PICHA: Kikwete kuzindua Ujenzi wa Nyumba za Kiwanda cha Tangawizi na Mama Kilango

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3]Rais Kikwete kuzindua Ujenzi wa Nyumba za Wahanga wa Maporomoko na Kiwanda cha Tangawizi Mamba Miamba leo[/h]






Rais Jakaya KiweteRais anatarajiwa kuzindua ujenzi wa nyumba Nane za wahanga wa maporomoko ya Ardhi yaliyotokea Novemba 2009 katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro.




Katika Maporomoko hayo watu 24 walipoteza maisha huku Kaya 8 zikikosa mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na maporomoko hayo.




Hiyo ni katika utekelezaji wa Ahadi ya Rais Kikwete yaliyotokea Novemba 2009 kujenga nyumba hizo kwa wahanga hao wakati alipowatembelea kuwafariji.



Rais Pia akiwa Mamba Miamba atapata fursa ya kufungua Kiwanda cha Kusindika Tangawizi cha Ushirika wa Walima Tangawizi Mamba Miamba.




Baada ya kufungua nyumba hizo na Kiwanda, Rais Kikwete atahutubia Mkutano wa hadhara na baadae kuelekea Wilaya ya Mwanga na kuweka jiwe la msingi hosteli ya wasichana shule ya Dkt. Asha-Rose Migiro.



Mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Tangawizi Mamba Miamba, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Omary Kapara akianika Tangawizi iliyokwisha safishwa kabla ya kuanza uzalishaj.



Mbunge wa Same Mashariki, Mh Anne Kilango Malecela akiwa katika maandalizi ya mwisho mho Kimejengwa kwa juhudi zake wisho kabla ya kufunguliwa Kiwanda cha Kusindika Tangawizi ambacho kimejengwa kwa jitihada zake kama Mbunge.
 
Kiwanda kinadaiwa kwa kimegharimu makadirio ya uanzishwaji wa kiwanda hicho unakaribia Sh bilioni 1.5,

Kiwanda kiko kama vile vipanda
 
Kiwanda kinadaiwa kwa kimegharimu makadirio ya uanzishwaji wa kiwanda hicho unakaribia Sh bilioni 1.5,

Kiwanda kiko kama vile vipanda

dah .... yaani hichi ndicho kiwanda huyu mama anapiga majigambo nacho .... yangu macho
 
Kiwanda kinadaiwa kwa kimegharimu makadirio ya uanzishwaji wa kiwanda hicho unakaribia Sh bilioni 1.5,

Kiwanda kiko kama vile vipanda

Hiyo nyumba hapo sio kiwanda bali ni sehemu ya kusindika hizo tangawizi yaani umaweza kuita ni factory,na sio kweli inaweza kuwa na garama ya tzs1.2 bil,labda ni tzs70m tu
 
Kweli huyu ndio raisi wa wadanganyika ahadi kaitoa 2009 nyumba zenyewe matofali ya kuchoma mpaka leo hazijakamilika bado anaenda kuzindua.Huo uzinduzi si ange'efanya mbunge hizo gharama za msafara wa raisi utumike kuzimalizia
 
Jamani kiwanda kiko wapi? Hiki ni kiwanda? Kweli hii nchi tunaliwa kama membe anayeliwa na siafu. Something is not right here. Yaani hili ni shine la kusaga tangawizi na si kiwanda. Hivi vibanda hapa ndizo nyumba za kufunguliwa na raisi? Watanzania tuache utani. Tufanye mambo ya kiukweli kulingana na hii karne na sii hii michezo ya kitoto kama hii.
 
Back
Top Bottom