Picha 10 China waanza kutengeneza meli inayofanana na TITANIC

marcs

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
1,067
570
1480696543965.png



Meli ya Titanic iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast, iligonga mwamba wa barafu na kuzama Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500 ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.

Leo ikiwa ni takribani miaka mia na nne ‘104’ imepita tangu meli hiyo izame, China wameamua kujenga meli inayofanana na Titanic, habari kuhusu meli hiyo imewashangaza raia wengi wa China baada ya ujenzi huo wa meli hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269 kuanza.

Meli hiyo ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic, itakuwa na sehemu ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya watu maalum ambayo itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
1480696619328.png

1480696679852.png

1480696700142.png

1480696708642.png

1480696717732.png




Meli ya Titanic mwaka 1912 ilipokuwa ikifanya ikitoka Southampton ikielekea NewYork
1480696870812.png


Ujenzi huo wa meli hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269, itawekwa katika hifadhi iliyoko mashambani, katika mkoa wa Sichuan
1480696850342.png


Chakula kitakachotolewa kwenye meli hakitatofautiana na kile ambacho kilitolewa Meli ya Titanic 1912

1480696759882.png



Chumba cha gharama zaidi kitakuwa ni Yuan 100,000 , sawa takribani Tsh 31,521,912
1480696791412.png
 
Wachina bana ila kuna meli inaitwa OASIS OF THE SEA ni kubwa a mara tano ya titanic
 
Hii imekuja na kuipiku harmony mkuu fuatilia vema.Mi ninayo documentary hapa
Hiyo Oasis of the seas nimeiona kwa macho, wakati ikiondoka bandari ya Turku Finland ilipotengenezwa.Wakati huo ilikuwa ndio kubwa kuliko zote ila ilishapitwa
 
Back
Top Bottom