mengi
Mkuu asante kwa kufunua haya! Ngoja nisubiri majibu ya Mohamed Said
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,409
2,000
Mkuu asante kwa kufunua haya! Ngoja nisubiri majibu ya Mohamed Said
Licking...
Unasubiri majibu gani kutoka kwangu?

Hii ndiyo faida ya kuandika kwani kunatoa nafasi ya watu kuchangia kilichoandikwa.

Katika ukoo wa Mzee Rajabu aliyekuwa mfanya biashara wa nyama na mchinjaji ng'ombe ni mwanae Salim.

Mzee Rajabu yeye alikuwa mkulima wa kahawa.

Ukoo wa Nkya Wachagga kabla ya kuingia Ukristo ulichukuliwa kama ukoo wa watu waliobarikiwa kwa hiyo Mangi alipotaka kuwatia wanae suna (kuwatahiri) atawatia na watoto kutoka ukoo wa Nkya katika kundi lile la vijana ili kuepusha mikosi.

Halikadhalika Mangi alipokuwa anachinja mnyama mchinjaji atakuwa kutoka ukoo wa Nkya.

Majemadari wa Vita wote wa Mangi wa Machame kutoka ukoo wa Shangali walikuwa kutoka ukoo wa Nkya kuanzia Nshau hadi Muro Mboyo baba yake Mzee Rajabu.

Hii ndiyo historia niliyoikuta katika utafiti wangu.
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,409
2,000
Asante sana mkuu kwa historia hii
Mzee Said hatuambii chanzo cha Rajabu kuwa muislamu
Mimi nilimwambia pia mchango wa wasudani na wazigua walowezi hapo Machame ila akapita kimya.
Kyalow,
Niwie radhi kama sikukufahamisha sababu ya Mzee Rajabu kuwa Muislam.

Mzee Rajabu alimsikia Shariff Muhsin akimzungumza Allah na maneno yale ndiyo yaliyomuathiri akasilimu.

Mchango wa Wazigua na Wasudani siujui ndiyo sababu nimekuwa kimya.

Nimejaribu kufanya utafiti kuhusu ulowezi kwa ujumla Uchaggani nilichofahamishwa ni kuwa hapajapata kuwa na ulowezi wa kabila lolote katika ardhi ya Wachagga ukitoa ule wa Wamishionari kutoka Ulaya ambao walikaribishwa na Mangi.

Ningependa kutoka kwako kujua zaidi historia hii ya Waafrika walowezi Wanubi na Wazigua Uchaggani.
 
MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
3,712
2,000
Waislamu wakiandika jambo lao huwa halina kichwa wala miguu sijui ni kwakuwa wanaanzia kushoto kwenda kulia?
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,409
2,000
Waislamu wakiandika jambo lao huwa halina kichwa wala miguu sijui ni kwakuwa wanaanzia kushoto kwenda kulia?
Mtochoro,

Haifai kutoa maneno kama haya ya kifedhuli.

Hatari yake utawakaribisha katika mjadala huu watu hodari wa matusi kukushinda.

Mjadala wetu wa heshima na staha utaharibika.

Ikiwa unaona naandika sieleweki wajibu wako ni kuniongoza ukanielekeza.
 
Giningi01

Member
Nov 19, 2020
17
45
Ni vema angefanya declaration, machifu wengi sio lazima wachukue majina ya baba zao, walikuwa wanachukua hata babu zao hata wa nne au vyovyote atakavyoamua.
 
FisadiKuu

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
6,830
2,000
Mzee Said Wasalaam

Ukifuatilia kwa undani,utagundua kuwa Mzee Rajabu hakuwa Muislam tu kwa hiyari yaje,aliamua kusilimu sababu ya ushawishi wa Wasomali waliokuwa wanachinja ng'ombe pale Boma La Ng'ombe,ambao ni mnada na machinjio ya ng'ombe toka enzi za Ukoloni.

Mzee Rajabu alikuwa mmoja wa wachinjaji wazuri sana,lakini akawa anapata vikwazo sbb mkoloni alitaka wachinjaji wawe waislam ili kutokukwaza wengine,na wachinjaji wengi walikuwa wasomali na Wagunya kutoka Mombasa.

Mzee Rajabu akaamua kusilimu ili asipoteze kazi yake ya kuchinja,na hapo akaanza kueneza uislam...na hawa akina Rajabu ni ukoo wa Nkya,ambao kwa kichaga ina maana ya mkia,na waliitwa hivyo sbb wakati wa kuchinja mwenye ng'ombe alichukua kila kitu akaacha mkia.

Ndio maana mpaka leo,ukoo wa akina Rajabu ndio wauza nyama maarufu,wenye connection na mirungi na ndio pekee wachaga wanaoenda Mombassa kama "Their Second home".Nikipata wasaa ntaeleza kwa kirefu jambo hili.

Ukifika Kimashuku(Lambo) mabali ambapo kulikuwa na swamp ya kunyweshea ng'ombe kabla ya kwenda Boma la Ng'ombe kutiwa kisu,utapata mengi
Na kwako ni pale Nkuu Sinde njia nne. Mpaka leo ni wauzaji wakubwa wa nyama.

Kuna mwaka ule waislam wanalilia kuchinja wachinje wao tu, kule Machame hawa akina Rajabu wakaivalia njuga, eti wachinje wao na kuuza nyama wauze wao wakati waislam ni 0.001 ya population yote Machame. Wakristo wala hawakutaka fujo, wakawaambia sisi tuacheni tutanunua kwenye bucha za wakristo wenzetu nyama hizihizi mnazoziita najisi na nyie wauzieni waislam wenzenu. Mbona wenyewe waliomba poo na kukubali yaishe.

Waislam kule uchagani ni tone tu lakini tunaishi nao vizuri bila matatizo yoyote, ila kama kwenye ile jamii waislam wangekuwa ni wengi kuliko wakristo sijui hata hawa wakristo wangeishije.
 
Kyalow

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,360
2,000
Kyalow,
Niwie radhi kama sikukufahamisha sababu ya Mzee Rajabu kuwa Muislam.

Mzee Rajabu alimsikia Shariff Muhsin akimzungumza Allah na maneno yale ndiyo yaliyomuathiri akasilimu.

Mchango wa Wazigua na Wasudani siujui ndiyo sababu nimekuwa kimya.

Nimejaribu kufanya utafiti kuhusu ulowezi kwa ujumla Uchaggani nilichofahamishwa ni kuwa hapajapata kuwa na ulowezi wa kabila lolote katika ardhi ya Wachagga ukitoa ule wa Wamishionari kutoka Ulaya ambao walikaribishwa na Mangi.

Ningependa kutoka kwako kujua zaidi historia hii ya Waafrika walowezi Wanubi na Wazigua Uchaggani.
Wanubi walikua wanyakazi kwenye mashamba nilikosea kuandika
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,705
2,000
Na kwako ni pale Nkuu Sinde njia nne.. Mpaka leo ni wauzaji wakubwa wa nyama..

Kuna mwaka ule waislam wanalilia kuchinja wachinje wao tu, kule Machame hawa akina Rajabu wakaivalia njuga, eti wachinje wao na kuuza nyama wauze wao wakati waislam ni 0.001 ya population yote Machame. Wakristo wala hawakutaka fujo, wakawaambia sisi tuacheni tutanunua kwenye bucha za wakristo wenzetu nyama hizihizi mnazoziita najisi na nyie wauzieni waislam wenzenu. Mbona wenyewe waliomba poo na kukubali yaishe..

Waislam kule uchagani ni tone tu lakini tunaishi nao vizuri bila matatizo yoyote, ila kama kwenye ile jamii waislam wangekuwa ni wengi kuliko wakristo sijui hata hawa wakristo wangeishije..
Hata mimi ndivyo navyofahamu.Ukoo huu ulikuwa ni ukoo wa wachinjaji miaka na miaka,toka enzi na enzi.

Ilipoanza kazi ya uchinjaji "rasmi" kwa minajili ya dini,kwa maana ya wachijaji LAZIMA wawe Waislam,kazi hii ilichukuliwa na Wasomali na Wagunya kutoka Mombasa,Mzee Rajabu hakutaka kuipoteza kazi hii,pale alipoamabiwa ili aendelee na kazi yake ni LAZIMA asilimu,na wao ukoo wa Nkya walijipa "haki miliki" ya kuchinja,akaamua kuwa Muislam,na waliomsilimisha ni hao Wagunya wa Mombasa.

Hapo ndio Uislam ukaingia eneo la Uchaga na hasa Machame,ili kuendelea na kazi yao ya uchinjaji,ukoo ukawa wa Kiislam..Imeenda hivyo mpaka kesho,wengi ni wauza nyama na wachinjaji na wauza mirungi toka Mombasa.

Hili ndio shina la ukoo wa akina Said Mwema
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom