Physics against Geography... A level

Oxygen gas

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
248
250
Wakuu, habari za muda huu na heri ya mwaka mpya 2019.

Moja kwa moja tujikite katika mada hii kama inavyosema hapo juu.

Masomo tajwa hapo juu ni moja ya masomo yenye ukakasi katika ufaulu.

Inasemekana ufaulu wa Geo huwa mkubwa kwa madaraja ya C&D ukilinganisha na madaraja ya A&B ambayo ni magumu kupatikana katika somo hili la wana Geography.

Upande wa Physics ufaulu si mkubwa kwa upande wa wasitani lakini kwa madaraja ya A&B ni ya kuridhisha ukilinganisha na Geography ambayo kuchomoa "A" si lelemama.

Swali kwenu wadau wa Elimu Tanzania
1. Je kati ya Geog na Physics lipi somo gumu zaidi katika usomaji na ufaulu?
2. Kwanini madaraja ya A&B kwa Geography ni nadra kupata ukilinganisha na Physics
3. Wanafunzi wanaosoma Physics ni bora sana ukilinganisha na wale wa Geography?

Wale wote tuliosoma/tunaosoma PCB,PCM,PCB,PGM,EGM,HGL,HGE & HGK. Jooni tushee ideas.

Cc
 
ahmedjad

Member
Sep 5, 2018
41
125
Tatizo la geography vitu vingi inatakiwa ukariri hasa hasa physical geography ,pia kn vitu vichache vinavyohitaji uelewe.pia wanafunzi wengi wa geography huwa hawasomi geography 2 ambayo huwa wanahisig ni nyepesi lakin kiuhalisia ndo inayotuangushaga wanageographia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
man dunga

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
479
1,000
Physics huwezi linganisha na geography kwa ugumu. Physics ni somo gumu sio tu kuliko geography bali kuliko masomo yote.

Waliosoma au wanaosoma PCM, PCB na PGM wengi wao walikuwa vile vile wanayamudu masomo ya arts olevel kwa hiyo hao watu wanauelewa mpana wakati wale wa H kunani wengi wao olevel hawafaulu masomo ya sayansi kwa hiyo wengi uelewa wao unazidiwa na wanaochukua PCM,PCB, PGM. Na ndio maana ni mara nyingi mwanafunzi wa kidato cha 5 aliye PCB, PCM,PGM kuhamia HGE,HKL nk na kufaulu vizuri tu lakini ni nadra HKL, HGL kuhamia PCM au PCB.
 
Nini kinafanya hao PGM wasipige A ya Geography?
 
Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
6,135
2,000
Hivi unaanzaje kulinganisha Physics na Geography...?

Kimsingi Physics ni masomo mawili yaliyopamoja "two compounded subjects", yaani ni Mathematics na Logic, ukishindwa kimoja kati ya hivyo, basi Physics itakupashida.
 
Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
3,774
2,000
Geography advance sijui ina nini ile....
EGM Anaweza jikuta ana maisha mazuri kwenye Maths kuliko Geography pia Economics nayo ni mchawi kama alivyo kijukuu chake Geography hawasomeki kabisa.
Anyway, baada ya matokeo geographers hujifariji na masomo mengine tu kikubwa cheti kikiruhusu kufanya matikulasheni tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
10,660
2,000
Hiyo nayo ni point watu tunajikuta tunasoma juu juu tu tena kinachotuumiza case study nyingi za geography 2 Hatuzijui
Tatizo la geography vitu vingi inatakiwa ukariri hasa hasa physical geography ,pia kn vitu vichache vinavyohitaji uelewe.pia wanafunzi wengi wa geography huwa hawasomi geography 2 ambayo huwa wanahisig ni nyepesi lakin kiuhalisia ndo inayotuangushaga wanageographia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom