Phobia? Selfishness, au Nini?

Unachoulizia wewe Mbu kwa mtizamo wangu jibu lake Ni Jealousy, ambayo ni the most dangerously feeling, Jealousy creates insecurity. Insecurity creates hatred, and hatred kills softly.

- jealousy?-

How possible bana unakuwa na wivu na spouse wako kiasi hiko cha kuzaa chuki za mafanikio yake?

How? Whyyyyy???
 
Last edited by a moderator:
hiyo kali!

but mie nafikiri unaweza usiyafurahie maendeleo ya mwenzi wako kama tu hayaleti baraka ktk mahusiano yenu.

yani kufanikiwa kwake badala yakufanya mahusiano yenu yastawi yanadorora.

mfano: kwa mwanaume kafanikiwa then anaishia kuhonga na kudhurura kwingi (haonekani)

mwanamke kafanikiwa anamdharau mumewe.

hapo kama ni mie sishindwi kuomba hata iyo kazi aipoteze, coz what we need is happinnes and mutual understanding na sio pesa.
 

umeelezea vyema kabisa Mr Rocky, na hii tabia wanaume sana ndio wanayo wakati mwingine anaweza akafanya juu chini mke afukuzwe kazi kabisa yote hii ni wivu na kutojiamini kwa mwanaume
 
Last edited by a moderator:


kutokujiamini
 
Last edited by a moderator:
Mtu akifikia hapo, basi hastahili kuitwa mwenza tena....

Mie nikipata hata msimbazi moja au nikatia ndani mchango wa King'asti basi hata bibi atashangilia...bila kusahau wajukuu!!

Na mambo yake yakiwa mswano basi wote tunashangilia na kuchelea...kwani siku hiyo lazima tupige bonge la dinner....

Sasa kweli huyo anayetaka kujinyoa eti kwa vile umefanikiwa atakuwa mwenza wako au ni kama wale wabaya wa Shemeji Ulimboka na Mzee Kibanda??

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:

Huo ni wivu tu mkuu hakuna lolote...anahisi kadri unavyofanikiwa ndivyo risk ya kukupoteza ukawa na mwingine ndivyo itavyoongezeka!!!
 
Reactions: Mbu
umeelezea vyema kabisa Mr Rocky, na hii tabia wanaume sana ndio wanayo wakati mwingine anaweza akafanya juu chini mke afukuzwe kazi kabisa yote hii ni wivu na kutojiamini kwa mwanaume

.......-wanaume wengi ndio wenye tabia hii-

Swahiba Dark City, Ponjoro na BADILI TABIA, naamini mmemsoma na kumuelewa Lady doctor!

Hata mimi namuunga mkono, maana so mara moja wala mbili kusikia migogoro ndani ya nyumba kisa mke "kala bingo!"

Hebu wanaume tujitafakari, nini tatizo...
 
Last edited by a moderator:
Hahahaha babu umenikumbusha. Naomba risiti yangu ya mchango lol.

Umenena vyema. Unajua ndo maana tunaambiwa upendo huvumilia yote na hauhesabu mabaya. Unaweza kukuta mwanzoni kila mmoja anafurahia mafanikio ya mwenzie. Lakini upendo ukipungua, kwa sababu mafanikio yanaweza kumpa mmoja uhuru binafsi, ama basi hakuna faida ya mafanikio kwa familia basi hata donge huanza.

Kuna shosti mumewe akitarajia ujira flani kutoka kazi zake binafsi basi yeye anakosa raha kabisa. Anajua manyanyaso yanakuja ni hadi hizo hela ziishe ndo mume atarudia ubinadamu.
 
Last edited by a moderator:
inawezekana kila ukifanikiwa family ndio inazidi kuwa na hali mbaya na mani inapotea, so madam anaona bora mbaki vilevile ili family iwe na amani. hayo ni maoni yangu tu
 
Reactions: Mbu
-insecurities.-

Hahahaha, kuna wengine wanafikia hata kuwauliza wake zao kama wamewahi kutongozwa, wakijibiwa "HAPANA!" Pia wana mind!

What's wrong with these insecurities?

Inawezekana labda there is nothing wrong with them. Some men insecurities are caused biologically.

Tena japokuwa kuna wanawake ambao wanadai kuwa hawapendi kuwa na mwanaume ambaye ni insecure, wapo wengine ambao wanapenda kuwa na mwanaume ambaye ni insecure hasa kama kwenye uhusiano uliopita mwanaume alikuwa all about himself, self-styled au alikuwa dependent kwake (mwanamke).

Wapo baadhi ya wanawake wanaoamini kuwa wanaume ambao siyo secure wako more sensitive and more interested into them (women), though it most believe that insecurity can seriously damage the relationship.
 

Yeah, wanaume lazima mtupe majibu ni kwa nini inakuwa hivyo? Kuna la ziada ukiacha kutokujiamini na wivu?
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu
......mnh, Husninyo wewe pia ni mmoja katika waoga?
Umeandika kwa uchungu sana mydear

hhhhhhhhaaaa!! Mbu mi mwenzio huwa nafunga na kusali kumuombea mafanikio maana mfuko wake ukitabasamu wakwangu unacheka. lol.
 
Last edited by a moderator:
hiyo ni roho ngumu na mbaya
hajipendi yeye kwanza
maana angejipenda angependa anaowapenda wafanikiwe
 
Reactions: Mbu



Mbona hii thread imekaa ki-CCM CCM, maana wao ndio hawataki watanzania waendelee, wao wanataka tukae kama mazezeta na kutupigia ngoma za Nape huko vijijini huku wakubwa wake wakila nchi bila hata jasho na huruma kwa watanzania.
 

Hii makitu inatokana na kutokujiamini mkuu
Watu wanataka waabudiwe kwa sababu wanadhani ni haki yao kufanyiwa hivyo
Na wanaamini kigezo kikubwa ni fedha,sasa wakiona mwingine anaelekea kupata iwe ni baba,mama,dada,mke,mume homa hupanda kwa kuwa wanaona ufalme umeisha!
 
Reactions: Mbu
-woga!-

Weye Lizzy weye.....
Sasa kama jamii yenyewe ishajikubalisha "mswahilu mpe cheo, au kipato!" Uyaone makucha yake...
Huoni kuna ugumu wa kumshawishi huyo spouse?

Ugumu upo ila kama ni woga tu unaomsumbua ukiweza kumtamkia kwamba hayo mafanikio yataboresha badala ya kuharibu ndoa yenu na matendo yakadhihirisha hilo utaona mwenyewe atakavyochanua. Ila kama kuna mengine, hapo sasa ndipo mtihani ulipo.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu
kama aliyepata promo ni KE ,kidume kitakua kinaogopa kumwagwa na kama ME most of the cases mbona inakua kawaida tu!!sema hii jinsia ya Eva inaweza hata badilisha kila kitu wakipanda vyeo dharau zinaongezeka n,k

na kama ni ME je???? nyumba ndogo zinaanza maana hela zinawasha unakuwa na nguvu zaidi
 
Reactions: Mbu
May be ni kutokujua utamu wa mafanikio ya mwenza wako.... lol!

Nakumbuka siku zileee chuo, "mtoto" alichaguliwa kuwa speaker kwenye bunge la chuo, mi nikiwa raia wa kawaida.....
Dah maisha yalikuwa matamu sana, maana sasa safari zote za madame speaker zilinihusu na ndio ikwaga mara yangu ya kwanza kufika Dodoma Bungeni na visafari vingine vingine mixer posho sijui visemina, basi bumu langu likawa linapumua sana lol

Dah ni raha hata kukumbuka tu japo mambo yameendelea sana siku hizi, nimejifunza kumuombea sana mafanikio mwenza wangu siku zijazo.

Whyyyyy???

Kujibu swali hili Mbu nadhani ni vile tu wengine wanajikuta hivyo labda kuhofia kumpoteza mwenzako, pia labda kwa kusemea upande wetu wanaume, wengine bado wana zile stereo type zimewakaa sana kuamini kuwa mwanamke siku zote anatakiwa awe chini.
Tiba ya hii kitu ni pale tu huyo "mwenza" anapopata mafanikio basi amuonyeshe mwenzie kuwa ulichokuwa unafikiria ni tofauti na haya mafanikio ni yetu sote..... Shida inakuja pale hii kitu inapopelekwa kiushindani na kumkomoa mwenzio....!

Pia...... uh ntaendelea bdae!
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…