Picha hizi hatuwatendei haki Polisi

Picha hizi hatuwatendei haki Polisi

Mgirik

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
13,258
Reaction score
13,367
Natumai wote mu buheri wa afya.
Napenda kurejea kwenye maada husika.

Katika social network nyingi hivi karibuni kumetokea na hili jambo la kuwarusha askari wetu wakiwa kwenye matukio mbalimbali ambayo hayaendani na maadili ya kazi au maadili ya jamii.

Binafsi kama raia sijapendezewa na mambo wanayoyafanya askari wetu, ni mambo ya kulidhalilisha jeshi letu la polisi na kuidhalilisha sare ya jeshi ambayo ni moja ya nembo ya taifa hili.

Lakin pamoja na udhaifu huo uliopo kwa hawa wenzetu, hatukupaswa kufanya kama hivi tulivyofanya. Kitendo cha kurusha picha hizi kwenye social network ni udhalilishaji mkubwa sana dhidi ya jeshi letu.

Nikweli yawezekana ikawa njia moja wapo ya kuwaamsha kuwa wawe makin katika utendaji wao na hasa wawapo maeneo ya kazi lakini kuna picha zingine zmevuka mpaka.

Tutambue kuwa askari naye ni binadamu kama tulivyo mimi na wewe na yeye ana mapungufu kama binadamu kwahyo ni bora tukatumia busara zaidi kuliko hivi tunavyofanya.

Inafikia hatua unampiga picha akiwa amesinzia bila kuangalia kuwa huyo askari na yeye anachoka kama ambavyo tunachoka mimi na wewe.
Tukumbuke kuwa kabla mimi na wewe hatujaamka kwenda kazini hawa jamaa wanakuwa wapo barabarani mpaka muda tunapokuwa kazini wao bado wanakuwa barabaran kwa ajili ya usalama wetu sasa kwa nini tufikie hatua ya kuwadhalilisha kias hcho?

Ni bora kama umemuona amekaa mahali kasinzia nenda kamwamshe hata yeye atakuona unamaana zaidi kuliko kumrusha kwenye mitandao.

Hebu fikiria angekuwa babayako,mama yako au dadayako au kaka yako ndio anarushwa vile na baadae anafukuzwa kaz kwa kosa dogo ambalo hata ww unauwezo wa kumsaidia.

Tukumbuke kuwa maisha yetu watanzania huwa walio wengi tunategemeana, unapomfukuzisha kazi mwenzako tayari unakuwa umewarudisha nyuma watu wengi sana wanao mtegemea.

Kama wabunge wenyewe pamoja na kuwa na viyoyozi ukumbin lakn bado wanasinzia sasa sembuse askari anayepigwa na jua masaa12?

Na tusisahau mfumo wa nchi yetu yule mwenye kosa dogo ndiyo anateketezwa lakn mwenye kosa kubwa ndiye analindwa.
.......(wanachuja mbu na kumeza ngamia)..........

Kama tunafanya hvyo eti kwa lengo la kuondoa uovu ulio ndani ya jeshi la polis tutakuwa tunakosea kabisa, . Watu wa kudeal nao ni viongoz wa juu , uongozi wa serikali ukiwa imara na thabit hata watendaji wake na wasimamia sheria watakuwa imara,.

Lakn haya tunayoyafanya huku ni kuwaonea tu hawa wenzetu.
Kumbuka hata polis wao sio wote ni wadhalim bali wanashindwa kufanya maamuzi sahihi ya haki kwa sababu ya kusaka tonge, wanaogopa wakienda tofauti na maelekezo watapoteza kazi zao kitu ambacho kitakuwa janga kwa familia zao na wategemezi wao..

....... Napenda niishie hapa.........
 
nakuunga mkono hoja .. Mgirik picha zile watu wamekomaliaaa.ni bora wakomalie na mabaya mengine yanayofanywa na viongozi wetu siyo wanapoona picha za ngono tu ndiyo wafatilieeee
 
Last edited by a moderator:
Mtoa Mada Nakuunga Mkono, Tumeshupalia Sana Haya Mambo Utafikiri Huwa Hatufanyangi?
Imagine Siku Mungu Ageuza USIKU KUWA MCHANA Ndipo Tutakapoona Ya Walimwengu.
 
Mtoa Mada Nakuunga Mkono, Tumeshupalia Sana Haya Mambo Utafikiri Huwa Hatufanyangi?
Imagine Siku Mungu Ageuza USIKU KUWA MCHANA Ndipo Tutakapoona Ya Walimwengu.
kuna vigogo wengi wana masulubaa tena mabaya hawawakomali...mauji ya malbino hawayakomalii .....ila wakishaona picha za mahaba au watu wako chumbanI wamepigwa picha alafu ni vidagaa ahh watakomaliwa mpaka basi
 
nakuunga mkono hoja .. Mgirik picha zile watu wamekomaliaaa.ni bora wakomalie na mabaya mengine yanayofanywa na viongozi wetu siyo wanapoona picha za ngono tu ndiyo wafatilie
Hili in sahihi kabisa, uongozi wa jeshi la polisi ni waonezi, hivi ni sahihi kwa Kamuhanda aliyekuwa RPC Iringa aliyeamuru Daudi Mwangosi auwawe astaafu kwa heshima badala ya fedheha? Bado kuna suala la Chagonja na mke wake na sakata la udalali wa ajira za upolisi, wao wanakomaa na vidagaa tu
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa utetezi wako au hujui kuwa picha nacho ni kithibitisha habari makini? na kwa nini uzembee katika kazi yako? siungi mkono hizo excuse!Askari amewajibishwa na mwajiri wake (jeshi la polisi) na hao wabunge sijui waheshimiwa watawajibishwa na mwajiri wao(mwananchi -kwa kura) mkiwachagua tena huo utakuwa utaahira wenu!
 
Pamoja na kuandika makala ndeeefu mimi wala sikuungi mkono naona kama umekurupuka tu.
Uovu hauwezi kuondoshwa kwa kunyamazia kimya au kuuficha au kuubatiza jina zuri ili kuzuga watu, uovu utaondoshwa kwa kuuanika hadharani kisha kuulani na kuukemea. Na si busara kuacha uovu mwingine uendelee kufanyika eti kwa sababu watu fulani wakifanya maovu hawachukuliwi hatua, ujue imefikia hapo kwa sababu ya watu wenye mtazamo kama wako.

Eti mtu kafukuzwa kazi kwa sababu ya ubadhirifu tunasema kaachishwa kazi kwa maslahi ya umma, mtu anajiuzulu kwa kuwajibika tunasema ni mstaafu! Tuache kutetea maovu, anaetetea maovu nae ni muovu, je ungekuwa ni boss wao ungefanyaje? Au ungewaambia siku nyingine wajifiche waende vichakani zaidi!
 
Mkuu nakuunga mkono, tunalipa kodi askari walipwe mishahara ya kwenda kungonoka porini na kulala kazini wakiamka wale rushwa.
Hawa wanaoingia na vyeti vya kufoji, inabidi tuwatetee, wanapowaonea raia na kuua waandishi wa habari, tuwapandishe vyeo.

Utakuwa CCM bila shaka yoyote.
 
Sio picha tu waungwana kuna shida kubwa mimi nadhani kati ya jeshi la polisi na baadhi/sehemu ya wananchi! !!

Inapotokea ndugu zetu polisi wanapatwa madhila unaweza kuona watu wanafurahi, kiasi kuomba "wangekufa wote" na kama hayo, hii sii ishara nzuri hata kidogo, yawezekana tunaona moshi tu ila moto bado umejificha.

Ni wakati sasa pande zote kujiangalia upya! !
 
.. Mukhabarat elewa siku zote anayepewa adhabu au kuwajibishwa katika nchi hii ni mtu wa chini siyo kigogo au mwenye cheo, ukiona mwenye cheo anawajibishwa ama kufikishwa katika vyombo vya sheria basi juaaa huyo ni kafara au hakulaa na wenzake
turudi kwenye mada hii hao polisi wa barabarani wangesimamishwa tu miezi kadhaa watie akili tatizo media na mitandao ya kijamiii imewashupaliaaaa, kisa picha zao zimekaa kimahabaa camon guys kuna viongozi wangapi na wakubwa wangapi wakuu wa polisina vyama na serikali washafanyaaa upuzi hadi wengine picha zao kupatikana lakini hawajasemwa wala kuwajibishwa..nchi hii siku zote mtu wa chini ndiyo anakandamizwa awe raia awe polisi awe mwanajeshi awe mkulimwa etc
 
Last edited by a moderator:
Sijaona mantiki yako kutetea hili, maadili ya umma hayaruhusu hayo acha waanikwe ili waache ujinga hasa wakiwa kazini
 
Kwani polisi wakiharibu ndio wapotezewe kisa polisi. Ndio maana wamekuwa ombaomba hadi wanatia aibu kabisa. Wakiharibu wapewe haki yao.
 
nmeelewa vizr sana madai yako.
Sio kwamba nawatetea bali najaribu kuasa tu.
Kama ww ni mwanamapinduzi halisi unatakiwa uanze na uongoz kwa kuyaweka wazi maovu yao.

Hiki kitendo cha kuwachongea wanakula denda na wanaosinzia unafikir kitasaidia kumaliza ulaji rushwa?
Kitamaliza udhalim na ukandamizaji? Na je ubadhilifu wa mali za walala hoi na kuwakingia kifua majambaz sugu na kuwatetea wauza unga je kitatokomezwa kwa kuwapiga picha wanaokulana denda na kusinzia?

Kwann tukomalie kukata matawi ya mti wakat shina lenyew lipo linalosababisha hayo matawi yachipue?
 
acha waanikwe mbona hao ma ccm wanawaambia wawapige wananch mabom na kuwamwagia maj ya kuwasha??mbaya zaid wanawadhuru waandish wa habar.
 
Wawajibishwe tu mana hawana mana hata kidogo wanajifanya wajuaji ukiingia kwenye anga zao halafu hawajielewi sheria ingeruhusu ningesisitiza na tusi
 
nchi wanawaogopa kuwaadabisha vigogo wana kimbilia
kuwa nyongaaaa vidagaa tu
ndomana hata walaji rushwa wakubwa wa mabilion hawaguswi wala kupigiwa kelele, lakini wale wanao chukua laki au elfu hamsini ahh wakikamatwa si kuandamwa.....ushauri wangu tu ni hatuo yoyote inayochukuliwa za kisheria kwa viongozi na wafanyakazi
ianze ngazi ya juuuu
 
Back
Top Bottom