Pete ya Ndoa na kidole maalum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pete ya Ndoa na kidole maalum

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by pilau, Sep 8, 2012.

 1. p

  pilau JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Waungwana nini sababu ya PETE ya ndoa kuvikwa kaika kidole maalum, kinachoitwa kidole cha pete? au hii ni katika hali ya kuiga ustaarabu wa wenzetu wa magharibi? Wachungaji Mapadre na Mashekh na wale ma MC hawaelezei maana halisi ya wanandoa kuvishana pete katika kidole hicho kwa nini mtu asiveshwe kwenye kidole Gumba???? Wana JF Pamoja na michango na michanganuo kuhusu mada hii lakini kama kuna daktari au mwana bailojia naomba anifahamishe .......... nimeambiwa kuwa ........ asili na chanzo kikuu cha PETE YA NDOA kuwa na kidole maalumu ni kwamba kidole kinachoveshwa mkono wa kushoto kina mshipa uluokwenda moja kwa moja katika moyo wa binadamu, hivyo kuvesha pete katika kidole hicho ni ishara ya upendo wa mke na mume katika mahusiano ya ndoa ambao unaunganishwa na moyo wa kila mmoja kupitia ishara ya PETE narudia wana baiolojia na madaktari wanaojua ukweli kusu hili wanisaidie!
   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  I wish ningeweza demostrate kwa video, ila ngoja nijaribu!

  Unganisha palms zako, vidole viendane, yaani kidole cha kati cha kushoto kigusane na cha kulia cha kati!

  Vikunje vidole vya kati peke yake!

  Vikiwa hivyo hivyo vimekunjwa, Jaribu kuachanisha vidole vidogo, utaweza, gumba (piece of cake), vya kupointia pia utaweza lkn huwezi achanisha vidole vya pete kama vidole vya kati vikiwa vimekunjwa. Hiyo inasymbolize kuwa marriage hazipaswi kutenganishwa na kama vile kidole cha pete usivyoweza tenganisha na kidole cha mkono wa kulia.

  Source: padre mmoja wakati wa mahubiri ya ndoa!
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kidole ni kidole tu hata ukiamua kuivaa kwenye vidole vya miguu haibadilishi kuwa huyo ulofunga nae ndoa mna agano la milele(kwa wakristu)........... sema yapendeza zaidi kuvaa kidole hicho....na pia mapokeo.... ingekua mapokeo pete huvaliwa kidole gumba hata kizazi iki kingepokea hivyo...
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Hii kitu ishawahi kuwekwa hapa jamvini siku za nyuma na niliijibu kama ulivyojibu with illustration.
  Ngoja niisake hiyo post,then niiweke hapa tena
   
 5. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Hivi ndivyo nilijibu last time

  Pia kuna hii nadharia:

  *kidole Gumba = kinawakilisha wazazi wako
  *Kidole kinachofuata baada ya gumba = Kinawakilisha ndugu wa tumbo moja
  *Kidole cha katikati = kinakuwakilisha wewe mwenyewe (binafsi)
  *Kidole cha nne = kinawakilisha mwenzi wa maisha
  *Kidole kidogo cha mwisho = kinawakilisha watoto wako

  Sasa jaribu kufanya hili zoezi dogo ili tuhakiki hiyo nadharia:

  [​IMG]

  Kutanisha vidole vya mikono yako kama ambavyo inaonekana katika hiyo picha hapo juu.

  1. Jaribu kuachanisha ncha za vidole gumba (wazazi), utagundua vinaachana - Maana yake hutaishi na wazazi wako milele

  2. Jaribu zoezi hilo kwa vidole vinavyofuata (ndugu), utagundua vinaachana - Maana yake hutaishi na nduguzo milele, kaka na dada zako watakuwa na maisha yao binafsi.

  3. Jaribu kuachanisha kwa vidole vidogo vya mwisho (watoto), utagundua vinaachana - Maana yake hutaishi na wanao milele maana nao watakua na kuolewa au kuoa.

  4. Mwisho, jaribu kuachanisha vidole vya PETE (mwenza), hahahah hutaweza ndugu maana hivyo vilishaandaliwa kuwa pamoja daima milele, maana yake mke na mume wataishi milele na hakuna cha kuwatenganisha. Na hii ndio sababu tunavaa pete kwenye kidole cha NNE.

  "Don't hesitate to hit the like button for this clue"
   
 6. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  DIDINT KNEW THIS!daaah!nimejaribuje kuvitenganisha vimegoma i see!safi sana hii!ngoja nitaitoa kwa wanangu wa ndoa manake wananidatisha kweli kuwa wanataka kuachana wakti ndo kwanza hata gauni nililowasimamia ndoa yao hata halojanibana yani ni ndoa ya mwaka jana tu!
   
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  watu 8 ameshakusaidia kuillustrate mwayego!dah nimeipenda i see!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  wajukuu washakuletea?
   
 9. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  hawajanileta bado mkuu!yani hizi ndoa siku hizi pasua kichwa kuliko maelezo!
   
 10. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Me too, nilivyoisikia kwa mara ya kwanza!

  watu8 thanks, nitakuLIKE nikingia PC; nikumbushe lkn!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Labda wanaona mama sista duh still hataki kuitwa bibi now
  wape habari unasubiri mjukuu itawasaidia kuelewana
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Ngoja niwaambie hii ambayo hamtaipenda:Wakati wa utawala wa Babeli,kulikua na imani ya kipagani,walikua wanaabudu sayari pamoja na nyota,hivyo walikua na miungu wengi,walikua 36,mungu mkuu alikua jua na alikua ana siku yake maalum ya kuabudiwa.Lakini pia miungu hii ilikua na alama tofauti ya kumuwakilisha kila mungu.Mungu jua ambae ndie alikua mkuu aliwakilishwa na alama ya circle,hivyo waumini hao walikua wanaivaa kidoleni kuonesha imani yao.Pete ilikua inavaliwa tangu nyakati hizo na ziliingizwa kwenye masuala ya ndoa na ibada ikipewa tafsiri kivuli lakini hiyo ni ishara ya imani kwa mungu jua.Hivyo ni upagani!
   
 13. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  na kweli inawezekana wananichukulia poa enh!itabidi ninze kutilia mkazo swala wa mjukuu sasa manake wanantia presha mimi kila siku kesi,binti juzi natoka kwenye send off namkuta kajaa tele chumbani kwa binti yangu analiaa hataki kurudi kwa mumewe,nikiuliza wala sipati jibu la kuleweka zaidi ya kunitaka nimpeleke kwa padri avunje ndoa ,kidgo nimwashe vibao,nilikuwa na tundovu kichwani kama vinne hiv,nikaona ngoja mr ampigie simu mumewe kuwa yupo huku!tukalala asubuhi namwuliza wala hanipi maelezo ya kueleweka imebidi tumtafute mumewe kesho kwa maelezo zaidi!
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Like hell hatuipendi na binafsi nimechoose kutoiamini my dearest but not so humble Eiyer!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  not yet. kwa nini nikunje vidole vya kati? what is the logic?
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Sasa inabidi mumewe apate twisheni
  Au ni wale watoto wa vi memo?
  hata mke atahitaji kupewa ki memo afanye nini lol
   
 17. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hata nikikunja vidole vidogo in inside out, bado ni ngumu kuachiana...kwa hiyo, kidole ni kidole, chochote can serve the purpose.
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kuna wengine watauliza ulazima wa pete ya ndoa kwanza kabla ya kidole cha kuvaliwa.

  Usipovaa pete ya ndoa ndio "ndoa haitadumu?"

  Na mantiki yake ni nini?
   
 19. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  na hiyo twisheni kijana namleta kwako The Boss kishakwa mtambuzi halafu kwa dark city halafu kwa pacha wangu Snowballna binti nampeleka kwa teacher mwalimu gfsonwin halafu mwali kishanyumba kubwa then kwa dadangu wa kingoni Fixed point
   
 20. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Zinavunjika kama zinavyofungwa pamoja na white gold rings!

  Nafikiri kwa maisha ya sasa, pete ya ndoa husaidia kusema kwa nguvu kuwa "I am not available" basi, ingawa bado kutangaza huko hakumfanyi mtu kuwa unavailable if s/he want to be 'available'.

  Mwisho wa siku twaweza sema ni utamaduni tu na ibada/ritual kwa baadhi ya madhehebu!
   
Loading...