Photo:unyanyasaji wa watoto mashuleni

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Hii picha ni ya wanafunzi wa MUHEZA PRIMARY SCHOOL...jinsi gani wanavyowanyanyasa watoto wadogo namna hii
tena ni wanafunzi wa shule...hivi tunajenga tunabomoa?? Adhabu za namna hii ni za kukumea vilivyo

WAPI SERIKALI???

watoto.jpg
 
Ilichangia kutengeneza kizazi cha watu wazalendo na wakakamavu!
To be honest mimi sioni unyanyasaji wowote hapo. Mi naona heri adhabu ya aina hiyo kuliko kuchapwa viboko ingawa pia sipingi adhabu ya kumchapa mtoto viboko viwili, vitatu. Adhabu za namna hii ndizo zilizojenga ukakamavu kwa kizazi kilichokuwa na uzalendowa kweli kwaTanzania na kufanya mengi tu tunayoyajutia leo kama kuwatoa wareno na makaburu kusini na kuwaondoa waliokuwa wakiimezea mate nchi yetu kama kina Iddi Amin. Hata Biblia na Qurani zimehimiza adhabu kwa watoto, na waliopuuza ushsuri huo wamejikuta wakifanya yanayofanywa na wenzetu wa magharibi leo hii! Sina hajaa ya kuyaeleza humu maana yanatia kinyaa!
 
Mbaya sana, Mwalim achukuliwe hatua kali sana. Hakuna mtoto asiyefanya utukutu shuleni lakini hii adhabu ni kali sana kwa mtoto inawaathiri kiafya.
 
Kutoa adhabu ni sawa lakini kwa kiwango hicho cha kuwabebesha wanafunzi tofali

vichwani+kupiga magoti sikubaliani nayo kabisa! Huo ni ukatili! hakuna uzalendo

unaojengwa hapo. Nina mashaka na hao walimu! au ndio wale waliopewa ualimu fasta fasta
bila mafunzo ya msingi?
 
Sisi tulifanya sana hizi na ndio maana tuna nidhamu!mitoto ya siku hizi(majority),wamepinda balaa!!
 
safi sana hawa wanakomaa idi ikifika 2015 watasaidia sana kulinda kura za chadema zisiibiwe na magamba
 
Back
Top Bottom