kosa moja haliwezi kuhalalishwa kwa kosa lingine. Polisi wana makosa mengi ambayo sio rahisi kupata ushahidi. Wananchi wana usongo nao sana. Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na kudai rushwa, kubambikia watu kesi, kuwapiga watuhumwa wakifika kituo cha polisi hata kabla ya kufika kituoni. Wananchi wanaofanyiwa madhira haya ni wananchi wanyonge wasio na kipato wala cheo. Tena wananchi hawa hufanyiwa na polisi wa vyeo vya chini. Wakubwa hawaguswi hata kidogo. Kwa ufupi ni kuwa katika nchi yetu wanyonge tunaoneana wenyewe kwa wenyewe wakati wakubwa hulindana wao kwa wao, hawatulindi sisi na wala hawajui uchungu tulionao. Mpaka wetu na wao ni mkubwa unaanzia kichwani 'Capture the brain, the trunk will follow by itself' Akili zetu bado hazijajua kama tunaumizana wao kwa wao hivyo kujiongezea shida juu ya shida. Tumetekwa akili kama mtumwa kulindwa na mtumwa mwenzie unyapala ni kilemba cha ukoka tu.
Polisi hawa wana makosa gani wakati sifa mojawapo ya kuajiriwa kazi ya polisi lazima uwe rijali na mapenzi humea popote na wakati wowote, mapenzi nidawa ya msongo wa mawazo, huondoa uchovu. Sio ajabu kukuta boss anapendana na PS (Katibu muhtasi) wake tena pengine ofisini mbele ya picha ya Rais.
Kibaya zaidi hawa polisi walipigwa picha na polisi mwenzao. Wakubwa, licha kupeana mapenzi kazini pia huhongana vyeo na wananchi tunawalipa wapenzi wao mishahara kwa kodi zetu. Si nia yangu kuwa wadogo tusiwe waadilifu la hasha, nataka tuige kusaidiana kama wanavyosaidia wakubwa wetu