Tumemuona hata Uturuki akiomba radhi kwa Mrusi kwa kitendo chake alichomfanyia Urusi, na hata hivi juzi waliingia mikataba ya kibiashara japo yeye ni NATO lakini kawapuuza wenzie kwa kitendo cha kumwekea Vikwazo Mrusi.
Na inaonyesha kwa sasa Mataifa mengine yatafuata nyao ya Rais Duterte kwa ujasiri aliuwafanya,
Sema kwa upande wa Africa bado tumelala kwa kuogopa kutopatiwa misaada, ila Burundi wamedhubutu kwa kujiondoa kwenye kichaka ICC kilichowekwa kwa ajili ya viongozi wa Africa.
Ni kweli mkuu, Rais wa Uturuki bila kutonywa na Putin kuhusu mpango wa Merikani wa kupindua Serikali yake na kumuua yeye, saa hizi angekuwa marehemu!! Awezi kusahau Putin na Urusi kwa kunusuru maisha yake.
Rais wa Uturuki amekwisha wekeana mkataba na Urusi kwa ajili ya kununua Air Defence System kutoka Urusi, wamekabaliana vile vile kujenga nuclear power reactor kwa ajili ya kuzalisha umeme, mambo ya utalii, Kampuni za ujenzi za Kituruki kwenda Urusi kuendelea na shughuli zao kama ilivyo kuwa mwanzo, uuzaji wa matunda na mboga mboga na kikubwa zaidi Uturuki imekubali bomba la gesi la Urusi kupitia nchini mwake kwenda Ulaya - makubaliano hayo yamemuhudhi Obama na wapambe wake, maanake uchochezi wote wa vita nchini Syria unao fanywa na Merikani na wapambe wake chanzo chake ni ujenzi wa bomba la gesi kutokea Qatar kwenda Ulaya kwa kupitia Syria.
Atittude za Uturuki 2wards Merikani kwa siku za karibuni huo ni mwanzo, Mataifa mengine nayo yatakuwa yanajitoa taratibu kutoka kwenye makucha ya Mayankee.
Linapo kuja suala la baadhi ya Waswahili wenzetu kuipigia debe Merikani ni kitu cha kushangaza kidogo, labda awajui historia ya siasa za Taifa hilo linavyo sababisha maafa yasiyo na kifani kwa baadhi ya Mataifa ya third World, awajui hata kama vurugu Sudani kusini mchochezi ni Merikani, kisa: mafuta na kuharibu kuwa contain Wachina nchini humo, juzi juzi hapa Serikali ya Ethiopia imeshutumu vikali Amerika kwa kusababisha/chochea ghasia nchini mwake - kisa? Wanajaribu kuzuia influence ya Wachina Barani Africa especially Ethiopia kwa kuwa China itahusisha Ethiopia kwenye mpango kabambe wa Silk Road.
Wachina wamewajengea reli Ethiopia kwenda Port Sudan, wali by pass Eritrea, reli hiyo itasaidia kuingizwa kwenye network ya reli za Silk road Project - lengo kuu la Project hiyo ni ku facilitate ufanyaji wa biashara na uchukuzi wa mizigo kutoka/kwenda Uchina, Urusi, Ulaya,mashariki ya kati na Africa kwa njia ya reli, mizigo inachukua siku chache kuliko usafiri wa meli.
Merikani inaogopa sana mpango huo wa kiuchumi maana wanajua mpango huo ukitekelezwa/fanikiwa hakuna ambaye atahangahika kujua kinacho endelea huko Merikani i.e Amerika haitakuwa na relevance yoyote Barani Ulaya, Middle East, Asia na Africa.
Hivi tunavyo zungumza majaribio ya mpango huo kabambe yamekwisha anza, train zinatoka Uchina kupitia Urusi na kuja Poland ndani ya wiki, kwa Africa nadhani itachukua wiki mbili!!