Peter Msigwa: Shoga hana tofauti na mtu anayetumia madaraka vibaya kuiba mali za umma kula rushwa kuonea watu kuteka na kuua watu na kudhibiti uhuru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
*NITAWATAJA MASHOGA HAWA*

Jamii yetu inapinga ushoga kwasababu moja tu ya msingi - ushoga ni kinyume cha maadili, sheria na ustaarabu wa nchi. Kwa msingi huo, Shoga hana tofauti na mwizi, muongo, muuaji, mlevi, mlafi, mzinzi na dikteta! Wote wanafanya mambo mabaya sana, ya aibu sana na yasiyokubalika.

Shoga hana tofauti na mtu anayetumia madaraka vibaya kuiba mali za umma, kula rushwa, kuonea watu, kuteka na kuua watu na kudhibiti uhuru wa watu.

Shoga hana tofauti yoyote ya msingi na mtu anayesigina katiba na asiyeheshimu utawala wa sheria, mwenye kiburi na majivuno ya kufanya atakavyo.
Hawa wote wanafanya mambo ya kishoga, yenye athari ile ile ya kuwa kinyume cha maadili, sheria na ustaarabu wa nchi. Na mambo yote hayo ni chukizo mbele za Mungu.
Hawa wote wamepungukiwa utukufu wa Mungu, na wanahitaji Neema yake!
Kwa hiyo, wakati tukiburuzwa tuwachukie mashoga wa maumbile, jinsia na tabia, tunapaswa kujua kuwa hata hawa wanaosigina Katiba, wasioheshimu utawala wa sheria, wanaoteka, kutesa na kuua watu, na wanaodhibiti uhuru wa kujieleza, kutoa maoni, kukosoa pamoja na kuminya uhuru wa vyombo vya habari, nao pia ni mashoga. Wanachofanya ni chukizo mbele za Mungu.

*Tofauti yao ni moja tu, mashoga hawa wameamua kuwa vinara wa kuhukumu mashoga wenzao*
Imeandikwa, usihukumu kabla ya kuhukumiwa.

Which ground are you standing to judge others
“Do not judge, or you too will be judged. For in the same way you judge others, you will be judged, and with the measure you use, it will be measured to you!

Ushoga ni zaidi ya kutenda ngono kinyume cha jinsia au kinyume cha maumbile, ushoga ni kwenda kinyume na maadili, sheria na ustaarabu.

*Mchezo wa kuhukumu na kutajataja wanaodaiwa kuwa mashoga wa kijinsia na kimaumbile ukizidi, na Mimi nitawataja kwa majina Mashoga wanaofanya udikteta, kusigina Katiba na kuonea watu*
Peter Msigwa
MP for Iringa Urban.
 
Aise kweli chadema siyo chama, SIKUTEGEMEA KABISA KAMA MTAKUJA KUTETEA USHOGA..... kumbe walivosema mnafadhiliwa na kile chama cha kijeruman kinachosaport ushoga hawakukosea kabisa. sasa mchungaji mzima unatetea ushoga kweli na kutaka kutuaminisha kuwa tuone sawa na matendo ayo ya ulafi na uongo?
 
Unakuta hata wapenzi wa video za ngono nao wanapinga ushoga!!!

Sijui ni dini gani inayoruhusu kutazama picha za ngono hata kama mko faragha!!

Unaweza kuta mtu hapa povu linamtoka kwa kupinga ushoga, lakini ukimpekua anakoishi; unaweza kumkuta na rundo la CD za ngono huku hana CD hata moja ya neno la Mungu!

Kwa hakika sisi binadamu ni viumbe wanafiki sana!!
 
Aise kweli chadema siyo chama, SIKUTEGEMEA KABISA KAMA MTAKUJA KUTETEA USHOGA..... kumbe walivosema mnafadhiliwa na kile chama cha kijeruman kinachosaport ushoga hawakukosea kabisa. sasa mchungaji mzima unatetea ushoga kweli na kutaka kutuaminisha kuwa tuone sawa na matendo ayo ya ulafi na uongo?
usijitekenye ukacheka mwenyewe jibu hoja
 
Tatizo hata hamuelewi mtu anamaanisha nini kukimbilia kulaumu for nothing

Unaweza kukuta mtu kama wewe ni mmojawapo wa wale maprofesa hata kuona hoja hujui

Aise kweli chadema siyo chama, SIKUTEGEMEA KABISA KAMA MTAKUJA KUTETEA USHOGA..... kumbe walivosema mnafadhiliwa na kile chama cha kijeruman kinachosaport ushoga hawakukosea kabisa. sasa mchungaji mzima unatetea ushoga kweli na kutaka kutuaminisha kuwa tuone sawa na matendo ayo ya ulafi na uongo?
 
Ni Shida kweli hizi siasa ni hatari
Aise kweli chadema siyo chama, SIKUTEGEMEA KABISA KAMA MTAKUJA KUTETEA USHOGA..... kumbe walivosema mnafadhiliwa na kile chama cha kijeruman kinachosaport ushoga hawakukosea kabisa. sasa mchungaji mzima unatetea ushoga kweli na kutaka kutuaminisha kuwa tuone sawa na matendo ayo ya ulafi na uongo?
 
Wapi katetea ushoga mkuu??

Back
Top Bottom