Ntale Wi Isumbi
JF-Expert Member
- Apr 4, 2012
- 480
- 127
Hii cinema nyingine mpya ndani ya CCM. Mzee Mangula (wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa CCM) aliyemkataa JK waziwazi asipitishwe kugombea urais mwaka 2005 maana hakuwa safi na report za sekretariati za mikoa nyingi zilikuwa chafu juu yake. Baada ya JK kushika hatamu za chama akampiga chini ukatibu mkuu. Mzee Mangula akagombea uenyekiti wa chama Mkoa wa Iringa, mara mbili mfululizo JK anampiga chini. Leo JK huyo huyo anageuka na kumkumbuka hasimu wake mkubwa. Kuna nini nyuma ya pazia? Unahitaji akili ya ziada (sio ya binadamu wa kawaida) kuendelea kuwa mwana CCM na kushuhudia haya maajabu huku ukipiga makofi na kuimba nyimbo ambazo moyoni mwako huziamini. Sina uhakika hata kama ukichanganya na za mbayuwayu unaweza kuwaelewa hawa jamaa.