Philip Mangula: Wale wote walioshinda kwa Rushwa watashughulikiwa ndani ya Miezi 6 kuanzia sasa

Huyu mzee amedandia gari ya ccm kwa mbele.

Kazi anayo.

Viongozi wa ccm ni wasanii kuliko ze comedy.
 
"A chicken in every pot and a car in every garage" . .let's call it a day peopleeeeeeeeez!
 
Ccm haiishi vituko! Kila kiongozi anaahidi yake kabla haya thubutu kuyatekeleza anatulizwa halafu anaondoshwa maisha yanaendelea silly season next part inaendelea.

Nadhani wakati akisema hayo Nape alitema mate chini halafu akacheka kimoyo moyo maana kwa sasa Nape ni mzoefu kuliko mzee Mangula.
 
Nimemsikia mwenyekiti wa ccm bara akinadi sera hii kwangu mimi huu ndio mwisho wake utamtoa nani na utamuacha nani kwa hili labda wenzangu nambieni kaulio hii ni ya kweli au yaleyale ya kuvua gamba.


AKIMFUKUZA mwenyekiti wake, ataweza kurudisha CCM enzi za Mwalimu, CCM ya wanyonge. Vinginevyo hii ni season two, baada ila ya "kujivua gamba". Kip on watching!!!!
 
Mkuu hata mimi nimemsikia kupitia ITV na TBC akisema hayo maneno nikashtuka sana.
It is a good promise but very difficulty and risk task.

Sijui kama kauli hii inaweza kutekelezeka au anaweza kujenga chama?

Anyway miezi sita toka leo itaisha tarehe 17/May/2013, Mungu akitupa uzima, tutakuja hapa hapa JF kutoa feedback ya kauli yake.

Tunaomba hiyo video cript itunzwe You tube ili asije akakanusha siku akibanwa.
 
Mzee Man'gula atapata shida sana. Mimi nashangaa kwa nini amekubali hayo madaraka ilihali akijua uchafu wa siku nyingi wa CCM? Ama kweli madaraka matamu! Hivi anafikiri ataanzia wapi mbona wote ni wachafu hasa ukianzia zile enzi za kukwapua fedha za EPA wakati yeye mwenyewe akiwa Katibu Mkuu wa CCM? He must be dreaming a lot of illusions in him too bad.
 
How clean he was or he is?

How clean the system is?

Anataka kujaribu kukata tawi alilolikaliwa, sijui kama anajipenda kweli?
Let watch and wait.
 
Msimsingizie mzee wa watu, kwanza mwenyewe hana maneno mengi na wala nafasi aliyopewa ni ya heshima tu hana uwezo wa kumtoa mtu japo ni mjuzi sana wa kupanga mbinu. mwacheni arudishe mwili kwanza msimtilie doa.
Kama hujaangalia ITV si ukae kimya? Nani kamsingizia?
 
Mkama na mustashi zake kaishia kutema mate tu chini unachezea ccm! Mafisadi woote wanajificha ccm!
 
Nadhani tumpongeze na kumpa maneno ya kumuongoza ili lengo lake ambalo lazima linatokana na historia yake iliyotukuka aliyonayo anaweza kukirudisha chama mahali panapoelezeka tofauti na kilivyo sasa!
 
Tunasubiri siku 90 walizotoa kuvua Gamba zikifika hizo ndo zinaanza kuhesabiwa za kushughulikia wala rushwa. Naona tutasubiri sana
 
Inaonekana haifahamu CCM ya leo! Anadhani ni ileee yao ya zamani. Kwa kuanzia tu ataambiwa gari la kuendea kazi hana mpaka yule mfadhili akubali kumnunulia. Akiuliza vizuri aambiwe apate kibali cha kuagiziwa lake kutoka kwa R1. Baada ya hapo atalainika tu!
 
mwisho wa ccm umefika haraka zaidi ya ilivotarajiwa
Nimemsikia mwenyekiti
wa ccm bara akinadi sera hii kwangu mimi huu ndio mwisho wake utamtoa
nani na utamuacha nani kwa hili labda wenzangu nambieni kaulio hii ni ya
kweli au yaleyale ya kuvua gamba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom