PGM Ina shida gani Tanzania

Marekebisho kidogo ni Aeronautical engineering humo ndani ndiyo utakutana na hayo mambo ya aerodynamics.
 
Combination hii haina tofauti sana na PCM.

Hiyo imani
kuhusu ugumu wa combination hii unakuja hapo kwenue Geography.

Geography inadeviate mbali kidogo kimaudhui na yale masomo (physics na mathematics) mengine mawili yaliyojaa hesabu nyingi.

Geograph huitwa social science, haisomeki kama science pure kabisa. Hapo ndipo utofauti.

Sasa hyo combination ina science pure (physics) ina Geography (social science) then mathematics
.. Yani ni kama huwa hayana correlation hvi na inapelekea usomaji kuwa mgumu kdogo ukilinganisha na combination kama PCM.

Maelezo haya ni kulingana na baadhi ya wasomi wa comb hyo.

Ila naamini ni imani ya watu tu.
 
Wengi hawajui urubani ukiwa na hela tu unamsomesha mtoto
 
Ilikuwa chaguo langu la Pili baada ya PCM, then PCB.

Nilikuwa na ndoto ya kusomea Urubani, bahati mbaya Umasikini wa familia ulikatisha ndoto yangu.

Sasa tunajenga Barabara, Majengo bila kusahau kuwajengea miradi ya Maji.

Muhimu mkono uende kinywani
 
Wengi hawajui urubani ukiwa na hela tu unamsomesha mtoto
Na wengi hawajui pia kuwa Urubani hauna hela kama wanavyodai watu
Ni kweli kabisa,kuna madogo wakishua wamemalia laurent sasa hv marubani ,wa kawaida tu ,ujiko ni vile rubani dereva wa angani
 
Anaambiwa na nani, au kukariri kusoma pgm lengo kusoma urubani?
 
Kama Umechaguliwa PGM kwa kuichagua wewe kutoka moyoni nenda kasome, Mimi nimeisoma iyo combination katika mazingira magumu sana japo sikufaulu nilivyotaka ila sio kozi ngumu.

Pili kuhusu outcome ya utaenda wapi after hapo angalia roho yako inataka nini suala la pesa weka pembeni then angalia simirality, Engineering zote zina tabia ya kukutana sehemu moja ama ingine ivo jua waitaji nn then pitia hapo kuangalia uelekeo, mfano ukitaka soma robotics sio lazima ukasome course chuo inayoitwa ivo ila kuna electronics. mechanical, computer, mechatronics nk.

ivo suala la watu kusema ni ngumu au urubani ni wewe unatakaje ndio ufuate roho.

Mimi nimesoma iyo then nikaenda MUST nikasoma Mechatronics, then nikajisomea Embedded hardware na electronics then nikarudi urubani wa ndege ndogo almaarufu kama drone, then na design na ku manufacture drones kwa matumizi yangu mwenyewe. Nimekupa hayo maneno kukuhamasisha maana mimi ndoto zangu ni ilikuwa kupeleka kitu angani suala la mimi nitakuwepo ndani au la limetokana na factors za pesa na vingine ila ninaendelea kutimiza ndoto, naomba niishie hapo kwa sasa.
 
Yote kwa yote hongera nimesoma nimekuelewa vizuri kabisa, kimsingi hata mimi hiyo electronics niliisoma kama mimi na nikatumia gharama kubwa kununua vitu kwa ajili ya practical na vitu kama software ili hali niliisoma Mech.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…