Pesa ni zaidi ya kile tunachokifikiria

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,565
8,427
Katika mgahawa wa hadhi ya chini kabisa nikiwa nakunywa chai, ameingia mtu mmoja tajiri mkubwa tu wa mashamba na hotel ya kulaza wageni, ameagiza chai na chapati moja, baada ya kumaliza ameagiza maji ya kunywa ya kawaida na yamechotwa kwenye diaba likiwa pembeni yangu la maji ya kisima, akapiga kikombe kizima cha plastiki, akalipa TSH 1000, akasepa.

PESA ni zaidi ya kile tufikiriacho

NB: Pesa inampa mtu amani lakini pia haitatui kila kitu kwenye maisha ya binadamu
 
Sijaelewa unataka kutupa ujumbe Gani mkuu? Au ulitaka ale kuku nusu na chapati 5!! Maskini tu wanakula Kula sana kuondoa stress tu, mi nikawa kwenye kazi zinazoniingizia pesa aisee hata njaa hua siskii, ukiwa na milioni kwenye wallet njaa itatoka wapi sheikh

Hapo kwenye maji Kuna waliozoea tu kunywa ya Bomba mkuu kwa io sioni kesi
 
Kuna Mzee mmoja ni tajiri sana, ana mahoteli ya nyota nne nk,lakini siku moja aliwahi kula ugali maharage kwenye sahani ya plastic, nje alikuwa amepaki cruiser yake.

Huyu ni mtu ambaye ana uwezo wa kula popote chakula cha bei au kwenda hotelini kwake akala chakula chochote, Airport ana ndege yake

Lakini alikaa na sisi akala ugali maharage, sometimes huwa wanatamani kuishi kama wengine tu, ukiwa na pesa nyingi vyakula inakua sio hobby yako
 
Ni uamuzi wake.
 
"Kutimiza malengo" ni danganya toto tu.

Inamaana akina Jeff Bezzos, Bill Gates, Mackzugeberck, Dangote n.k bado tu hawajatimiza malengo kwa ukwasi walionao?
 
Hii wanayo sana matajiri wa kisukuma hawanaga complications kabisa na wako humble sana, kuna mmoja yeye alikuwa anakula na mashamba boy kwenye shamba lake la kunenepesha ng'ombe ule ugali mgumu kabisa na dagaa chukuchuku tena kwenye sahani moja na story zinaendelea kwa lugha ya kisukuma. Unaona kabisa tajiri kajishusha kwenye hadhi ya mashamba boy na kuonekana kama ni mwenzao kabisa pamoja pia na kumiliki hotel kadhaa za hadhi ya juu jijini, na pia atanunua mahindi ya kuchoma na kutafuna tu huko barabarani.​
 
Maskini ndio huwa wanazuzuka na hela sana kuliko matajiri.

Elewa somo, tajiri hata akiwa hana hela siku hizo hapati tabu ambazo maskini anapata. Lakini maskini anapataga tabu akiwa hana hela na hata akiwanazo kwake bado ni tabu tupu.

Imagine maskini akapata hela anataka ale pilau nyama kila siku na soda. Baada ya mda mfupi anaanza kudili na matatizo ya kijinga kabisa! Eti kweli mtu anapelekwa hospitali kwa kisa cha kushindwa kunya.
 
Sijaelewa unataka kutupa ujumbe Gani mkuu? Au ulitaka ale kuku nusu na chapati 5!! Maskini tu wanakula Kula sana kuondoa stress tu, mi nikawa kwenye kazi zinazoniingizia pesa aisee hata njaa hua siskii, ukiwa na milioni kwenye wallet njaa itatoka wapi sheikh

Hapo kwenye maji Kuna waliozoea tu kunywa ya Bomba mkuu kwa io sioni kesi
Labda hujajua jinsi pesa inavyo wapelekesha watu, nimemtafisiri kama mtu anaye hitaji kukua zaidi ya hapo alipo kiuchumi, pia ni mtu mwenye maamuzi magumu kuamua kutumia kidogo zaidi ya kikubwa alicho nacho, inafundisha watu ya kwamba kutapanya pesa kununua nunua vitu vya gharama ni kutengeneza umasikini wa kizazi chako baadae, mtu anaifikiria shilingi elfu moja ya kwamba aitunze ataitumia baada ya miaka 20 akiwa mzee au itawasaidia watoto wake wasije kinywanyaswa na watu kwa umasikini wao. Nimeona ni mtu mwenye kuichukulia poa pesa, na hajifananishi na wenye hadhi kimatumizi, inafundisha namna ya kukua kiuchumi japo ni ngumu Kwa maamuzi ya wengi
 
Kuna Mzee mmoja ni tajiri sana, ana mahoteli ya nyota nne nk,lakini siku moja aliwahi kula ugali maharage kwenye sahani ya plastic, nje alikuwa amepaki cruiser yake.

Huyu ni mtu ambaye ana uwezo wa kula popote chakula cha bei au kwenda hotelini kwake akala chakula chochote, Airport ana ndege yake

Lakini alikaa na sisi akala ugali maharage, sometimes huwa wanatamani kuishi kama wengine tu, ukiwa na pesa nyingi vyakula inakua sio hobby yako
Uko sawa kabisa
 
Back
Top Bottom