KWELI Picha hii ni kutoka Pacific Palisades, Los Angeles, California nchini Marekani

KWELI Picha hii ni kutoka Pacific Palisades, Los Angeles, California nchini Marekani

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kwa kutumia nyenzo za kidigitali zinazokuwezesha kuthibitisha uhalisia wa picha bainisha eneo halisi picha ilipopigwa na nyenzo uliyotumia.


1758787761012.png
 
Tunachokijua
Jamiicheck imejiridhisha kuwa hiyo ni halisi. Kwa kutumia Google Reverse Image Search imebainika tovuti mbalimbali za habari zilitumia picha hiyo zikiripoti tukio la moto lililotokea Mwezi Januari, 2025 Pacific Palisades, Los Angeles, California nchini Marekani.

Januari 10, 2025 tovuti ya VOA News ichapisha picha hiyo huku ikiambatanisha maelezo yanayosema "Katika mwonekano huu wa angani uliopigwa kutoka kwenye helikopta, nyumba zilizoteketea zinaonekana kutoka juu wakati wa moto wa Palisades karibu na kitongoji cha Pacific Palisades, Los Angeles, California, mnamo Januari 9, 2025.

Aidha NBC Los Angeles inaonesha video ya tukio hilo, iliyorekodiwa kwa ndege nyuki (Drone) na kueleza kuwa ni karibu na pwani ya Kaunti ya Los Angeles kwenye vilima vya kaskazini mashariki mwa Los Angeles.

Kwa mujibu wa CalFire, Moto wa Palisades pekee uliokuwa miongoni mwa milipuko mikubwa, uliingia katika historia kama moto wa kumi kwa kusababisha vifo vingi na wa tatu kwa uharibifu mkubwa zaidi nchini Marekani, ukiua watu 11, kuharibu zaidi ya majengo 6,500 na kuchoma zaidi ya ekari 23,000.








Bila shaka ni
Los Angeles (L.A)
California
 
Bila kupepesa macho majibu mengi niliyopata kupitia Google Reverse image search yanaonesha picha hii ni ya tukio la moto Los Angeles, California.
 
Back
Top Bottom