Petrol na Diseli imekuwa adimu sana huku tulipo

Yenga08

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
464
891
Habari zenu wana janvi.,

Wenye kujua nini tatizo watujuze, maana kwa baadhi ya sehemu huku kanda ya Ziwa hususani sehemu za pembezoni na mjini Petrol na Diseli zimeadimika sana siku ya tatu leo.

Kuna baadhi ya Petrol station zimefunga hakuna mafuta. Kuna Petrol station moja inauza mafuta yasiyozidi kiasi cha 2000 tu, hata ukimwambia niwekee ya laki hakubali.

Wahusika wa hizi mambo fuatilieni maana vijiweni mpaka 4000 wanauza kwa lita moja ya petrol.
 
Namna ya kupandisha bei za bidhaa hyo mkuu,ulikuwa hujajua? Na bei hyo itaenea nchi nzima
 
Mamlaka ifatilie,hili tattizo kweli lipo,ni almost nchi nzima kuna mgomo baridi wa wafanyabiashara wa mafuta...
 
Habari zenu wana janvi.,
Wenye kujua nin tatizo watujuze, maana kwa baadhi ya sehem huku kanda ya ziwa hususai sehem za pembezon na mjini Petrol na Diseli zimeadimika sana siku ya tatu leo.

Kuna baadhi ya Petrol station zimefunga hakuna mafuta. Kuna Petrol station moja inauza mafuta yasiyozidi kiasi cha 2000 tu, hata ukimwambia niwekee ya laki hakubali.

Wahusika wa hizi mambo fuatilieni maana vijiweni mpaka 4000 wanauza kwa lita moja ya petrol.
Simzam hapo Burundi au Rwanda chap kwa haraka au nako mmeambiwa hayapo🤔
 
Back
Top Bottom