pete wapendazo wadada na mabinti.

pete wapendazo wadada na mabinti.

kuna wale wauza urembo kwenye vikapu huwa wanapita mitaani, wasubiri hao mkuu utapata ya buku nadhani. haya mambo nadhani huyawezi mweleze tu mchumba kuwa huna uwezo asubiri pete ya ndoa ambayo na kwa 70,000 hutapata.

asante kaka, pete ya ndoa haisumbui ata milion. Ok ntamwambia ukwel kuwa uwezo wangu unaishia hapo. AMA KWELI MAPENZI NA PESA HAVITENGANI.
 
ongeza namba wewe au unampango wa kuwavisha wangapi... kwa sababu ninyi amchelewi kuvisha hata kumi?

ha ha ha! Umenifurahisha. Nataka kumvisha mmoja, tatizo mabinti hawaaminiki unamvisha pete ya lak2, ata wiki2 nyingi kashasepa. Angalau elfu70 ata akisepa nitaumia kumkosa yeye na si pesa.
 
Kama kwelibwampenda basi hutijali gharama bali utamjali yy, haijalishi umemkosa ama vipi
 
nataka kumvisha pete mpenzi wangu, nimeaanda 20,000/=. Je ni pete rangi gani ambazo mabinti wanazipenda zaidi? Msaada wenu wanajamvi. Asanteni!

mpe tu hiyo elfu ishirini akajitaftie zake bikini swafiii cassandra. au sio Preta?
 
Last edited by a moderator:
acha mashaka,jiridhishe kwanza............
ring-exchange.jpg

 
ha ha ha! Umenifurahisha. Nataka kumvisha mmoja, tatizo mabinti hawaaminiki unamvisha pete ya lak2, ata wiki2 nyingi kashasepa. Angalau elfu70 ata akisepa nitaumia kumkosa yeye na si pesa.

acha ubaili wewe yani tuachane nishindwe hata kuuza nikapata laki moja na nusu..
 
Unatakiwa kujua huyo mpenzi wako anathamani gani kwako! Ukijua hilo haitakusumbua kichwa ununue Pete ya thamani gani!!
 
duuuuuh 20000??????????????hiyo pete ya mfano?au pete nayojua mimi?....ongeza hela urudi humu nikutumie pete za kueleweka...
 
we kaka kiboko, kama umefosiwa, na sie wadada tuache kulazimisha vitu jamani
 
Kwani lazima umvalishe Pete ya uchumba hata kama uwezo huna?? fuata taratibu za kujitambulisha nyumbani kwao acha mambo ya kuiga!
 
Za ring ndo zikoje?

bht nakumiss wewe umenitupa kabisa aise
Yaani kimya kimya tuu unapita huku
Ring ni zile za kimachinga bana ambazo ukioga nazo ule mng'ao wake unapotea hapo hapo
Maana kama anataka pete haswa dah ajiandae kutoboka mfuko na sio hiyo 20
Kwani anataka amvike pete akae miaka kumi ndo aje kuoa au inakuwaje
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: bht
Imebidi nicheke tu jamani..kwa comment za wadau..binafsi ninachokushauri mkuu usivunjike moyo! kaa nae mshauriane tena..muweke wazi kuhusu bajeti yako..
 
Back
Top Bottom