PICHA; Jinsi Shigella & T. Hiza 'Walivyoiteka' Mtwara!

Hivi Tambwe Hiza bado anapewa platform CCM?. CCM inatakiwa ku-transition sasa, waachane na mipasho waanze kuwa na substance. I mean waanze kuonesha matendo hasa ya kuinua watanzania si mikutano ya kuendelea kuwadanganya watanzania. Mtu kama Hiza kila akionekana kwenye jukwaa basi ni Minus kwa CCM. Kwani kila mtu anaujua jamaa ni mchumia tumbo.

Yaani CCM ya leo inataka mtu uwe na moyo wa paka kujionesha kuwa ni mwanachama wake. Neno CCM kwa sasa limekuwa ni kama 'Taboo' fulani vile.
 
Mkuu ni lugha ya uandishi tu..
nakuwapa moyo CCM angalau nao wafungue thread hii
Uliposema kuiteka nilitegemea umati mkubwa wa watu!
Mbona waliopo apo ni idadi ndogo sana na wengi ni wanachama wao!
So ni lazima watakuwa wamekusanywa toka maeneo mbalimbali na kuletwa eneo la tukio na POSHO JUU!
 
jamani mimi nilikuwepo hapo mtwara hao jamaaa wamekuja na kama kawaida yao walisomba watu kutoka vijiji vya naliendele, ziwani na nanguruwe.. Kwa kuwa watu wa hapo mjini hatoi sapoti ya kutosha na nina ushahidi rafiki zangu wawili ni viongozi wa uvccm na ndio walikuwa waratibu wa usafiri.
 
Haukuwa mkutano wa CCM,Shigella na Hiza walikuwa kwenye mizunguko yao wakakuta wana ukoo wamemaliza kikao chao cha ukoo wao wakaomba kuwasalimia wana ukoo.lkn kusema ulikuwa mkutano wa CCM si kweli {WATU WOTE UNAOWAONA KWENYE PICHA NI UKOO WA CHINTINDILE}
 
Uliposema kuiteka nilitegemea umati mkubwa wa watu!
Mbona waliopo apo ni idadi ndogo sana na wengi ni wanachama wao!
So ni lazima watakuwa wamekusanywa toka maeneo mbalimbali na kuletwa eneo la tukio na POSHO JUU!

Mkuu, kwao kwa sasa huo ni umati mkubwa sana wa malaki ya watu waliohudhuria mkutano.
 
Ccm hoiii.!!..... watu hooiiiiiiiiii*3 Ccm ina wenyewe, na wenyewe ndio sisi wachumia tumbo!!
 
mbonaZomba.Ritz.Rejao.Njiwa na pro CCM wengine hawatii neno hapa au wapo sabasaba kusheherekea sikukuuu.?

kuna taizo la hawa wadau uliowataja kutokuwa hoja ya msingi kama maisha bora kwa wantanzania wote, je yamefikiwa, na yatafikiwa kiuhalisia?pia je wakulima kama wa korosho mbona kuna longolongo nyingi kuhusu mfumo wa soko lao na malipo ya pili ya zao lao?kama ni hivyo je wakulima wa pamba nao vipi?je hizi sera za masoko ya mazao ya kilimo mbona yana kuzungumti?hizo ndo sera za MAGAMBA?hakuna cha shigela, wala cha hiza, hoja ni je ni namna gani MAGAMBA bado wana sera ya ujamaa inayotetea wanyonge?na je hizi kauli na uhalisia wa sasa wa kukumbatia na kutetea matajiri, huoni tayari sera ya kutetea wanyonge imekufa kifo kitakatifu?huyo shigela na hiza njaa zimewauma , wametafuta mradi japo wangange njaa.Mbona arumeru mashariki hawakupewa kama makampeni meneja?imekuwaje leo.tatizo ni nape hajaona kuwa haya mageuzi si upepo tu , bali hali halisi inatakawa watu wenye hekima kuongea uhalisia na si hiza mropokaji na mnafiki, wala shigela kakaa uvccm bila kazi japo akaropoke mtwara, maake hapa dar ,alikatazwa kuwa anakiua chama kwa kauli zake chafu.
 
Kweli wameuteka mji naona umati wa watu jamani...!!!!!!! WAPINZANI KAZI MNAYO...
 
Ninavyowajua watu wa mtwara walivyopauka hapo hakuna wa mtwara hata mmoja.
itakuwa wamepelekwa na mabasi ya Sumri kutoka Dar
 
ninavyowajua watu wa mtwara walivyopauka hapo hakuna wa mtwara hata mmoja.
Itakuwa wamepelekwa na mabasi ya sumri kutoka dar

hapa ndo nahamini pia ninahapa ccm inaelekea mwisho, tutaizika rasmi 2015, hili chama gubegube na wafuasi idadi hii kweli?? Hili lichama litakuwa ndo limeshakufa ila ba rizimoko ndo kabakia
 
mi naona nyomi la vitambaa vya rangi ya njano na kijani, watu bado naendelea kuangalia vizuri km nitaona vyomi!
 
Uliposema kuiteka nilitegemea umati mkubwa wa watu!
Mbona waliopo apo ni idadi ndogo sana na wengi ni wanachama wao!
So ni lazima watakuwa wamekusanywa toka maeneo mbalimbali na kuletwa eneo la tukio na POSHO JUU!


Wee Njowepo, hujui lugha au? Mimi hata kabla sijafungua thread hii nilijua aliyepost mada alikuwa anamanisha kinyume chake.
 
Back
Top Bottom