Kibingu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2022
- 1,077
- 1,452
Mzoga wake ulilaanika. Ndiyo maana ishara mbaya ziliandamana na maziko yake. Watu 7 walifia uwanja wa taifa kwa kukanyagana, baada ya kuhamasishwa bila utaratibu na kusombwa na mabasi kwenda kuaga.Marehemu Magufuli alipendwa sana..period!!
Pia, ishara mbaya ni "legacy" ya miradi yake aliyoanzisha. Yote ina kasoro nyingi zinazoendelea kuwaumiza kichwa waliorithi mikoba yake na kujitutumua kuikamilisha. Wasipofika mahali na kukiri ukweli kuhusu uongo wa niradi hii, wataumia sana mpaka ikamilike. Uongo hausahihishwi kwa uongo mpya.
Magu yampasa aundiwe tume maalum ya kumaliza mambo yake, hasa yale maovu. Serikali iwaombe msamaha na kuwapa fidia wale wote watakaothibitishwa kuumizwa bila haki, ikiwepo waliokaa jela bila haki. Na hili lifanyike haraka, kwa uwazi au kwa kificho.
Baada ya kumalizana na mapungufu haya, ifanyike ibada maalum ya toba, aombewe msamaha, ili mzimu wake usiendelee kulitesa taifa na serikali, mpaka kulazimisha nchi iingie kwenye umwagaji damu usio wa lazima.
Mungu wa msamaha awabariki.