Hivi utaratibu wa kutoa au kutunuku PhD ya heshima ukoje? Hivi hao wanaotoa hiyo PhD ya heshima kama waliweza kuwapa akina fulani wanashindwaje kumpa Babu wa Loliondo?
Kwani nani kasema Babu hawezi kupewa PhD ya heshima? Lakini hazitolewi kwa fujo namna hiyo. Mpaka mchango au manufaa ya mchango wa mtu kwa jamii yawe yamethibitishwa bila shaka. Nadhani bado ni mapema mno kwa Babu. Mchango wake bado una mashaka hata kama mamilioni ya watu wamefurika kwenda Loliondo. Ukitumia idadi ya watu tu kama kigezo hata waanzilishi wa DECI watastahili PhD.Fikiria hata nanihiii naye kapewa siku hizi anaitwa dokuta. basi na yeye apewe