Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,315
- 72,740
Kumekuwa na upotoshaji wa makusudi kutoka kwa watu wa kitengo cha propaganda cha ccm kuwa kunyimwa fedha za msaada za MCC kuwa ni serikali kukataa kunyenyekea misaada kwa vile inaelekea katika kujitegemea na inaboresha makusanyo.
Huu ni uongo wa wazi, tumenyimwa fedha hizo ambazo tayari tulisha ziweka kwenye budget yetu ya Maendeleo na kutamba kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwa sababu serikali imeshindwa kutekeleza shari la kuheshimu demokrasia kule Zanzibar na kurekebisha sheria kandamizi ya mitandao.
Ukweli kati ya serikali yetu na hiyo ya USA anayetetea watu wetu wanyonge hapo atakuwa USA. Vyama vya siasa vimejaribu kupiga kelele lakini kwa vile havina rungu la kulazimisha vineshindwa sasa wenye rungu wametumia.
Ni kweli mambo ya ndani hayatakiwi kuingiliwa, lakini ni yale ya haki na kujipangia maendeleo sio ukandamizaji. Familia jirani yako huwezi kuiingilia katika mipango yake ya elimu,afya na mengineyo lakini huwezi ona anachinja watoto na mkamuacha eti hayo ni mambo yake ya ndani.
Wananchi waelimishwe kuwa ukandamizaji wa demokrasia ndio uliokosesha fedha hizo za maendeleo na athari zake ni zipi. Misaada katika development expenditure budget sio jambo la ajabu duniani, bali nchi kama hata recurrent exp inategemea wahisani hiyo ndio aibu.
Bado sana tutaendelea kuhitaji misaada ya miradi ya maendeleo sio fedha tuu bali hata utaalam.
Hili la MCC serikali kwa kumbeba Shein inechemsha