Peter Kibatala: Awashika pabaya polisi sakata la Gwajima

Kilaza

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
3,324
Reaction score
1,379
Wakuu

Kibatala ameandika hivi

Tumekubaliana kimsingi na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kama ifuatavyo;

1. Kwamba zoezi/hitaji la Askofu Josephat Gwajima kuwasilisha nyaraka kadhaa zilizoombwa na Jeshi hilo limesitishwa kusubiri utatuzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali/DPP kuhusu hoja za kisheria tulizotoa kuhusu zoezi/ hitaji hilo, nasi kujibiwa rasmi.

2. Kesho mnamo tarehe 16 April 2015 Askofu Josephat Gwajima hatafika Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam mpaka pale zoezi la (1) hapo juu litakapokamilika. Tutatoa taarifa zaidi huko mbeleni.

Law; one of the most beautiful things in the World.
........................

Professor Kilaza
 
wakuu

kibatala ameandika hivi

Kwa wale wote waliokuwa wakitupinga;
tumekubaliana na Police Kanda Maalum ya Dar
es Salaam kwamba Askofu Gwajima hata-report
Police wala kutakiwa kuwasilisha nyaraka yoyote
mpaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
itakapotoa maelekezo kwa Police kuhusu barua
yetu. Sheria siyo kukariri...tukutane high court

Usijali baadhi ya nyaraka atazipeleka kwa waziri CHIKAWE wizara ya mambo ya ndani ambako kisheria anatakiwa kuziwakilisha FROM TIME TO TIME kwa mujibu wa sheria za usajili wa makanisa.
Ripoti kama zinazoonyesha mali na madeni nk.zilizokaguliwa na wakaguzi na ripoti za utendaji wa kanisa.
HIzo huwa hazisubiri high court wala ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni za kisheria.Kama kagoma kutoa polisi atazitoa wizara ya mambo ya ndani.It Is not a big issue.Nadhani umemsikia Chikawe kasema wasiopeleka hizo taarifa wajiandae kufutiwa usajili.Wewe endelea tu kula hela za mteja wako kwa raha zako kama wakili.
 
namkubali sana kibatala lakini kwa hili advocates ethics n values naona zinampitia pembeni
 
Siku hizi miiko ya sheria hamna,minutes za kesi unazikuta fb,twitter ,Instagram ,JF n.k mbaya zaidi judgement bado

Ni kweli ila acha tu kwani pia itakuwa ni somo la uraia. Zamani polisi walikuwa wanafanya wapendavyo kwa kuwa watu hawakuwa na elimu ya uraia. Mimi mwenyewe nilidhani ni lazima uandike maelezo polisi, kumbe maelezo sahihi yanaandikwa mahakamani. Kitendo hicho cha polisi kimechangia sana idara hiyo kunuka rushwa kwani kila mtu akikamatwa na polisi wanafanya wapendavyo na kipigo juu ili useme wanachotaka wao. Leo hii polisi wasiojua sheria eti wanatangaza kupitia kamanda wa polisi kwamba wanataka mtuhumiwa alete vithibitisho polisi wao ni mahakama? Acha facebook waandike hata mitaani kwenye kuta kwamba polisi sio mahakamani na polisi haruhusiwi kutaka ushahidi kutoka kwa mtuhumiwa bila ridhaa yake bali ushahidi ukapatikane mahakamani. Bigup Kibatala.
 
Usijali baadhi ya nyaraka atazipeleka kwa waziri CHIKAWE wizara ya mambo ya ndani ambako kisheria anatakiwa kuziwakilisha FROM TIME TO TIME kwa mujibu wa sheria za usajili wa makanisa.
Ripoti kama zinazoonyesha mali na madeni nk.zilizokaguliwa na wakaguzi na ripoti za utendaji wa kanisa.
HIzo huwa hazisubiri high court wala ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni za kisheria.Kama kagoma kutoa polisi atazitoa wizara ya mambo ya ndani.It Is not a big issue.Nadhani umemsikia Chikawe kasema wasiopeleka hizo taarifa wajiandae kufutiwa usajili.Wewe endelea tu kula hela za mteja wako kwa raha zako kama wakili.
,,,then inagundulika kuwa kanisa lake halijasajiliwa kama wanavyotaka ionekane, ni nani ataabika!?
Maana tangia Ubungo mpaka Kawe amekuwa akuiendesha shughuli zake wazi na mchana kweupee kwa miaka kadhaa huku mawaziri na dignitaries wengine wakienda pale lakini haikuonekana kama kulikuwa na shida!

We tafuta glass ya juice jinywee taratibu.Utayajua muda si mrefu.Subira yavuta heri.
 
Ukiacha mbali masuala ya kisheria, Gwajima hawezi kujiamini kuziwasilisha tu ili watu wawe naye kiimani (sio kisheria)?
 
Hongera Mh. Kibatala. Kitaeleweka tu kwa police. Tujiulize, ni watu wangapi tena maskini wanaonewa na police kwa kubambikiziwa kesi za kipuuzi.

wakuu

kibatala ameandika hivi

Kwa wale wote waliokuwa wakitupinga;
tumekubaliana na Police Kanda Maalum ya Dar
es Salaam kwamba Askofu Gwajima hata-report
Police wala kutakiwa kuwasilisha nyaraka yoyote
mpaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
itakapotoa maelekezo kwa Police kuhusu barua
yetu. Sheria siyo kukariri...tukutane high court
 
Kibatala naye apunguze promo. Anajitangaza kuliko alivyo. Atakiuka hata miiko ya uwakili ya kujitangaza
Hapana sikubaliani na wewe mkuu. Dunia imebadilika na hata sisi vikongwe tunajitahidi kuendana nayo hivyo hivyo. Kama mtu hayuko tayari kwenda na wakati, hana wa kumlaumu. The yesterdays are gone and will never come back. Hebu fikiria hapa Tanzania kuna watu bado wanafikiria kupiga marufuku mitandao wakiamini wanaweza kuizuia tsunami kwa mikono. Angalia kesi zilizoko mahakamani zinavyojadiliwa ulimwenguni na kwenye mitandao isipokuwa hapa Tanzania...yaani hata kwa mambo ya kipuuzi tumetia fora! Heko Kibatala, zidi kuwaelimisha wananchi kupitia mtandao.
 
Ukiacha mbali masuala ya kisheria, Gwajima hawezi kujiamini kuziwasilisha tu ili watu wawe naye kiimani (sio kisheria)?

Huu ushauri ni mzuri tena wa maana na waweza mjengea credibility kubwa.Kukataa kuzitoa kunamshushia credibility kwamba hayuko vile anadai yuko sababu kutoa documents si kitu kigumu.Na mimi nashangaa kuona anakodi hadi mawakili asipeleke documents!!! There is something fishy somewhere
 
Usijali baadhi ya nyaraka atazipeleka kwa waziri CHIKAWE wizara ya mambo ya ndani ambako kisheria anatakiwa kuziwakilisha FROM TIME TO TIME kwa mujibu wa sheria za usajili wa makanisa.
Ripoti kama zinazoonyesha mali na madeni nk.zilizokaguliwa na wakaguzi na ripoti za utendaji wa kanisa.
HIzo huwa hazisubiri high court wala ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni za kisheria.Kama kagoma kutoa polisi atazitoa wizara ya mambo ya ndani.It Is not a big issue.Nadhani umemsikia Chikawe kasema wasiopeleka hizo taarifa wajiandae kufutiwa usajili.Wewe endelea tu kula hela za mteja wako kwa raha zako kama wakili.
Chikawe? Huyu huyu msema chochote?
Tell me one thing alichowahi kufanya huyu jamaa!!...akiwa solo au akiwa serikalini......JUST ONE DAMN THING.
 
Kibatala naye apunguze promo. Anajitangaza kuliko alivyo. Atakiuka hata miiko ya uwakili ya kujitangaza

Yaah...nakubaliana na wewe. Bora atumie word of mouth promotion. At least he can stay safe when some decide to roll the stone.
 
Hapana sikubaliani na wewe mkuu. Dunia imebadilika na hata sisi vikongwe tunajitahidi kuendana nayo hivyo hivyo. Kama mtu hayuko tayari kwenda na wakati, hana wa kumlaumu. The yesterdays are gone and will never come back. Hebu fikiria hapa Tanzania kuna watu bado wanafikiria kupiga marufuku mitandao wakiamini wanaweza kuizuia tsunami kwa mikono. Angalia kesi zilizoko mahakamani zinavyojadiliwa ulimwenguni na kwenye mitandao isipokuwa hapa Tanzania...yaani hata kwa mambo ya kipuuzi tumetia fora! Heko Kibatala, zidi kuwaelimisha wananchi kupitia mtandao.
Tumuulize kwani ile kesi ya Oscar Pistorius ilikuaje?
 
Back
Top Bottom