Ha ha ha ha Mkuu vioja.. naomba ninukuu gazeti la Mwananchi la leo.
Mbwete: Mpango wetu kwa Obama uko pale pale
Makamu Mkuu wa chuo kikuu huria Tanzania Profesa Tolly Mbwete amesema kuwa walichelewa kufanya mawasiliano na vyombo vinavyohusika na ili kupata fursa ya kumkabidhi Raisi ya Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kama walivyokuwa wamepanga.
Profesa Mbwete akizungumza kwa njia ya simu alisema kuwa, ingawa Raisi Obama ameondoka bado wana njia mbili za kuweza kumkabidhi cheti ikiwa ni ishara ya kumtunuku shahada hiyo.
"Yule ni mtu mkubwa bwana ingetakiwa tufanye mawasiliano ya kupata nafasi ya kumkabidhi kwa miezi mitatu kabla, hata hivyo hiyo shahada kwa maana halisi tulishampa kwa sababu Mkuu wa chuo ndo mwenye mamlaka ya kuitoa, kilichokuwa kinasuburiwa ni kumkabidhi cheti tu na yeye atoe hotuba ya kuikubali," alisema Profesa Mbwete.
Anasema kuwa, chuo hicho kitawasiliana na Ubalozi wa Marekani nchini ili kuona njia itakayotumiwa katika kumaliza mchakato huo.
Kwa sasa kuna njia mbili za kumkabidhi, sisi tunaweza kwenda ama kukituma cheti hicho kupitia ubalozi na yeye akatuma hotuba yake," alisema Profesa Mbwete.
​