Pete ya uchumba ipoje?

Shabdullah

Member
Feb 17, 2020
65
52
Habari kaka na ndugu zangu,

Nimekuja na swali kwenu wanajukwaa nataka kujua kuhusu pete ya uchumba. Sasa nimeingia kwenye penzi la kweli na tunahitaji kuvishana pete ya uchumba. Binafsi mimi ni mgeni sana kwenye suala la pete, sijui hata naanzia wapi, mpaka najiuliza, kwani pete yenyewe inasemaje kuhusu mimi.

Kuna maswali mengi najiuliza kuhusu pete hio ya uchumba. Nataka kijua kua:-

Pete hii ina utofauti gani na pete nyengine kimuonekano?

Je, inavalishwaje, ni lazima kupiga magoti, ni lazima mbele za watu. (Inahitaji sehemu maalumu)

Je, nilazima nivae popote niendapo au nilipo?

Je, pete hii ina gharama gani (bei yake)?

Faida ya pete hii ni ipi? (mimi najua ni alama ya uchumba).

Hasara ya pete hii ni ipi?

Na jamii inakuonaje ukivaa pete hii.

Wanajukwaa hili naomba msaada wa maswali yangu haya nataka nijue ili nijue nafanya nn?
 
Hongera sana,ila jitahidi usitumie gharama sana mwenye masuala hayo,utaja umia baadae kama huna uvumilivu.Wanawake hatukumbukagi gharama mlizotumia tukiolewa.(Just keep in your mind what i tell u,pleasee)
Wanaume huwa hatuna haja na sherehe ya ndoa, ile ni kitu ya wanawake. Kikao cha mwisho cha wanaume ngazi ya taifa, tumeazimia kuanzisha mjadala wa kuhamishia gharama za harusi kwa mwanamke na familia yake. Ili mkiwa katika ndoa muwe serious sababu pesa zenu na familia zenu ndizo zimetumika. Na pia kiherehere cha kutupangia tufanye sherehe za gharama kitaisha.
 
1. Pete hii ina utofauti gani na pete nyengine kimuonekano?

2. Je, inavalishwaje, ni lazima kupiga magoti, ni lazima mbele za watu. (Inahitaji sehemu maalumu)

3. Je, nilazima nivae popote niendapo au nilipo?

4. Je, pete hii ina gharama gani (bei yake)?

5. Faida ya pete hii ni ipi? (mimi najua ni alama ya uchumba).

5. Hasara ya pete hii ni ipi?

6. Na jamii inakuonaje ukivaa pete hii.

1. Tofauti ya pete hii na pete ya ndoa ni kwamba hii hua inakua na "jiwe" kama tanzanite, diamond japo nyingi zina chupa.

2. Kumvalisha mchumba pete mbele za watu ni ushamba na gharama zisizo na sababu. Ile inatakiwa ifanywe sapraiz. Hayo mengine ni mbwembwe tu.

3. Kama wewe ni mwanamke ni vizuri uivae ili theoretically wanaume wasikutongoze

4. Gharama inategemea na material kama ni silver, gold, shaba au bati

5. Hasara ni pesa unazoilipia

6. Jamii inakuona unanyodo na wengi wanasema "mtaachana tu". Pia ukishavalishwa ile watu wanaanza kusubiria harusi sasa ikipita miaka ndio maneno yanaanza.
 
Aise hiv alieanzisha huu utamaduni alitoka wap? Kwanza nn maana yake? Kusudi lake hasa ni lipi?

Ebu acha ulimbukeni kama upo serious nae katoe posa kwao
 
Pete ya uchumba huwa na stone juu kama hii hapa. Unaweza kumvalisha pete ya dhahabu gram 3 kwa 450,000 tu.
Screenshot_20200809-234347_Pinterest.jpg
 
sio kwa utandawazi huu wa sasa utakufa kwa stree tu uwaachi watu wale kwa bure
upendo hauko kweny materials things nikujidanganya hko

Mkuu kama unampenda mgharamie mnunulie hata iphone 12 pro max freshy tu. Kumbuka anakuja kukuzalia watoto uyo
 
Hongera sana,ila jitahidi usitumie gharama sana mwenye masuala hayo,utaja umia baadae kama huna uvumilivu.Wanawake hatukumbukagi gharama mlizotumia tukiolewa.(Just keep in your mind what i tell u,pleasee)
🤔
 
Pete nzuri anzia 1.2m ya Tanzanite
Unamvisha Pete ya hela ndefu 1.2m alaf washenz wanapiga tackel zao kazaa wife anawah kukupikia na amevaa bado Pete,hapo ndo utajua hujui,mi nakumbuka nilinunua Pete ya uchumba ya elf 10000 na box ya Pete ikakamilika 15000maisha yakaenda fresh,all in all acha kutumia gharama zisizo za msingi,kama unashida sana ya Pete nenda kwa sonara nunua Pete ya 10000 tupia silver hata gram 2 inatosha mengine tukutane ukileta mrejesho wa kuomba msaada kama wanakupasulia au vp,nakusalimia kwa jina la jamuhuri.............kazi iendeleee
 
NAUNGA MKONO HOJA
 
Msimpangie mtu anunue nn, kila mtu ana maamuzi yake na kipato chake. Kuchapiwa kupo tu kwani wewe huchapi wa wenzako??
 
Back
Top Bottom